Babu Anganga
Senior Member
- Jun 13, 2009
- 169
- 110
Elimu nzuri. Asante Mshana Jr
Hahahaaa mkuu usikute ata humu watoa uzi na wachangiaji baadhi ni ivyo viumbe
Nimechoka kusikia, kusimuliwa kwamba kuna viumbe wanaonekana kwa jicho la tatu.
Mwenye dawa ya kutumia ili kuwaona hao viumbe ani PM nimeshakua mtu mzima nataka nione mwenyewe.
Naomba sasa mimi ndio nikupe darasa
Mizimu inatokana na roho za wanadamu waliokufa, kuna matabaka matatu ya roho hizi
1.roho ambazo zipo makaburini zikisubiri kiama, hizi ni roho ambazo katika maisha yao wamiliki wake walitenda mema sana kwahiyo hazihangaiki
2.roho zinazotangatanga wondering souls hizi ni roho za kishetani zinazosumbua mno ulimwengu hasa kwenye mabalaa Kama vita magonjwa na mifarakano, ndani ya hizi kuna hungry ghosts, wamiliki wa roho hizi wengi ni wale ambao waliishi maisha yasiyompendeza Mungu na kufanya mambo mabaya sana
3.roho za mizimu hizi ni roho za watu wazima sana walioishi maisha mengi na kufanya maagano mengi kwenye ukoo kabila hata familia na kuweka wazi kuwa baada ya yeye kufa lazima kifanyike hiki au kile au fulani akizaa mtoto ampe jina fulani nk nk ...!!!msipotekeleza hayo ule mzimu wake(roho) hukuandameni kwa mabaya. Na ndio maana huwa tunasema mzimu wa mtu fulani
Tukija kwenye majini ni kwamba hawa ni viumbe walikuwepo tangu uumbaji majini si watu hawajawahi kuwa watu bali wanachoweza kufanya huweza kumuingia mtu na kuzaa naye...! Au huweza kujigeuza na kuwa kama binadamu na kuishi maisha ya kawaida japo hayadumu, ndani ya hayo majini ndio utapata variety yake kama jini subiani, mataka nk
Wote mpo sahihi mlicho tofautiana ni mipaka katika ufahamu juu ya hili
Kuna majini yaliyo kwenye koo na roho za wafu zote kwa pamoja ni (mizimu) hutenda kazi kwa sawa, shetani kawagawa ili kuwatawala wanadamu
Maana ata bibilia inasema katika ufunuo nyakati za mwisho na kuzimu itatoa wafu wao
Hapo utagundua dhairi kwamba kuna roho za wafu ambazo zipo kuzimu na wakati huohuo tunajua wazi kuzimu ni makazi ya majini, mizimu n.k (roho chafu au mashetani)
Kuna makabila wanasemaga wao mzimu wao ni nyoka au chui au njiwa.na hao inakuajekuaje??
That's critical thinking. ...big up
Kuna makabila wanasemaga wao mzimu wao ni nyoka au chui au njiwa.na hao inakuajekuaje??
Wamerithishwa hivyo ilikuwa ni utamaduni wa watu wa zamani kujitambulisha kwa uhalisia wa wanyama kwamba yeye ni simba chui nyati nk kwahiyo hata baada ya kufa waliobaki humtambulisha mnyama husika kama mzimu wao wakimuenzi marehemu
Mshana wale uliowaahidi kuwafundisha kuona ya ulimwengu usoonekana kwa macho haya,je darasa leo linaendelea private!??%
Nahisi labda na wengine tungependa kujua hivyo mwaga utaalam hadharani.
Kuna safari ya msata mpaka wami kesho sijapata hata mmoja mpaka sasa wakwenda, yale hayaandikwi hapa bali kila mmoja anabeba zana zake tunaenda field
Tutaanzia makaburi ya msata na kumalizia mtoni wami usiku mwingi
Nnaona yamekuingia ukashindwa la ku comment.
Hata Yesu alikumbwa na majinni, kasome biblia.