econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 15,804
- 21,776
Wakati akiwa kwenye mkutano wa JWTZ, Rais Samia alijulishwa na Mkuu wa majeshi Jenerali Jacob Mkunda kuwa Kuna wakimbizi wameteuliwa kwenye vyombo vya maamuzi.
Ili kukwepa hiyo kauli ya CDF, Rais Samia alipopewa nafasi ya kuongea kwenye mkutano huo, akaleta mada nyingine kwamba mwaka 2025 ni mwaka wa uchaguzi hivyo vyama vipo vingi na vingine havina Nia njema, hivyo jeshi liwe tayari kwa lolote.
Kauli ya Rais ilikuwa ya kinafiki na kujaribu kujenga taswira ya kwamba vyama vya Upinzani vinalenga kuleta fujo au kauli ya Rais ililenga kuwaingiza wanajeshi kwenye siasa za kuilinda CCM .
Namuomba Rais asitumie vyama vya Upinzani Kama Chaka la kujifichia, kwani tumefanya chaguzi nyingi na JWTZ haijawahi kuhusishwa. Yeye ajikite kushughulikia kauli ya CDF kuhusu wakimbizi kuteuliwa kwenye nafasi za kisiasa. Aache longolongo.