Je ni kweli wazazi huwa wanaona mbali linapofika kuoa au kuolewa

Mboka man

JF-Expert Member
Aug 22, 2020
478
1,638
Japo sio wote ila kuna aina flani ya wazazi ambao linapofika swala la kuoa au kuolewa wana tabia ya kuwapinga watoto wasioe au kuolewa kutokana sababu wanazozijua wenyewe kama vile kabila , Dini, familia n. K kwa hofu watoto watakuja kuteseka

Je katika hili kuna ukweli wowote ule
 
Wengine ni hofu zao. Na hii inasababisha baadhi ya vijana kushindwa kujitegemea kifikra. Matokeo yake wanawategemea zaidi wazazi wao. Wazazi wanachotakiwa kufanya ni kuwaombea baraka watoto wao na si kuwawekea vikwazo

Halafu mara nyingi inajitokeza kwa mtoto wa kwanza au mtoto pekee au anayependwa ama kutegemewa na wazazi. Wanakuwa na hofu nyingi ya kupoteza ukaribu, heshima au upendo kutoka kwa huyo kijana au binti yao.
 
Wengine ni hofu zao.
Na hii inasababisha baadhi ya vijana kushindwa kujitegemea kifikra. Matokeo yake wanawategemea zaidi wazazi wao.
Wazazi wanachotakiwa kufanya ni kuwaombea baraka watoto wao na si kuwawekea vikwazo

Halafu mara nyingi inajitokeza kwa mtoto wa kwanza au mtoto pekee au anayependwa ama kutegemewa na wazazi. Wanakuwa na hofu nyingi ya kupoteza ukaribu, heshima au upendo kutoka kwa huyo kijana au binti yao.
Sawa kabisaa
 
Wazazi hujua vitu vya kuangalia unapo taka kuoa au kuolewa,wewe unaweza kutaka kuoa kwa tamaa ya kalio kubwa tu!

Historia ya sehemu/familia unayo kwenda kuoa au kuolewa ni muhimu sana,
wanasema mwenye mapenzi haoni ingawa macho anayo,na hapo ndipo macho ya wazazi hutumika ili kukuongoza.
 
Wazazi huwa wanaona mbali pia kunawengine wanahila tu hawanasabbu za msingi na wazazi wengi sikuhiz wengi wanapenda watoto wao waolew na waoe kwenye familia zinazojiweza maisha yanaenda Kasi sana
 
Wengine ni hofu zao. Na hii inasababisha baadhi ya vijana kushindwa kujitegemea kifikra. Matokeo yake wanawategemea zaidi wazazi wao. Wazazi wanachotakiwa kufanya ni kuwaombea baraka watoto wao na si kuwawekea vikwazo

Halafu mara nyingi inajitokeza kwa mtoto wa kwanza au mtoto pekee au anayependwa ama kutegemewa na wazazi. Wanakuwa na hofu nyingi ya kupoteza ukaribu, heshima au upendo kutoka kwa huyo kijana au binti yao.
Duu kweli mkuu hii imenikuta so nimekuelewa sana!
 
Back
Top Bottom