Je, ni kweli kuwa vichaa wana jicho la tatu?

Je, ni kweli kuwa vichaa wana jicho la tatu?

20150304_170202.jpg
aibu3.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahhahahaaaa kama ungelijua hilo si ungeleta post tangu mwanzo, replies za namna hii kwangu ni burudani mwanzo mwisho na sibabaiki nazo
Kwa ufupi wewe ni BONGE LA MPUUZI na utakuwa hivyo mpaka mwisho wa uhai wako! Kumbuka hili neno kuwa wewe ni BONGE LA MPUUZI kila siku ukipiga mswaki asubuhi kuanzia leo mpaka siku unakufa, usisahau hili kuwa mshana jr kakuita BONGE LA MPUUZI kila uamkapo na upigapo mswaki
Imeandikwa usilaani,ila kikweli faizafoxy huwa anapoint Fulani lakini kutokana na kugoma kutibu tabia yake gonjwa nami nadhani ni vema tumuombee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naamini wote tuna ufahamu wa kutosha kuhusu jicho la tatu, kuona yasiyoonekana katika macho ya kawaida na kusikia pia ikiwemo na ufahamu wa yajayo.

Vichaa ni watu waliodharaulika katika jamii wana majina yote mabaya hawaogi ni wachafu wananuka hawana faida yoyote kuwa na ndugu kichaa ni msiba .

Ukichaa ni familia moja kubwa sana humo wapo machizi, wendawazimu, punguani wote hawa wanaingia kwenye kundi moja kubwa la vichaa.

Kwa tafsiri ya kawaida Ukichaa nk ni kutenda kinyume na kawaida kufanya mambo yasiyoeleweka na kutojitambua kuwa wewe ni nani uko wapi na unafanya nini. Zipo hospital maalum zinatoa tiba lakini kwa kiasi kikubwa mafanikio ni hafifu.

Kwahiyo tuzungumzie Ukichaa katika ulimwengu wa roho na ni kipi ambacho hutokea hata mtu akafikia hatua ya kuwa mwendawazimu chizi au kichaa kabisa.

Lakini vile vile tujiulize ni kwanini vichaa wengi hutibiwa kwa waganga wa jadi hasa wanaitumia maruhani mizimu na majini ? Kisha wakapona kabisa? Hapa sizungumzii wale wanaowehuka baada ya kutumia vitu kama bhangi nk .

Ukichaa ni roho chafu za mapepo majini na maruhani za kutangatanga zinazomuingia mtu na kufanya kikao ndani ya mwili wake...lakini pia kuna ule Ukichaa wa kukiuka masharti fulani ya mizimu ya ukoo au kabila .

Kinachofanyika ni hiki, aidha kwa kutupiwa kukanyaga au kuingiwa na hizi roho , mtu huondoka kwenye kikomo chake cha kawaida cha binadamu cha kuona na kusikia na kufunguliwa ulimwengu mwingine wenye mambo ya kutisha kuwehuka huanzia hapa.

Mwenzenu anaona kabisa mliokaa nao sio watu anakimbia anawashangaa mkimkimbiza na kumfunga kamba kumbe kiuhalisia alichoona ndio hicho ila kwakuwa mmefungwa na kiwango cha kuona nyie mnaona mmekaa na watu.

Huwa tunawashangaa wakiongea pekeyao Kimsimgi hawaongei pekeyao kuna watu wapo karibu yao na wanaongea nao wanapanga nao na kujadiliana mengi tu.

Kwakuwa kilichowaingia ni roho wabaya wachafu wanaotangatanga ndio maana hata siku moja hutamkuta kichaa wa namna hii anaoga au anakaa na kutulia sehemu moja ukimkuta wa hivyo ujue ni wale waliovunja masharti ya kimila kiukoo kuhusiana na mizimu ya kwao.

Nimekuwa na rafiki zangu hapa jukwaani wenye hamu ya kutaka kuwaona wachawi nikaambia wakishakuwa na huo uwezo hawakuwa wao tena! Sababu ni hii!!! Utafika kariakoo na kuona fisi wengi sana utakimbia na kupiga kelele watu watakukamata wakufunge kamba wao wanaona umewehuka wewe unawashangaa.

Utafika kwako utakuta kuna watu wanawanga sebuleni kwako utaanza kupigana nao.. loh mkeo atajua huyu tayari mirembe inamhusu kumbe maskini haoni kile unachokiona wewe.

Mifano ni mingi ngoja nikomee hapa kwanza.

Ukichaa mwingine huanzia kwenye siasa na madaraka.
 
Kuna wanasayansi wamesema katika Tanzania kati ya watu 4 mmoja anaugonjwa wa akili... Maanake kichaa
 
Back
Top Bottom