Inside10
JF-Expert Member
- May 20, 2011
- 33,614
- 40,160
Anaandika Aloyse Nyanda Mtozi kupitia ukurasa wake wa Instagram:
Je Fr Kitima anachuki na serikali au ana chuki na Rais Samia au anachuki na Uislamu?
Jibu ni HAPANA ila ukweli ni kwamba Kitima mbali na kuwa ni mlezi wa wengi pia ni Mwalimu wa Human rights alifundisha vijana chuo Kikuu na linapokuja swala la Haki na Usawa hatazami Mtu.
Alikuwa VC wa SAUT na mwaka 2003 wakati huo Rais wa Nchi akiwa Mkapa.
Wakati huo Fr alikuwa anapiga kelele sana kuhusu uwekezaji kwenye sekta ya Madini,alitaka kuona Watanzania wananufaika na uwekezaji kwenye sekta ya Madini. Alimshambulia Mkapa Mkatoliki
Fr Kitima 2005 alianzisha kituo cha haki za binadamu cha SAUT ambapo alikuwa anapambana na mauaji ya watu wenye ulemavu pamoja na Vikongwe.
Fr Kitima yeye mwenyewe alikwenda field kuzungumza na wananchi na kutoa elimu kwa wakazi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Sauti ya Fr ilisikika kanda yote ya ziwa,alitumia njia nyingi kuhakikisha watu wenye ulemavu pamoja na vikongwe wanabaki salama.
2.Wakati wa Kikwete Fr kitima alipiga kelele kuhusu masuala ya haki za binadamu alimshambulia kikwete wala sio Uislamu wake
Mwaka 2009 ,Fr alipiga kelele kuitaka serikali iwasomeshe wanafunzi wote wa vyuo vikuu,na hili alilifanikisha.
3 .Wakati wa JPM Fr Kitima alimkosoa vikali JPM pale alipoanza kuwakandamiza wapinzani wake,kufungia media na NGOs kuzuia uhuru na JPM ni mkatoliki
Aliukosoa waziwazi uchaguzi wa 2020 na kusema hakukuwa na uchaguzi na kumeliacha taifa kwenye majonzi
Wakati wa sakata la Covid,Fr hakukubaliana na serikali,aliitaka serikali ya JPM kuweka wazi idadi ya wagonjwa na waliofariki kwa covid.
Fr alifanya mkutano na waandishi na kutamka idadi ya mapadri waliopoteza maisha kwa covid hali ambayo ilizua sintofahamu kuhusu msimamo wake.
Hivyo Fr kuikosoa serikali hii,si chuki kwa Rais wa sasa wala kusema anamchukia Rais Samia.
Nadhani wale vijana wahuni wameshindwa kutafsiri akili kubwa ya Fr Kitima.
Fr kwa sisi tunaomjua na tuliemuona Pale Saut,tulimsikiliza na tuliomfuatilia ,ni muumini mzuri sana wa Ujamaa wa Mwalimu Nyerere.
Ukosoaji wake huwa hautazami anayemkosoa dini gani,chama gani,jinsia gani.
Yeye ana mambo mawili anayasimamia.
1.HAKI
2.Umasikini(Huwa anaumia sana kuona watu ni masikini katikati ya utajiri)
Mtozi