Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,484
- 30,162
Rais Samia ametoa kauli yenye utata mkubwa, wakati wa ziara yake huko Usa River, Arusha, hapo majuzi.
Wakati akitoka kwenye semina elekezi ya viongozi waandamizi huko Arusha, alitoa kauli hii wakati anazungumzia ujio wa Godbless Lema, hapa nchini, kuwa "Mwanaume ni yule anayejiamini" na akaendelea keleza kuwa mwanasiasa huyo wa Chama Cha upinzani Cha Chadema, alimwomba kurudi nchini, lakini akaeleza wasiwasi wake kuwa anaogopa kurudi nchini, kutokana na kuhofia usalama wake, pia aliomba afutiwe kesi nyingi alizo ambazo amebambikiwa na Jeshi la Polisi nchini.
Ndipo Rais Samia, alimuhakikishia mwanasiasa huyo wa upinzani, kuwa aondoe wasiwasi na akamuhakikishia usalama wake na kumweleza kuwa anaweza kurudi nchini na kesi zote zilizoko mahalamani atazifuta.
Akeleza zaidi kuwa baada ya kurudi Mwanasiasa huyo wa upinzani, hakuna baya lolote lililomkuta.
Ndipo akatumbukiza kibwagizo hicho Cha "Mwanaume ni yule anayejiamini"
Ndipo hapo ninapojiuliza, je hiyo kauli ni kijembe kwa Mwendazake?
Kwa kuwa ni katika utawala wake, Hayati Magufuli, ndipo wanasiasa wengi wa vyama vya upinzani, waliomba ukimbizi, nje ya nchi hii, wakiwemo, nikiwataja wachache, Tundu Lissu na Ezekia Wenje.
Kwa kuwa huyo mwanasiasa Lema, aliikimbia nchini mwaka 2020, wakati wa utawala wa Rais wa awamu ya 5, Hayati John Pombe Magufuli, ambaye aliiendesha nchi kibabe Sana, bila kufuata Katiba ya nchi na ndiye aliyepiga marufuku mikutano yote ya vyama vya kisiasa ya vyama vya upinzani nchini.,na alikwenda mbele zaidi, Kwa kuliagiza Jeshi la Polisi, liwabambikie kesi viongozi hao wa upinzani, pale alipojisikia!
Ndipo hapo nimewaza Sana kuhusu kauli hiyo ya "Mwanaume ni yule anayejiamini"
Je alimlenga nani, kama siyo, Hayati Magufuli?
Kwa kuwa ndiye aliyekuwa akiyafanya hayo maovu yote, Kwa kutojiamini kwenye siasa.