Je ni kweli GPA Kubwa iliniponza!! Nimechemsha au!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je ni kweli GPA Kubwa iliniponza!! Nimechemsha au!!

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by BIG Banned, Jun 2, 2012.

 1. BIG Banned

  BIG Banned JF-Expert Member

  #1
  Jun 2, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 263
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nilimaliza chuo miaka kadhaa iliyopita na sasa ni mhadhiri chuo kimoja hapa TZ. Ukweli ni kwamba GPA nzuri (ambayo sasa mi naiita mbaya!) ndio iliyonifanya nishawishiwe na kushawishika kubaki hapo nilipo!, Nikapata nafasi ya kwenda kusoma masters then PhD kwa takriban miaka kama 6 hivi. Tulipomaliza Undergrad kama kawaida watu/classmates tulitawanyika kila mtu kutafuta maisha kwa namna yake. Sasa kwahiyo miaka sita niliyopoteza kwa kusoma, wenzangu walibaki nchini wengine walipata kazi serikalini, wengine kampuni binafsi ambapo huko ni watu wenye vyeo na experience nzuri sana. Ukiachana na hayo ukweli ni kwamba wenzangu wapo mbali sana kimaisha kiasi kwamba nahisi mimi kama vile nilipotea au ile GPA niliyopata ndio iliniponza ingawa kwa wakati ule nilijihisi mi ndio mwenye bahati, lakini naona ni tofauti kabisa hasa nikijilinganisha na wenzangu na hiyo miiaka sita nimefanya maendeleo gani, wenzangu wana mengi sana ambayo mi ndio nafikiria kuanza.

  Mbaya zaidi uhadhiri haulipi kabisa, yani ni kutegemea mshahara tu!. Na nikiangalia masenior wangu (Professors etc) hawana maendeleo yoyote, wanalia na njaa tu, wapo wanahangaika na vibiasharabiashara vidogo ambavyo kweli vinachangia kwa wahadhiri wengi kutojiandaa vizuri wanapoingia madarasani kufundisha. Maisha na heshima ya mwalimu wa chuo ni vitu viwili tofauti kabisa (sivyo vile watu wanavyofikiria)!.

  Kweli uwalimu ni wito!, lakini kama hauridhiki na unachokipata na hauwezi kujikwamua na maisha magumu na majukumu ambayo unayo kila siku, kweli uwezekano wa kufunza tu ilimradi siku ziende utakuwepo tu miaka yote, sababu utakuwa unatumia muda mwingi kufanya madili mengine nje na kazi ya kufundisha.

  Je ni Kweli GPA kubwa iliniponza!! Niache hii kazi nitafute nyingine!!.
   
 2. t

  thinka JF-Expert Member

  #2
  Jun 2, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 335
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  jarib kujifunza kwa wenzako wamefanikiwaje inaweza kukusaidia ila sio kuacha kaz
   
 3. MJIMPYA

  MJIMPYA JF-Expert Member

  #3
  Jun 2, 2012
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 465
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Mkuu kuna mtu alisema pale ambapo haupo ndo pazuri, ukiwauliza hao unaosema wana maendeleo utakuta nao wanatamani kuwa na phd kama wewe (kama nimekuelewa vizuri unayo phd), na wewe unawatamani pia.

  Lakini niseme hivi, maisha (i.e kupata mali) hakuna fomula kabisaaaaa, ukiangalia vizuri kuna wengine uliwaacha miaka hiyo 6 na hawajafanya chochote, si shule si utajiri, mambo yao bado magumu. So nakushauri wala usikate tamaa, furahia phd yako, kuwa na matumaini, weka malengo na kwa kuwa umesoma vya kutosha nakuhakikishia unaweza kutoka ndani ya miaka 2 au 3 ukawapita hao unaowaona wameendelea sana, ila fanya kazi kwa moyo na watendee haki wateja (students) wako.
  Ila pia kila mtu anayo maisha yake, Mungu ni mwema kwa kila mtu haijalishi, so its fine to be challenged and put effort to archieve but dont be jealous, trust God he gave u a phd he will give u the rest of your good desires on due time.
   
 4. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #4
  Jun 2, 2012
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,169
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Wivu wa maendeleo, nimeupenda
   
 5. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #5
  Jun 2, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Usikate Tamaa ingia REDET kama mkandara mambo yako yatakua safi tu,kuna jamaa tulimaliza nae chuo miaka hyo alikua na Bonge la GPA alisaga lami mwaka na nusu mtaani.
   
 6. A

  Andrew Jr JF-Expert Member

  #6
  Jun 2, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Ni ukweli usiopingika, GPA na kufanikiwa mtu kimaisha ni vitu 2 tofauti. Watu wanapew GPA zisizo zao, unaweza kumkuta mtu ana GPA ndogo lakini content anayo kubwa sana. Kuna hatari mwenye GPA kubwa ukimbana akashimwa kuitetea. Kwa hiyo falsafa ya Maisha bado itabaki kuwa ni akili ya Mtu
   
 7. Goodrich

  Goodrich JF-Expert Member

  #7
  Jun 2, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 2,050
  Likes Received: 632
  Trophy Points: 280
  Inaonyesha wazi kabisa kuwa elimu yako haijakusaidia kuwa na upeo!!!
  Kwanza sio maadili kabisa (professional ethics) kwa msomi kama wewe kuandika mambo kama haya yenye muelekeo wa kulinganisha elimu na kipato.
  Pili ujue kwamba mafanikio sio kujenga au kuwa na gari au kuwa tajiri. Mafanikio ni kufikia malengo. Hiyo phd yako ni mafanikio makubwa kuliko hao wenye utajiri.
  Tatu Elimu hailinganishwi na utajiri. Kumbuka wakati upo sekondari wenzako walioishia la saba wengine walikuwa matajiri tayari.
  Mwisho, nimegundua kuwa una elimu ya darasani lakini huna Hekima. Anza sasa kujifunza hekima !!!

   
 8. E

  ELX JF-Expert Member

  #8
  Jun 2, 2012
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 259
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 60
  naungana nawe goodrich,
  je, kama kweli yeye ni mhadhili na kwa upeo wake kaonesha kuwa elimu si kitu ila ni kupoteza muda sasa anafanya nini? Je, anawajengea nini wanafunzi wake? Wote waache shule waingie kwenye ujasiliamali? Naamini kweli kama ni mhadhili na kasoma atumie elimu yake kujijienga zaidi, kuna consultation anaweza fanya zikamuingizia hela na wakati huo anaendelea kutoa utaalam kwa wanafunzi!
  Nimeamini "kusoma sana si kuelimika"
   
 9. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #9
  Jun 2, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Jamani mafanikio ni kupata maendeleo katika maisha na sio elimu.Unaweza ukawa unaelimu lakini ukawa huna maisha mazuri uki compare na wenzako.Hapo elimu yako haijakusaidiao
   
 10. MKATA KIU

  MKATA KIU JF-Expert Member

  #10
  Jun 2, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,167
  Likes Received: 966
  Trophy Points: 280
  Kaka acha presha shule haileti utajiri hata siku moja, angalia list ya matajiri 1000 duniani kama kuna proffessor hata mmoja, au anzia tanzania tafuta list ya kibongo kama kuna profesa au mwenye shuke ya kutisha, au huko mbali tuanzie mtaani kwako wa akina masawe, mangi na bishanga kama kuna profesa anaongoza kwa utajiri

  Kutengeneza pesa ni skills nyingine isiyoendana na madesa kabisa, shule ni all about theories but maisha ni real practical things, my mother ni lecture wa miaka mingi sana alishatuambia na anaendelea kutuambia shule haileti utajiri hata siku moja zaidi ya kujenga nyumba 2 au 3 na kuendesha japanese car hata usome vipi,

  Making money needs to be street wise and creativity... hata siku moja usifikirie intergration na hesabu za cos sijui tan x zitakufikisha levo ya kumsomesha mtoto havard au alabama kwa pesa yako mwenyewe.. Hiyo ni street degree ambayo haipimwi na gpa...

  Wasomi wameletwa ili waajiriwe na wafanyabishara kuwasaidia kupata utajiri sio kuwazidi utajiri.. B mkubwa anapendaga kusema hivyo na baada ya kumaliza xul nimeanza kuamini alichokisema ni ukweli
   
 11. Bazazi

  Bazazi JF-Expert Member

  #11
  Jun 2, 2012
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 2,029
  Likes Received: 558
  Trophy Points: 280
  GPA = Grade Point Average ukiwa na daraja la kwanza hongera. Wengine tuliondoka na Likikwete na tunapeta maishani.

  Tuyaacha mapuuza. Tumia elimu yako na mashahara wako kidogo upatao kuanzisha mradi uliokatikafani yako naamini utafanikiwa.
   
 12. odinyo

  odinyo JF-Expert Member

  #12
  Jun 2, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 428
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Mkuu,

  Kama kweli ww ni msomi mwenye GPA kubwa na umeendelea kama ulivyoadithia basi
  usitupotoshe wenzio na wengine wenye nia nzuri ya kufanya/kusoma kwa jitihada kupata marks nzuri,
  kwako ww si tu uhaziri bali ndio uliandikiwa kua na maisha hayo. je hujaona mtu akawa na mali kibao then akarudi kua hana kitu?!!

  acha kudidimiza watu. ndg zangu tusome tena kwa jitihada kubwa, hiyo ndio funguo ya maisha
   
 13. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #13
  Jun 2, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,963
  Likes Received: 1,850
  Trophy Points: 280
  nimesoma comments za nyote wana jf ila kunakitu naona kama mmekisahau vile mtoa mada ana hoja ya msingi sana tena siyo ya kupuuzwa hata kidogo

  kwanza kabisa katuonyesha dhahiri kuwa alikuwa na bidiii sana lkn returs of investment are poor. hil linatokana na mfumo tu uliopo wa serikali yetu kuwa hata kama umesoma mishahara bado ni midogo na hapa kwetu Tz serikali haitulipi kutokana na tunavyo deliver. swala hili hata hao wahadhiri wa vyuo kupitia bodi zao huwa nwanalalamika sana, so ni tatizo la kitaifa.

  pili mtu unapoondoka kwenda nje kusoma, utajitahd sana na utapenda urudipo uje ufanikiwe haraka zaid kwani tayari unayo exposure kubwa lkn hali hii huwa ni tofaut kabisa kwani kwanza utakuwa umeshapoteza network yako na wale close friends. kitu ambacho itakugharimu kama miaka 2 hivi kuirudisha.

  wenzio waliobaki ni kwasababu ya good networking unakuta mtu anatoka hata kama anakipato kidogo.

  ushauri wangu dont dare give up, create good networking as possible as yuo can. usilete ubrazamen wa kutoka ulaya hapa kaa hata kwenye migahawa ya kawadia kula na kunywa ili upate network, ukiweza kuipata hii basi utaona ndani ya mwaka mambo ni mazuri manake source of capital tayari ipo. tafuta kazi kwenye miradi, wwrite your propasal for different projects ukipata fanya na ionekana imefanakiwa basi lazima utatoka tu.
   
 14. Tmlekwa

  Tmlekwa Senior Member

  #14
  Jun 2, 2012
  Joined: Apr 27, 2012
  Messages: 184
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  yes kaka,ushaur wako mzur sana.mungu ndo mtoaji wa kila kitu na hutoa kwa wakat.wakat ukifika utaona kila jambo linakuja automatical
   
 15. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #15
  Jun 2, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Unaposema wenzako wako mbali kimaisha unamaanisha nini?

  Je, ulipokubali kuingia kwenye uhadhiri ulikuwa na mipango gani kimaisha?

  Je, unafahamu kuwa academicians hupata mapato zaidi kwa kupitia grants za tafiti na miradi mbalimbali, je umewahi kuapply grants ngapi? Je, umebuni projects ngapi?

  Baada ya kujibu haya maswali jiulize kama cha kulaumu ni GPA, uhadhiri au your own lack of creativity?!!!
   
 16. Mapi

  Mapi JF-Expert Member

  #16
  Jun 2, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 6,871
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Goodrich umeandka vyema ila umesehau ulichokisema kwamba "mafanikio ni kufikia MALENGO" sasa yeye anaomba ushauri kwani hajafka hapo na elimu aliyonayo hajasema ndio yaliyokuwa malengo yake.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #17
  Jun 2, 2012
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Wazo zuri, ila si suala la GPA ndo limekuponza ni wewe ndo ulipenda kubakia kufundisha na ukaona raha kufundisha. Unaweza toka hapo ulipo ukatafuta sehemu nyingine inayolipa zaidi, maisha haya yakutegemea mshahara tu hayaendi... ila uwaulize wengine hao wamafikaje hapo walipo isije ikawa ni uifsadi maofisini...hi si sahihi, Nenda pale penye malipo halali. Mwenyewe ni jana tu nilikuwa naongea na rafiki yangu aanaiulizia kuhusu kusoma PHD nikasema wapi, sasa naangalia kutafuta pesa, after all udr wenyewe usio na results kwa nchi, majina tu akhuuu... Wapo kina Diamond, Ray ni mamilionea na viform 4 vyao wanapeta, ukimwambia achangie milioni 1 kwa mafuriko anatoa fsata we dr unatoa macho.
   
 18. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #18
  Jun 2, 2012
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Hapo si sahihi...kabisa...imani inatufundisha kubweteka na kujipa moyo eti iko siku utapewa, wapo wengi tu wamekufa na umaskini wao tena kwa kukosa pesa za matibabu. Suala kubwa ni kustruggle, Mungu hubariki kazi ya mikono yako. Kuna watu mashuleni walikuwa kutwa na kusali eti Mungu atawafaulisha wakiashia mazero na kudisco. Kaa hapo hapo useme automaticaly vitakuja.
   
 19. BIG Banned

  BIG Banned JF-Expert Member

  #19
  Jun 2, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 263
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Malengo ni nini ndugu yangu!!, Na hekima ni nini!!
   
 20. BIG Banned

  BIG Banned JF-Expert Member

  #20
  Jun 2, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 263
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ndugu Kifupi ni kwamba hayo unayosema si rahisi kwa TZ, ndio mana wataalam wote wanakimbilia kwenye siasa.
   
Loading...