Je, naweza kutumia fungu la kumi kwa kununua mahitaji ya watoto yatima?

Fungu la kumi ni fungu la Mungu, peleka madhabahuni unapoabudia.
Kitabu cha Yoeli Mungu anasema mnaniibia kwa kutotoa zaka, leteni zaka kamili ghalani Ili kiwepo chakula nyumbani mwangu.

Misaada kwa yatima hiyo ni sadaka.
Fungu la Mungu au fungu la mchungaji? Hawa hawa manabii wetu wa siku hizi uwapelekee fedha halafu useme umepeleka kwa Mungu? Hawa hawa kina Gwajima na Mzee wa Upako au kina Mwamposa? Kina 'nabii'' Malisa?
 
Je, fungu la kumi linaweza tolewa kwa wajane, yatima na wenye shida au ni lazima nikatoe kanisani?

Naomba hekima zenu juu ya hili.
Mkuu hiyo ela pelekea watu wenye uhitaji, japo fungu la kumi linapaswa kwenda kanisani.

Nakuomba hiyo pesa pelekea watoto wenye kuishi mazingira magumu, kama utashindwa kufanya hivyo kula mbuzi choma mpaka hiyo pesa iishe.
Kama ni mkristo agiza kitimoto nusu nusu mpaka pesa iishe utaongeza afya na utapata nguvu ya kutafuta nyingine.
 
Fungu la Mungu au fungu la mchungaji? Hawa hawa manabii wetu wa siku hizi uwapelekee fedha halafu useme umepeleka kwa Mungu? Hawa hawa kina Gwajima na Mzee wa Upako au kina Mwamposa? Kina 'nabii'' Malisa?

Kama huwelewi maandiko omba uelekezwe,fungu la 10 lilitolewa maalumu kwa wana walawi waliokua ni makuhani na waangalizi wa hekalu,ambao hata katika urithi wa ardhi hawakupewa,hivyo ili waishi na kuendelea kuhudumia hekalu fungu la 10 lilipelekwa hekaluni
 
Maandiko yanasema hivyo nakubali. Swali: wana wa walawi wa sasa ni sawa na wale wa zamani? Makuhani wa sasa ni sawa na wale wa zamani? Waangalizi wa hekalu wa sasa ni sawa na wale wa zamani? Hawa wa sasa mbona wanapewa urithi wa ardhi na ''wanatafuna'' kondoo huku wakijirekodi na simu?
 
Kama huwelewi maandiko omba uelekezwe,fungu la 10 lilitolewa maalumu kwa wana walawi waliokua ni makuhani na waangalizi wa hekalu,ambao hata katika urithi wa ardhi hawakupewa,hivyo ili waishi na kuendelea kuhudumia hekalu fungu la 10 lilipelekwa hekaluni
Na ndomana Mungu anasema leteni zaka kamili Ili kiwemo chakula katika nyumba yangu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom