Je ni kweli GPA Kubwa iliniponza!! Nimechemsha au!!

Du! una PHD kweli wewe? mbona hoja yako kama hujasoma?

Hakuna utajiri hapa duniani kama elimu. uliowaacha na unaodhani wamefanikiwa wengi wao niwezi na mafisadi.
Lakini pia labda ungetuelewesha una define vipi maendeleo.
Baada ya hapo ndo tuendelee na mada. Lakini kama una maanisha nyumba na gari basi sina la kusema.
Ushauri wangu:
Tumia vizuri phd yako na kuorodhesha matatizo a yako halafu ya transform to OPPORTUNITIES! Fikiri kama mtu mwenye PHD! soma magazeti kuna requests kibao za ku express interests.
Tumia KALAMU na kichwa chako kutunisha mfuko wako wakati ukiendelea na kazi yako ya uhadhri lakini kwanza tuambie MAENDELEO NI NINI?

ALAMSIKI....PROFESA KILAZA

Akhsante!.
 
Pole sana mkuu aliyeseam ujanja kupata si kuwahi alikuwa na maana sana. Tanzania imekuwa corrupted na siasa. Miaka sisi tunasoma ilikuwa kubakizwa kuwa mwalimu wa University ni big deal na wengi walikuwa wanaishi maisha mazuri sana na yenye mafanikio. Kinachoua elimu Tanzania ni greed ya wanasiasa siku hizi utakuta mshahara wa mwanasia mwenye elimu ya darasa la saba aliyejipachika katika nafasi ya uongozi kwa uwezo wa kuchonga mdomo na kusifia waliopo juu yake anaishi maisha ya hali ya juu sana. Ndiyo maana ukiangalia watu wanakimbia chaki madarasani na kukimbia profession zao kuingia kwenye siasa na kugombea ubunge.

Wanasiasa wanajilimbikizia malipo ya kufuru huku watu waliotumia muda wao kusoma kwa ajili ya Taifa wakibakia kuwa ombaomba na watu wa kujipendekeza kwa wanasiasa wenye elimu duni dhidi yao. Nchi yetu imekuwa haiheshimu tena wataalam ndiyo maana wengi wa wataalam wame-compromise taaluma kwa kuwasikiliza wanasiasa wenye uelewa finyu na hata wakati mwingine kudiriki kuwafuata wanavyotaka mradi tu wasipoteze nafasi za kupata hata hicho kidogo.

Bado ninaamini kabisa kama tuna nia ya kuwa-retain watu kama wewe kwenye elimu ya juu tunatakiwa kuwaonesha kuwa education pays. Otherwise sooner or later utajikuta na wewe unapata mawazo ya kupanda jukwaani na kuizika taaluma yako, matokeo yake taifa linazidi kushuka chini. Tokea kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi kumekuwa na ongezeko kubwa sana la wanataaluma kuingia kwenye siasa maana ndipo kunalipa kwa sasa. Ukiangalia baadhi ya taaluma za wabunge waliopo bungeni leo utaona kuwa unaweza kutoa Univeristy moja yenye kukamilika kwenye kila nyanja kwa jinsi wanataaluma walivyojikita huko.

Lakini hata hivyo usikate tamaa, kama una PhD unaweza tafuta kazi nchi zinazothamini elimu kama Botswana na hata Rwanda na kujikuta miaka yako mitatu tu unakuwa sawa na wale uliomaliza nao undergrad. Wao wansisitiza uzalendo huku wakijilimbikizia, its time sasa na wewe kutafuta sehemu muafaka nchi ikitengemaa utarudi kuijenga.

Wanasiasa wanathamini wale watu wanaofanya na kudumisha uwepo katika madaraka kama vile majeshi, polisi tena wale wenye vyeo vya juu. Mwalimu kama wewe unaonekana si lolote kwani suala la elimu bora au duni haliathiri madaraka yao. Mkianza kukimbilia kwenye nchi zenye masilahi kwa wenye taaluma huenda watastuka.

Bonus video hiyo chini, ukiwa na taaluma ni kama vile huyo mwenye convertible car body, hata mtu akikuwahi vipi utapark gari na kumuacha akihangaika kutoka.

Nakushukuru Mkuu, umeongea vizuri. Nashangaa kwanini kwako sehemu ya kulike haipo!.
 
Last edited by a moderator:
ASANTE KUSHUKURU. Ningejua taaluma yako ningekupa connection ya kazi za consultancy. Usianze kutafuta kazi nyingine. utaajiriwa sehemu itabidi usaini ukiingia na kutoka, muda wako utatawaliwa, utapewa dola nyingi lakini utakuwa mtumwa.
kila kitu na wakati wake, tulia hapo ulipo ualimu una heshima yake. Pesa zitakuja tu usiwe na haraka. TRUST ME
 
Nilimaliza chuo miaka kadhaa iliyopita na sasa ni mhadhiri chuo kimoja hapa TZ. Ukweli ni kwamba GPA nzuri (ambayo sasa mi naiita mbaya!) ndio iliyonifanya nishawishiwe na kushawishika kubaki hapo nilipo!, Nikapata nafasi ya kwenda kusoma masters then PhD kwa takriban miaka kama 6 hivi. Tulipomaliza Undergrad kama kawaida watu/classmates tulitawanyika kila mtu kutafuta maisha kwa namna yake. Sasa kwahiyo miaka sita niliyopoteza kwa kusoma, wenzangu walibaki nchini wengine walipata kazi serikalini, wengine kampuni binafsi ambapo huko ni watu wenye vyeo na experience nzuri sana. Ukiachana na hayo ukweli ni kwamba wenzangu wapo mbali sana kimaisha kiasi kwamba nahisi mimi kama vile nilipotea au ile GPA niliyopata ndio iliniponza ingawa kwa wakati ule nilijihisi mi ndio mwenye bahati, lakini naona ni tofauti kabisa hasa nikijilinganisha na wenzangu na hiyo miiaka sita nimefanya maendeleo gani, wenzangu wana mengi sana ambayo mi ndio nafikiria kuanza.

Mbaya zaidi uhadhiri haulipi kabisa, yani ni kutegemea mshahara tu!. Na nikiangalia masenior wangu (Professors etc) hawana maendeleo yoyote, wanalia na njaa tu, wapo wanahangaika na vibiasharabiashara vidogo ambavyo kweli vinachangia kwa wahadhiri wengi kutojiandaa vizuri wanapoingia madarasani kufundisha. Maisha na heshima ya mwalimu wa chuo ni vitu viwili tofauti kabisa (sivyo vile watu wanavyofikiria)!.

Kweli uwalimu ni wito!, lakini kama hauridhiki na unachokipata na hauwezi kujikwamua na maisha magumu na majukumu ambayo unayo kila siku, kweli uwezekano wa kufunza tu ilimradi siku ziende utakuwepo tu miaka yote, sababu utakuwa unatumia muda mwingi kufanya madili mengine nje na kazi ya kufundisha.

Je ni Kweli GPA kubwa iliniponza!! Niache hii kazi nitafute nyingine!!.

Wambie CHADEMA wakupe pesa walizochangisha pale Jangwani, au wakuunganishe na Sabodo.
 
mkuu punguza munkari hata mm niko machimboni lakini baada ya digrii ya kwanza nlifaya kazi kwa muda
ndo nikaenda kusoma tena na sasa nasoma tena lkn sijutii kuwa nimeachwa sana
cha msingi tumia elimu uliyo nayo kutafuta kipato zaidi unaweza kutafuta part time job
vyuo viko vingi kwa sasa vinahitaji walimu wa masaa
pili kuwa mbunifu wa kuandika proposals mbalimbali utapata research za kufanya mbona ziko nyingi tu
inategemea una phd ya kitu gani lkn jitahidi
vipi ukiwa nje hukubeba box au ulileta ubrazameni? nijuavo ukibeba box kwa 3 years ungeweza kufanya
mambo makubwa zaidi ya hao unajotia wamekupita.
 
GPA haina kazi yoyote kwenye kufanyakazi..watu tuna GPA ndogo kama punje ya ulezi lakini tunapiga kazi bab kubwa town hapa acha kabisa walio na ma GPA makubwa kutwa wanatupiga virungu kuomba vocha..tushafahamiana???
 
Kwahiyo soln ni kuamua kupata GPA ndogo kama punje!!.
 
Kwanza hongera kwa hatua hiyo ya kielimu uliyofikia,pia nikupe pole kwa changamoto unazopitia kwani hata mimi yamenikuta,
mimi nilianza kazi ya ualimu mwaka 2005 kama mwalimu shule ya msingi,
nikajiendeleza na kuhitimu shahada yangu mwaka jana august pale duce,
kwa sasa nimerudi kazini ila mwajiri kanipa u-head teacher primary, halafu nikijiangalia sina hata usafiri wa kuendea kazini na sina hata asseti yoyote zaid ya vitu vichache vya ndani,
ila hapa kuna walimu ni form four na cheti ndio ma head teacher, wana nyumba, usafiri ,yaani mpaka nashindwa kuelewa nini maana ya hii elimu niliyoitafta kwa speed na kwa matumaini makubwa,
 
Pole sana mwenzangu, Labda cha kujiuliza wanaposema 'Elimu ni ufunguo wa Maisha' hii Elimu inayomaanishwa hapa ni Elimu ya namna/kiwango gani!!. Mi nadhani ni elimu ya kujumlisha na kutoa tu!, zaidi ya hapo ni kupoteza muda tu!!.
 
Mkuu kuna mtu alisema pale ambapo haupo ndo pazuri, ukiwauliza hao unaosema wana maendeleo utakuta nao wanatamani kuwa na phd kama wewe (kama nimekuelewa vizuri unayo phd), na wewe unawatamani pia.

Lakini niseme hivi, maisha (i.e kupata mali) hakuna fomula kabisaaaaa, ukiangalia vizuri kuna wengine uliwaacha miaka hiyo 6 na hawajafanya chochote, si shule si utajiri, mambo yao bado magumu. So nakushauri wala usikate tamaa, furahia phd yako, kuwa na matumaini, weka malengo na kwa kuwa umesoma vya kutosha nakuhakikishia unaweza kutoka ndani ya miaka 2 au 3 ukawapita hao unaowaona wameendelea sana, ila fanya kazi kwa moyo na watendee haki wateja (students) wako.
Ila pia kila mtu anayo maisha yake, Mungu ni mwema kwa kila mtu haijalishi, so its fine to be challenged and put effort to archieve but dont be jealous, trust God he gave u a phd he will give u the rest of your good desires on due time.

hivi mkuu unaamini kuwa huyu ndugu ana PHD sasa?, mbona maelezo yake yanaelea? ninaamini hana PHD, kama anayo basi hakuisoma yeye,alifanyiwa na mtu
 
mkuu punguza munkari hata mm niko machimboni lakini baada ya digrii ya kwanza nlifaya kazi kwa muda
ndo nikaenda kusoma tena na sasa nasoma tena lkn sijutii kuwa nimeachwa sana
cha msingi tumia elimu uliyo nayo kutafuta kipato zaidi unaweza kutafuta part time job
vyuo viko vingi kwa sasa vinahitaji walimu wa masaa
pili kuwa mbunifu wa kuandika proposals mbalimbali utapata research za kufanya mbona ziko nyingi tu
inategemea una phd ya kitu gani lkn jitahidi
vipi ukiwa nje hukubeba box au ulileta ubrazameni? nijuavo ukibeba box kwa 3 years ungeweza kufanya
mambo makubwa zaidi ya hao unajotia wamekupita.

Mkuu achana na mtoa maada, hiki ni kimeo , anayoyasema hapa siyo ndivyo yalivyo, wewe unakubaliuko chimbo sawa, sema ukweli wako ni sahihi mtu kama huyu kudai ana phd halafu analaumu GPA yake ya bachelor degree? ni kweli amepita kwenye tunnel ya master na PHD huyu?. huyu mtoa maada hana lolote. aidha wewe mkuu unajua unapata kiasi gani kwa sasa, unajua hao wanaosemwa wanatembea na vibahasha maisha yao yakoje, sasa hushangai huyu jamaa malalamiko yake yanatoka wapi?

watu wa aina hii ni wavivu, wape kazi yoyote kwa malipo makubwa kiasi gani wanaishia kulalamika tu. ukitaka kujua anamatatizo mwone anavyoiabudu GPA badala ya kufanya kazi, kweli GPA manake mshahara mkubwa? au maisha bora?

tujifunze kutumia elimu ktk kuendesha maisha na siyo kutumia certificates kuendesha maisha
 
Nilimaliza chuo miaka kadhaa iliyopita na sasa ni mhadhiri chuo kimoja hapa TZ. Ukweli ni kwamba GPA nzuri (ambayo sasa mi naiita mbaya!) ndio iliyonifanya nishawishiwe na kushawishika kubaki hapo nilipo!, Nikapata nafasi ya kwenda kusoma masters then PhD kwa takriban miaka kama 6 hivi. Tulipomaliza Undergrad kama kawaida watu/classmates tulitawanyika kila mtu kutafuta maisha kwa namna yake. Sasa kwahiyo miaka sita niliyopoteza kwa kusoma, wenzangu walibaki nchini wengine walipata kazi serikalini, wengine kampuni binafsi ambapo huko ni watu wenye vyeo na experience nzuri sana. Ukiachana na hayo ukweli ni kwamba wenzangu wapo mbali sana kimaisha kiasi kwamba nahisi mimi kama vile nilipotea au ile GPA niliyopata ndio iliniponza ingawa kwa wakati ule nilijihisi mi ndio mwenye bahati, lakini naona ni tofauti kabisa hasa nikijilinganisha na wenzangu na hiyo miiaka sita nimefanya maendeleo gani, wenzangu wana mengi sana ambayo mi ndio nafikiria kuanza.

Mbaya zaidi uhadhiri haulipi kabisa, yani ni kutegemea mshahara tu!. Na nikiangalia masenior wangu (Professors etc) hawana maendeleo yoyote, wanalia na njaa tu, wapo wanahangaika na vibiasharabiashara vidogo ambavyo kweli vinachangia kwa wahadhiri wengi kutojiandaa vizuri wanapoingia madarasani kufundisha. Maisha na heshima ya mwalimu wa chuo ni vitu viwili tofauti kabisa (sivyo vile watu wanavyofikiria)!.

Kweli uwalimu ni wito!, lakini kama hauridhiki na unachokipata na hauwezi kujikwamua na maisha magumu na majukumu ambayo unayo kila siku, kweli uwezekano wa kufunza tu ilimradi siku ziende utakuwepo tu miaka yote, sababu utakuwa unatumia muda mwingi kufanya madili mengine nje na kazi ya kufundisha.

Je ni Kweli GPA kubwa iliniponza!! Niache hii kazi nitafute nyingine!!.

Pasco

Yesterday 14:46
#11 JF Premium Member
premium.png
Array

Join Date : 22nd September 2008
Posts : 6,889
Rep Power : 0
Likes Received2939
Likes Given7349

[h=2]
icon1.png
Re: Nafasi za Kazi DFID na Ubalozi wa Uingereza: Mshahara kuanzia Milioni 4!.[/h]
Na kwa kuwasaidia tuu wasiojua, mshahara huo ndio mshahara wa mahaji wa Mahakama Kuu ya Rufani na mawaziri wetu na makatibu wakuuu. Ma DC wanalipwa M.2 sambamba na wakurugenzi na wahadhiri wa vyuo vyetu vikuu!. Ma RC wanalipwa M.3 sambamba na majaji wa Mahakama Kuu na manaibu makatibu wakuu na manaibu mawaziri!.

Tukubali tukatae M. 8 Ni pesa ndefu!. AFDB watu wanavuta M.30! per month hapa hapa bongo!.

Angalizo: Money is not everything, job satisfaction ndio mambo yote ndio maana nilipomaliza contract yangu waliomba nirenew nikakataa na sasa nasaga lami na kula vumbi mitaani!. Just do what you love hata kama unapata nothing na sio kukimbilia top paying job that makes millions na kuishia kuwa miserable mtumwa!.

If big money makes you happy, go for it, if you prefer freedom, then think twice!.​

  • kama wewe ni mtanzania na ni PHD holder usingelialia kwa ku pitia GPA wakati una PHD, aidha pasco ameandika wenzako wanacholipwa , sasa kama hata hicho umeshindwa kukimanage kikakupa heshima , unataka heshima akupe nani?., PHD holder unazungumzia madili bila kujua madili nini nini?. unastahili kupata maisha magumu kwakuwa umesoma lakini hujaelimika. aidha wewe ni hatali kubwa hapo unapofundisha kwani hufanani na hiyo kazi
 
Mkuu achana na mtoa maada, hiki ni kimeo , anayoyasema hapa siyo ndivyo yalivyo, wewe unakubaliuko chimbo sawa, sema ukweli wako ni sahihi mtu kama huyu kudai ana phd halafu analaumu GPA yake ya bachelor degree? ni kweli amepita kwenye tunnel ya master na PHD huyu?. huyu mtoa maada hana lolote. aidha wewe mkuu unajua unapata kiasi gani kwa sasa, unajua hao wanaosemwa wanatembea na vibahasha maisha yao yakoje, sasa hushangai huyu jamaa malalamiko yake yanatoka wapi?

watu wa aina hii ni wavivu, wape kazi yoyote kwa malipo makubwa kiasi gani wanaishia kulalamika tu. ukitaka kujua anamatatizo mwone anavyoiabudu GPA badala ya kufanya kazi, kweli GPA manake mshahara mkubwa? au maisha bora?

tujifunze kutumia elimu ktk kuendesha maisha na siyo kutumia certificates kuendesha maisha

Sidhani kama umeelewa nilichomaanisha!! unasoma ukiwa baa nini!!.
 
Pasco

Yesterday 14:46
#11 JF Premium Member
premium.png
Array

Join Date : 22nd September 2008
Posts : 6,889
Rep Power : 0
Likes Received2939
Likes Given7349

icon1.png
Re: Nafasi za Kazi DFID na Ubalozi wa Uingereza: Mshahara kuanzia Milioni 4!.

Na kwa kuwasaidia tuu wasiojua, mshahara huo ndio mshahara wa mahaji wa Mahakama Kuu ya Rufani na mawaziri wetu na makatibu wakuuu. Ma DC wanalipwa M.2 sambamba na wakurugenzi na wahadhiri wa vyuo vyetu vikuu!. Ma RC wanalipwa M.3 sambamba na majaji wa Mahakama Kuu na manaibu makatibu wakuu na manaibu mawaziri!.

Tukubali tukatae M. 8 Ni pesa ndefu!. AFDB watu wanavuta M.30! per month hapa hapa bongo!.

Angalizo: Money is not everything, job satisfaction ndio mambo yote ndio maana nilipomaliza contract yangu waliomba nirenew nikakataa na sasa nasaga lami na kula vumbi mitaani!. Just do what you love hata kama unapata nothing na sio kukimbilia top paying job that makes millions na kuishia kuwa miserable mtumwa!.

If big money makes you happy, go for it, if you prefer freedom, then think twice!.​

  • kama wewe ni mtanzania na ni PHD holder usingelialia kwa ku pitia GPA wakati una PHD, aidha pasco ameandika wenzako wanacholipwa , sasa kama hata hicho umeshindwa kukimanage kikakupa heshima , unataka heshima akupe nani?., PHD holder unazungumzia madili bila kujua madili nini nini?. unastahili kupata maisha magumu kwakuwa umesoma lakini hujaelimika. aidha wewe ni hatali kubwa hapo unapofundisha kwani hufanani na hiyo kazi

Mi hatari kiasi gani ndugu!! wakati mwingine bora kusema ukweli kuliko kuumia tu moyoni, Ni elimu gani nitakayoweza kuitoa vizuri kwa wanafunzi wangu, wakati sina uwezo wa kukabiliana na majumu ambayo ninayo kila siku, sina uwezo wa kuwapeleka watoto wangu shule nzuri. Sina..... sina.... sina..... darani wanafunzi 200 mpaka 500 uwahudumie vizuri, sivyo hivyo unavyofikiria ndungu. Usione wahadhiri wanatembea ukadhani mambo yao safi. Ungekuwa kwenye hiki kiatu ungeelewa kama ni cha size gani!!. Kama nimekukera kusema kilicho moyoni mwangu basi we mezea tu. Lakini huo ndio ukweli. Na nakwambia utakuwa shahidi baada ya miaka michache vyuo vyetu vinaweza visiwe na walimu tena kama hiyo serikali yako haitachukua maamuzi ya busara.
 
kwa kifupi jamani, lazima mtofautishe maProf. na maDr. wa zamani enzi zao wakati wanaanza kazi mambo yalikuwa ni mazuri, kwahiyo waliweza kufanya investments mbali mbali na ndio hao mnaowaona nyie kwamba ni mambo safi. Lakini sisi tunaoibukia sasa hali ni ngumu, ngumu tena ngumu sana (ielweke hivyo)!. Kipato na majukumu ambayo tunayo hayafanani kabisa, yani kushoto na kulia kabisa. Zamani walikuwa na madarasa yenye wanafunzi 20 mpaka 40. sasa madarasa yana wanafunzi mpaka 500. huo muda wa mambo mengine utautoa wapi!!. Hebu tujaribui kutofautisha wa zamani na sisi vijana tunaoibukia!!.
 
mkuu pole sana, naona upo katika dimbwi la mawazo kuhusu mafanikio ya wenzako uliokuwa nao school, hata wewe hujachelewa maana mafanikio ni kujipanga na kutekeleza yale unayoitajika kuyatekeleza kama hawa jamaa hapa chini wanavyosema: "there are no secrets to success. It is the result of preparation, hard work, and learning from failure." - colin powel "the man who follows the crowd will usually get no further than the crowd. The man who walks alone is likely to find himself in places no one has ever been." - alan ashley-pitt "successful people are always looking for opportunities to help others. Unsuccessful people are always asking, 'what's in it for me?'" - brian tracy "if you don't set goals, you can't regret not reaching them." - yogi berra "success is achieved by those who try and keep trying with a positive mental attitude." - w. Clement stone "a native american grandfather was talking to his grandson about how he felt. He said, 'i feel as if i have two wolves fighting in my heart. One wolf is the vengeful, violent one, the other wolf is the loving compassionate one.' the grandson asked him, 'which wolf will win the fight in your heart?' the grandfather answered, 'the one i feed.'" - blackhawk

like,like,like !!
 
Brother, najaribu kujiweka kwenye shoes zako.....nahisi kimsingi hujasomea kitu unachokipenda bali ni yale mambo ya nafasi za uchina/asia na eastern europe.....mwisho wa siku unamaliza unagundua hiyo elimu kwako sio mafanikio....lakini yaliyopita si ndwele.......chakufanya hapo ni kuitumia hiyo PhD kama vile kufanya consultancy, ku-partner na watu wenye pesa kuanzisha biashara...wewe unajina na taaluma unaweza kuuza jina kupata mafanikio......

Vile vile unaweza kuamua kwenda nchi ambazo ualimu unalipa ukapata pesa nzuri kama mdau alivyoshauri hapo juu........lakini pia ukiwa makini hao waliokutangulia unaweza kuwakuta na kuwapita..........

hatujui taaluma yako lakini pia unaweza kuanzisha kampuni yako kutokana na taaluma kwasababu ninavyojua ualimu wa chuo haubani sana.......kimsingi maisha ni jinsi uyaonavyo......kuhusu GPA sidhani kama ili kuponza...isipokuwa desperation na hali ya insecurity watu wana yokuwa nayo wakimaliza chuo huamua kuchukua the first offer....wachache wanaotulia na kufikiri nini hasa cha kufanya.........
 
1. Lakini pia ni wavivu kuchanganyika na watu wa kitaa hawa wasomi wetu......wanajiona special na wanadhani wanajua mambo mengi eti.....jamani eenh mafanikio ya ofisini yanapatikana kwa watu wachache saaana ambao wanapata gud pay.....wengi ni deal tu kwenda mbele na hawa wasomi wengi sio wazuri kwenye mishe za kitaa ambazo ndo zinatusua

2. Wahadihiri wamezoea superiority huko vyuoni na baadhi wanakuwa na attitude flani kama ya mtoa mada kwamba amesoma so anatakiwa awe juu kimapato n ol that ndo maana wakija huku kitaani hata wakipewa michongo wanaona kama sio ya hadhi yao vile......jishusheni kidogo na mjue Street Uni. inasongaje kwa Bongo hapa

unayoyasema ni kweli kabisa
wahadhili wengi wanaamini wanaakili zaidi ya watu wengine kwakuwa walipata GPA kubwa. ndo maana wakisha pata PHD zao wanadhani watakula bure- hakuna hiyo. pia wakumbuke hizo research opportunities and funding zipo mikononi mwa watu waliopata GPA za chini , sasa kwakuwa wahadhili hawa feki wanaona kushirikiana na watu wa GPA ya chini watadhalilisha PHD zao hawatoi ushirikiano na mwisho wanasema hakuna research au hakuna pesa.

suala la mtu kusema anawafunzi wengi darasani, hiyo ndo kazi yake, hapo ndo aonyeshe uwezo wake na siyo kulalamika tu. eti wanafunzi 500 ni wengi, na hii PHD aliipataje?.
wahadhili waache kulalamika , either watafute mabadiliko huko ndani ya vyuo vyao, au waache kazi watafute nyingine nje ya kufundisha wakafanye, lakini ninachafahamu hata wakija huku mtaani , hawa jamaa watashindwa ku cope kutokana na mitazamo yao ya ajabu ajabu
 
Sidhani kama umeelewa nilichomaanisha!! unasoma ukiwa baa nini!!.

Lecturer, kama ambavyo umekuwa mvivu wa kuchukua ushauri huu,ndiyo utaendelea kuona kazi yako haikulipi,

nakushauri tena, achana na hiyo kazi ya kufundisha , karibu huku mtaana. angalizo, kabla hujaacha hakikisha upotayari kwa changamoto za huku mtaani, kwakuwa hata hizo kitu unaita dili haziletwi tu kiulaini kama hii hewa tunayovuta hapa duniani ambayo Mungu anatupatie bure bila kuumiza vichwa vyetu kuitafuta
 
Back
Top Bottom