Je, shilingi milioni 2 Itatosha kwa biashara ya vifaa vya ujenzi na umeme?

Majigo

JF-Expert Member
Feb 23, 2012
5,519
1,825
Wakuu!

Nipo DAR Kuna kamkopo Natarajia Kupewa Mwez Wa Pili Mwakani.

Wazoefu naomba mnishauri Kama pesa hizo zitatosha
na vp upatikanaji wa bidhaa hizo kwa bei ya jumla na mapendekezo yenu ikibidi!

Ahsanteni wakuu!
 
Duh!
Basi itabidi nijipange kivingne...Ahsante Sana Kiongozi!

mkuu, usikate tamaa !! kama fremu ya biashara unayo tayari katika location nzuri i mean kodi haimo kwenye 2M, basi unaweza kuanza kwa kuweka vitu ambavyo ni fast moving na visivyohitaji mtaji mkubwa, uneweza anza na misumari, binding wire, square box, conduit pipes, hata switches na sockets ukanunua nusu dozen, baada ya kuwa na duka then kuna suppliers wenye maduka makubwa ya wholesale watakupa mzigo kwa mali kauli

mtaji wa cement ni mkubwa faida ndogo sana

all the best
 
bluetooth,

Mkuu umenena kitu cha maana sana
pango linajitegemea

Ila hapo kwenye blue inakuwaje hyo biashara vilevile ni maduka na mtaa gani kwa hapa kariakoo kuna maduka ya jumla yenye bidhaa za bei nafuu?
Ahsante sana Mkuu!
 
Kwani ungesema 21M haitoshi si angekuelewa tu? Mpaka umkatishe tamaa kwa kumvunja moyo eti afungue genge? Binadamu bwana!!!

mim pia nimeshangaa,2million kuna watu wanaona nyingi wengine wanaona kidogo,hivo ni kutoa ushauri bila kuingiza mazarau kwa mtu,unaweza kuta mtu anatoa zarau wakat yeye hio 2 million ajawai kushika,tutumia lugha nzuri ambazo hazina zarau
 
Nalo hilo, limfikie huyo jamaa!
Hakuna anayeanzia juu labda kama Ukute vya urithi Na kuviendeleza Au Zali Likuangukie
Ila Utasahau kuwa Cha Chini Ndicho Kinachokupandisha Juu!
 
Nalo hilo, limfikie huyo jamaa!
Hakuna anayeanzia juu labda kama Ukute vya urithi Na kuviendeleza Au Zali Likuangukie
Ila Utasahau kuwa Cha Chini Ndicho Kinachokupandisha Juu!

kweli mkuu,wafanyabiashara wote uanzia chini mimi pia nilianza chini,unajua unapoanza biashara usianze kuwekeza pesa nyingi ata ama unazo lazima uanze kidogo,usikilizie kwamba watu watarespond vipi,hivyo ndio watu uanza biashara si utoe million 30 yote ubak hauna kitu,watu wajifunze apa
 
Nakutunuku Viroba Vya Manyota Kiongozi Wangu Money Stunna
Ili Kujenga Uzoefu Ulio Imara, Lazima Kufanya Hayo Uliyoandika Tena Hata Kama Una Mtaji Mkubwa!
Et "Hata Genge Ni Lile La Chini Sana"
He! Sijui Hilo Genge litakalokidhi Pesa Anazoziwazia Yeye, Nikafungulie Ktk Ikulu Ya Madiba?

Kanichosha Sana Huyu Jamaa!
 
niliwahi kuwa na wazo kama lako na nilikuwa na kama 5mil but watu niliowaconsult waliniambia hicho ni kiasi kidogo at least ningekuwa na 10mil ningeanza na kitu fulani ambacho kwasababu faida yake sitakuwa naitegemea kwa matumizi yangu binafsi basi litajikuza lenyewe na hatimaye litakuwa kubwa tu. hiyo 2 mil unaweza ukafungua kiubishi kama alivyokuchambulia mdau hapo juu but itachukua muda MREFU SANA kuja kuona faida au duka kuwa kubwa so ni bora ujipange na angalau uwe na hiyo kuanzia 10. huyo jamaa anayesema hata mil 21 haitoshi nadhani anahisi unataka ukifungua leo basi wiki ijayo ushindane na wale wenye maduka kariakoo tangu mwaka 92,na sidhani kama pia meza ya CHINI KABISA ya matunda ni mil 2 labda kama embe moja ni 10,000. usikate tamaa lakini pia usianzie chini sana u will waste time bure.
wish u the best
 
telecom,

Basi itabidi niangalie namna nyingine ya kuwekeza hizo mil 2 ili ziweze kukamilisha lengo langu
Nimeona bora niuze vinywaji baridi hapa mjini!
Au mnaonaje wadau?
Ahsante pia!
 
mim pia nimeshangaa,2million kuna watu wanaona nyingi wengine wanaona kidogo,hivo ni kutoa ushauri bila kuingiza mazarau kwa mtu,unaweza kuta mtu anatoa zarau wakat yeye hio 2 million ajawai kushika,tutumia lugha nzuri ambazo hazina zarau

Uko sahihi kaka, nadhani Mkuu Bluetooth keshamaliza fitina hapo juu, inategemea na yuko eneo gani, tayari ana kitu gani sasa hivi, na vitu gani aanze navyo kutokana na soko la hilo eneo.

Mali kauli itakuja baadae baada ya kupata uzoefu na kuaminiana na wauzaji wa jumla kulingana na mwenendo wa biashara yako ya sasa hivi. Usikate tamaa mkuu.
 
Umeandika pointi za Ukweli mtupu, niko Dar kigambon Itabidi Nisome Mazingira!
Shukrani sana kwa kunipa moyo mkuu
 
2 MILION HIYO NI KUBWA SANA

- Tatizo letu sisi watanzania tunataka kuanzia juu, tunataka kuanzisha duka na kujaza vitu bila kujalisha vinanunuliwa au la, tunataka kupendezesha maduka, tunapenda kusifiwa kwamba duka la fulani limesheheni sana vitu,

Mkuu 2 milioni inatosha kabisa ni wewe kujipanga tu na kuja na strategies za kureduce cost na katika kupunguza kost hapo utafanikiwa, kuna watu walianza na mchicha fungu mbili lakini leo hii wako mbali sana, Yule Marehemu MUGUKU wa kule Kenya alianza na kuku wasio pungua kumi ila mwisho wa siku akaja kuingia kwenye Orodha ya matajiri watano wakubwa kabisa nchini Kenya, kinacho takiwa ni determination na si vinginevyo,

Unaweza kuwa na milioni 200 na bado ukashindwa kufanya hiyo biashara, tatizo tuna tageti utajiri wa haraka haraka na kutaka kusifiwa,

Ukiondoa mawazo ya kutaka utajirike fasta, kutaka uonekane, kutaka usifiwe utaweza songa mbele na hiyo milioni 2,

Na katika biashara kuna kitu kinaitwa kujiposition, na si lazima wewe uuze kila kitu, si lazima upambe duka kwa vitu visivyo nunuliwa mkuu,

NA MWISHO KABISA, TATIZO LILIPO HUKU JF NA MTAANI ni kwamba Unapo taka ushauri wa biashara ni bora kabisa ukawatageti wahusika means wafanya biashara wengine, HUMU JF UTAKUTANA NA WAHANGA WA MISHAHARA NA WATAKUKATISHA TAMAA BALAA, Mtu alisha zoea mwsiho wa mwezi na yeye kwake Biashara ni kama gereza so ni lazima ukatishwe tamaa, usitarajie hata siku moja kwenda kuomba ushauri kw amtu ambaye ni mwajiriwa utarajie Postive ushauri, atajitahidi sana kukuvunja moyo na kukuogopesha ili wote muwe kundi moja la Mwisho wa Mwezi
 
Back
Top Bottom