Je, ile momentum iliyokuwepo itaturusha nje ya dunia kama mtu anavyorushwa kwenye kioo cha mbele cha gari?
Nakubaliana na maoni ya
simplemind lakini ngoja nifafanue kidogo. Samahani kwa urefu wa hili jibu.
Kuna mizunguuko mitatu ya dunia yetu:
- Mzunguuko unaotupa usiku na mchana (mara moja kila masaa 24 about the north-south axis).
- Mzunguuko unaotupa majira ya mwaka (kulizunguuka jua, mara moja kila siku 365.25).
- Mzunguuko au m-yumbo wa hii North-South Axis (precessional rotation au the wobbling of the north-south axis) na huchukua miaka 26,000 kwa kila mzunguuko mmoja.
Sasa tuone kitatokea nini kama moja ya mizunguuko hii mitatu itasimama.
Kabla sijaendelea, ni lazima ujue kuwa kuna kanuni za fizikia kuhusu mizunguuko. Kanuni muhimu ni kuwa kitu kinachotembea kitaendelea kutembea mpaka kikutane na nguvu itakayokisimamisha au kubadili muelekeo wake. Swali lako linakosa mashiko kwa sababu hicho kitu (au dhoruba) kitakachotusimamisha ghafla kitamaliza uhai wote hapa duniani kwa hiyo haileti maana kuulizia kuwa sisi tutaathirika vipi. Ni sawa na kuuliza kitatokea nini kama unasafiri kwenye gari (la wazi au lililofunikwa) kwa kasi ya 200 km/saa na ukagonga ukuta au mwamba. Lakini, just as a non-serious academic exercise, ngoja nijibu.
1. Kusimama kwa mzunguuko wa kwanza:
Kwanza mabadiliko ya uhakika ya usiku na mchana yatakoma. Pili, tutayumba kwa sababu ile stability inayoletwa na huu mzunguuko (gyroscopic stability haitakuwepo tena). Kwa hiyo ingawaje hatutakuwa na mabadiliko ya uhakika ya mchana na usiku lakini majira yetu (kiangazi, vuli/masika) havitakuwepo. Jet stream itasimama na kuharibu kabisa hali ya hewa.
2. Kusimama kutolizunguuka jua.
Kama mkuu
simplemind alivyosema tutadondoka kama embe kuelekea kwenye jua. Dunia yetu ni kama satelite ya jua. Tunabakia kwenye orbit yetu kwa ajili ya huu mzunguuko. Kama ilivyo tunapotaka kudondosha satelite zetu tunapunguza kasi yake basi itakuwa hivyo hivyo kwa dunia. Tutaangukia kwenye jua na hapo mchezo ndio utakuwa umekwisha.
3. Kusimama kwa precessional rotation (au Gyroscopic Precession).
Kwa wale wanaofuatilia maswala ya unajimu (Astrology) watajua kuwa
Spring au Vernal Equinox (siku ambayo urefu wa usiku na mchana ni sawa) hutokea
March 20 na wakati huo jua linakuwa kwenye mkusanyiko wa nyota (constellation) wa
Pisces (au Samaki). Lakini kwa ajili ya hii Gyroscopic Precession, kila baada ya miaka 2,150 jua linahamia constellation nyingine (kutoka Pisces, to Aquarius, to Capricorn, to Sagittarius, to ...). Sasa hivi jua linapaswa kuwa limehamia kwenye constellation ya
Aquarius (Maji). Huu mzunguuko utaendelea kubadili jua litakapokuwepo (constellation) na utaendelea kwa miaka 26,000 ili kurudi ulipoanzia. Soma zaidi kuhusu
AGE OF AQUARIUS hapa -
Age of Aquarius - Wikipedia, the free encyclopedia.
Sasa kama huu mzunguuko (gyroscopic precession) ukisimama basi siku zote
Spring Equinox ikitokea jua litakuwa kwenye constellation moja tu na haitabadilika kamwe. Hii ina
serious astrological implications ambazo sitazielezea zaidi. Pengine nimekwisha wapoteza wengi na hiyo sio dhamira yangu.
Mkuu
neo1 upo lakini? Usiniulize swali la kinajimu tu.