BIG Banned
JF-Expert Member
- May 4, 2012
- 262
- 71
- Thread starter
- #101
Kama ni msomi uliyekubuhu na kufikia kiwango cha PhD ambacho si wengi walio-bahatika kufikia. Inabidi uwe na ufahamu wa kuwa, fedha na mali sio kila kitu.
Achievement bora zaidi ni kuwa na furaha ya moyoni kuridhika na ukifanyacho. Kama unaona huridhiki na kufundisha fanya utachoona kinakuridhisha satisfaction), lakini, usifikiri kuwa achievement ya usomi ni kipato, ungekuwa unataka kipato ungeachana na kusoma ukajiingiza kwenye biashara, unakumbuka kisa cha Bill Gates?
Fanya unachoona kitakupa wewe "tranquility" au inner self happiness.
Mkuu mi sijaongelea kuwa na mali kiasi hivyo we unasema. Lakini pia hakuna mtu yoyote ambaye anasoma tu ili kupata sifa kwamba yeye ni msomi, utakubaliana na mimi popote pale watu wanakimbilia kusoma ili kipato chake kiongozeke. Inakuwa ngumu sana au haiingii akilini wale ambao wamesoma na wanajitolea kusomesha na wengine lakini wenyewe binafsi hawana uwezo wa kupeleka watoto wako shule nzuri, hana nyumba ya kuishi (si serikali wala mwajiri wake anamjali kwenye hili), Unakaa mbali na eneo la kazi, usafiri huna. Isitoshe familia, ndugu wanakuangalia na kukusikiza wewe kwa vile umesoma lakini bado wanakushangaa huna hela. Kwahiyo katika haya yote ndio mana nikasema ni ngumu sana kuwafikia wale wenzangu ambao waliachana na mambo ya kusoma wakajiendeleza kifamilia kwanza. Kuwa muhadhiri bongo ni kupotezana muda tu.