OMKEIT 93
JF-Expert Member
- May 12, 2026
- 226
- 323
Kumekuwa na ongezeko la watu wanaodai kuwa Dunia si duara bali ni bapa (flat). Ningependa kusikia kutoka kwa wanaoamini nadharia hiyo.
Maswali yangu ni haya:
Mnasemaje kuhusu mchana na usiku? Vinatokeaje ikiwa Dunia ni bapa?
Jua na Mwezi vinazungukaje juu ya Dunia bapa?
Kwa nini meli zinapoenda mbali baharini huanza kutoweka kuanzia chini kwenda juu?
Kwa nini watu waliopo upande tofauti wa Dunia wana nyakati tofauti?
Ikiwa Dunia ni bapa, mpaka wake uko wapi? Je, kuna mtu amewahi kuufikia na kuonyesha ushahidi?
Je, ni ushahidi gani wa kisayansi unaowafanya muamini kwamba Dunia ni bapa?
Lengo la mada hii si kubeza mtu yeyote, bali kusikia hoja na ushahidi. Kama unaamini Dunia ni bapa, karibu utoe maelezo yako. Kama unaamini ni duara, pia unaweza kujibu kwa ushahidi na heshima.
Karibuni kwa mjadala wa hoja, si matusi.