Je, tamko la Rais ni sheria? Kama halijatekelezwa hatua gani huchukuliwa?

pathfind

New Member
Oct 17, 2023
4
2
Je, tamko la Rais ni sheria? Kama ni sheria au lazima litekelezwe? Ikitokea halijatekelezwa au kufanyika kama alivoagiza inakuwaje?

Mimi ni mmoja kati ya wahanga waliokutana na tamko hilo halafu halikutekelezwa.

Binafsi ilikuwa hivi; mimi nilikuwa mshiriki wa baadhi ujenzi miradi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nikiwa kama kama fundi umeme (nikiwa askari wa JKT operation Magufuli).

Nimeshiriki ujenzi wa maghala ya kuhifadhia silaha mapya JKT, ujenzi wa Ikulu, ujenzi wa nyumba 41 ulinzi kikosi cha Rais na ujenzi wa nyumba za jeshi la magereza Ukonga. With evidence Rais alitutamkia mbele ya umma kuwa kuanzia siku hiyo ya makabidhiano sote ni waajiriwa.

Ila ndugu Watanzania wale vijana tulioshiriki idara hizo nyeti tupo mtaani na tulipigwa na butwaa ndio maana leo nimeamua kuuliza swali hili hapa huenda ufahamu wangu mdogo.👋👋
 
Nijuavyo mimi rais ni Amiri Jeshi Mkuu na anapotoa tamko mbele ya umma tena mbele ya wakuu wa majeshi, agizo hilo linapaswa kutekelezwa mara moja.

Fanyeni kila muwezalo suala hilo lifike kwa wakubwa ikibidi kwa Amiri Jeshi Mkuu wa sasa. Kusema kweli agizo hilo lilipaswa kutekelezwa.

Poleni!
 
Hapo mpk rais akumbuke na kwa bahat mby secretary nae kagoma kumkumbusha,hakuna namna zaid ya kukumbushwa na kama alikuwa magufuli sizan kama ulikuwa hamjui kwa sifa yule ndugu.
 
ndungu watanzania hakika inauma sana nilishindwa ta kujua hata wapi niende maana hata wenzangu waliojalibu kwenda sehemu mbali mbali ilishindikana pia.binafsi kwangu nidonda ambalo lanitesa maisha yangu yote,inauma tena sana
 
Nijuavyo mimi rais ni Amiri Jeshi Mkuu na anapotoa tamko mbele ya umma tena mbele ya wakuu wa majeshi, agizo hilo linapaswa kutekelezwa mara moja.

Fanyeni kila muwezalo suala hilo lifike kwa wakubwa ikibidi kwa Amiri Jeshi Mkuu wa sasa. Kusema kweli agizo hilo lilipaswa kutekelezwa.

Poleni!
dah! asante
 
Ni hatari mtu aliyeshiriki kujenga IKULU akawa mtaani jobless,

Mamlaka zibueni masikio tafadhali🙏
 
Back
Top Bottom