Mashaurijr
JF-Expert Member
- Oct 8, 2016
- 646
- 1,026
Wakuu mimi ni kijana wa miaka 28 elimu ya form six chuo niliishia mwaka wa 2 kwa sababu ya kuugua baada ya hapo nikajikita zaidi kwenye biashara ambazo ndio zinaharibu akili yangu.
Tatizo kubwa linaletwa na upweke nilioishi utotoni. Niliishi na wazazi lakini mama alikuwa mtu wa kuugua na baba alikuwa akisafiri mara kwa mara hivyo tokea msingi nilikuwa karibu sana na mama nikimuuguza akiumwa na kukosa nafasi ya kujiunga na watoto wenzangu mara kwa mara kucheza.
Hata shuleni mpaka namaliza form 4 sikuwa mtu wa marafiki wengi au makundi. Hivyo matatizo yangu ni ngumu kumweleza mtu
Muda mwingi nabeba matatizo mwenyewe. Kiufupi sipo social sana japokuwa natamani na najitahidi ili kuondoa msongo wa mawazo.
Pia nimekuwa na malengo makubwa sana kwenye maisha ambayo nalazimisha sana kuyatimiza ila changamoto zinanifelisha. Akili yangu imeshindwa kukubaliana na ukweli kuwa inahitajika muda zaidi ili kufanikiwa.
Napata shida sana kwa sasa, napata maumivu makali ya kichwa navurugwa haswa baada ya kurudi tena nyuma kiuchumi natamani niachane na biashara niajiriwe lakini nani ataniajiri? Kichwa kinauma sana.
Kuna muda nafanya vitu ambavyo baadae nashindwa kuelewa nilifanya kwa akili yangu au ilikuwaje.
Nimekuwa mwoga sana wa kufanya maamuzi haswa ya biashara kitu kinachonimaliza kabisa.
Wakuu nifanyeje nijitoe kwenye kupania maisha kupitiliza na kuhofia nachelewa? Woga wa kufanya maamuzi? Nifanyeje nisije kuwa chizi najitahidi niwe social sana ila nafeli kutokana na maisha ya utotoni.