Je, Tanzania tuna Media Freedom kubwa kuliko UK na US? Tushuhudie kitachompata Julian Assange wa WikiLeaks! Tujifunze kwake

Mkuu Joka Kuu, heshima mbele.
Amini usiami kwa Tanzania tatizo ni letu sisi waandishi, wala usiende mbali hadi ulaya kwa Asange, nenda tu hapo jirani zetu Kenya kwa Mohammed Amin na Jicho Pevu, sisi tunashindwa nini?.
Nimesema waandishi wetu wengi ni reporters tuu kazi kubwa ya media zetu ni kuripoti matukio na pressvm conferences, mikutano, semina, warsha na makongamano. Hutuzami deep na hatuna competent team za kufanya IJ.

Tangu awamu ya 5 imeingia madarakani, fungu la Vote 20, ndilo linaloongoza kuchota fedha hazina bila ya idhini ya Bunge na bila kuidhinishwa na CAG, this time limechota zaidi ya bilioni 900. Tungekuwa na serious media, zamani wangeshutumia IJ kujua hizi fedha za vote 20 ambazo hazikuidhinishwa na Bunge, zinafanyia nini?.

Kabla Lissu hajadhambuliwa , kuna mtu alisema kuhusu tunadukua simu mtu fulani, intelligence agencies zote duniani zinadukua sio simu tuu, hata tailing, emails hadi private lives, lakini haya mambo huwa hayasemwi.

Akakamilisha kwa kumuita mdukuliwa ni msaliti na kusema msaliti hawezi kuachwa hivi hivi akasurvive na kutolea mfano usaliti vitani huwa wanafanywa nini.

Baada ya muda mfupi Lissu kashambuliwa. Tungekuwa na serious media, aliyemtaka maneno hayo angeulizwa alimaanisha nini


Ninachosema hapa kama hizi serious media zipo, zifanye tuone.
Kwa vile hatuna then inawezekana kabisa sisi tuko huru kuliko UK na US ila hatuna competent person who can do some serious stuff.
P
 
Kipindi cha JK Kubenea alipata wapi taarifa za Ikulu?mbona alitetewa kuwa ni uhuru wa habari?kwanini huyu jamaa akamatwe na watu waliomtetea Kubenea?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Achana naye huyo, analeta ukada. Yaani upuuzi wa Makonda wa kuutetea kweli?
Wema ni akiba.
 
wa hivi karibuni sijawahi kusikia Mwandishi wa habari wa Tanzania kukamatwa na kushitakiwa kwa alichoandika
Pascal, wote sasa hivi si wanaandika kwa kumsifia Magufuli, watashitakiwa kwa lipi? Waandishi nyinyi mnaongoza kwa uoga baada ya Azory kupotea.

Wewe ulijaribu kuwa huru, kilikupata nini? huko Bunge ukapelekwa na Tangu muda huo ukaamua kujikalia kimywa au kuunga mkono juhudi kiujanja ujanja!... ukiwa na nai ya kukosoa lkn ka woga kanakufanya usite kuandika ubaya, maoni huru uliyonayo
 
Kipindi cha JK Kubenea alipata wapi taarifa za Ikulu?mbona alitetewa kuwa ni uhuru wa habari?kwanini huyu jamaa akamatwe na watu waliomtetea Kubenea?

Sent using Jamii Forums mobile app
Uchungizi haukuonyesha km kubenea alihack information inawezekana kuna mtu alivujisha taarifa zikamfikia kubenea. Sidhani km hilo ni kosa la mwandishi, hilo ni tatizo la maafisa wa usalama kuwa taarifa hazitoki nje. Lkn Julian anakiuka sheria za kimtandao ambazo mataifa yote wanaheshimu. Majasusi huwa wana hack baadhi ya information kwa matumizi yao ya kiusalama, huwa hawapublish. Hata zile email za Hilary, sio km alikua anaziaccess peke yake, mashirika mengi ya kijasusi huwa yanazipata ila hawawezi kuanika kwa raia wa kawaida.
 
Sidhani Pascal ila mazingira ya kuandika habari za kiuchunguzi yamebinywa. Kumbuka wakati Ndugu Ulimwengu alipoanza kuandika makala zake za uchunguzi, akifuatiwa na Mwana halisi, na wengine nini kiliwakuta??. Pia kumbuka kukua kwa aina fulani ya uandishi ni mazingira na kama mazingira hayaruhusu huwezi ona kukua kwa aina hiyo ya uandishi.

Na mara nyingi waandishi wa Tanzania wanaandika kufutana na nani yuko madarakani na anataka nini, hata uandishi wako wewe mwenyewe umebalika sana sio wa Pascal yuleee na wote waliosoma maandishi yako ya kabla wanajua ni influensi ya mazingira. Hivyo kiufupi demokrasia ya kuandika inaendani na demokrasia ya uhuru wa kujieleza na uhuru wa watu kutafuta platform nyingi wawezavyo ilikuandika na kutoa mawazo yao kwa mujibu wa sheria zinazo waongoza.
Sijui kama tanzania tunasheria inayoruhusu na kulinda investigative journalism?
 
Kigogo India Asange wetu, kama anatafutwa akamatwe, na tusubiri kwanza akamatwe, maana sikuwahi kusikia kama wale wasiojulikana kumshambulia Tundu Lissu wakitafutwa hivi, ila akipatikana, tusubirie nini kitamkuta
P.
 
Wanabodi,
Leo ni siku ya kimataifa ya uhuru wa habari, kila mwaka sisi waandishi huwa tunakutana mahali kwa siku 2 na kujadili mambo mbalimbali kuhusu uhuru wa habari, na katika mkusanyiko huo, serikali, vyama vya habari na Taasisi za habari hutoa matamko kede kede kuhusu uhuru wa habari, lakini kwa mwaka huu, kufuatia janga la Corona, hakuna maadhimisho yoyote rasmi ya kukutana, ila nilitegemea wizara ya habari, vyama vya habari na mashirika na Taasisi za habari zitoe matamko mbalimbali.

Bado sijabahatika kuona tamko lolote!, ila usikute zile speech huwa zinaandaliwa kwa ajili ya presentations kwenye kongamano hotelini, safari na per diem!, leo hakuna safari, no trip, no per diem, no hotel gathering, hivyo this time hata speech tuu hakuna?!.

Nawatakia waandishi wenzangu, maadhimisho haya ya kimya kimya, nawashauri wale wafadhili mbalimbali wa tukio hili, kwa vile hatukusafiri, wala kula na kulala hotelini, then naomba hao wafadhili watutumie tuu hizo per diem, tutahama majumbani mwetu na kuhamia hotelini 3 days kisha tutatoa matamko.

Paskali
 
 
Mkuu snow snow , karibu na mitaa hii .
P
 

Yaani Watanzania siku hizi ni siasa za mashindano tu kila tatizo letu tukiwa nalo badala ya kulitatua ni kujaribu kushindanisha. Tukishidwa hoja siku hizi msemo ni tuachie nchi yetu😂 na ndiyo maana mijadala ya hivi yote inaishia tuachie nchi yetu! Kaeni na mabeberu wenu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…