KAMA UNAFIKIRI KUHUSU UTHIBITISHO KIASI HICHO ULIKUWA NA HAJA GANI YA KUAMINI MUNGU?MAANA INAONESHA HADI SASA HAUJAONA HATA DALILI YEYOTE AU ATHARI YA KUAMINI MUNGU,SASA KWANINI UNAENDELEA KUAMINI?Unajua mkuu, binafsi sina shida kabisa na mtu anayemini chochote, either Mungu yupo au hayupo, kwangu mimi wote wako sahihi.
Sababu kubwa ni kwamba, wote, wanaoamini kuwa yupo na wale wasioamini kuwa yupo, hakuna mwenye uthibitisho wa 100%. Zote zinabaki kuwa ni imani.
Lakini shida inakuwa moja, mtu anataka kulazimisha imani ya kuwa yupo au hayupo ili hali hata kuthibitisha uwepo au ukutokuwepo wake hawezi.
Mi binafsi msimamo wangu kuhusu haya mambo ni huu, kwamba japokuwa ni muumini wa dini ya Kikristu, lakini kiuhakika siwezi kuthibitisha kuwa Mungu yupo au la!
Cha msingi ni kuwa, kila mtu asimame katika imani yake, na yupo sahihi katika hiyo imani yake. Ila asianze kudharau imani ya mtu!!
Mkuu, hata nisipoamini kuwa kuna Mungu ni sawa tu na kuamini kuna Mungu, hakuna tofauti yoyote ya kifizikia.KAMA UNAFIKIRI KUHUSU UTHIBITISHO KIASI HICHO ULIKUWA NA HAJA GANI YA KUAMINI MUNGU?MAANA INAONESHA HADI SASA HAUJAONA HATA DALILI YEYOTE AU ATHARI YA KUAMINI MUNGU,SASA KWANINI UNAENDELEA KUAMINI?
Basi wewe hauamini Mungu au hauna hakika na unachoamini na ndio maana unaamini Mungu bila dalili yeyote.Mkuu, hata nisipoamini kuwa kuna Mungu ni sawa tu na kuamini kuna Mungu, hakuna tofauti yoyote ya kifizikia.
Mi nimemua kuwa mfuasi wa dini ya kikristu, kwa sababu kadhaa, lakini kubwa ni maamuzi tu binafsi!!
Lakini kwa maoni yangu, kuwa mfuasi wa dini au dhehebu flani angalau kunaleta ahueni na faraja kwamba shida tupitiazo yupo ambaye atatutatulia kwa imani.
Pia, kujumuika na watu kwa lengo flani, kunawafanya muwe na mahusiano ambayo yanaweza yakaleta matokeo chanya baina yenu, kama vile upendo, faraja, ushirikiano, n.k
Sababu hizo haziifanyi imani niliyonayo iwe ndio sahihi kuliko imani za wengine.
Na wala kiwa katika imani hii, hakuniwezeshi kuwaaminisha watu wasio wa imani yangu waamini, kumuona na kujua kuwa kweli Mungu yupo. Uwepo wa Mungu mimi siujui ukweli wake aisee!!
Bwana Tz mbongo, Je, imani yako ndio sahihi kuliko za wengine!?
Mimi sijui kama Mungu yupo.Basi wewe hauamini Mungu au hauna hakika na unachoamini na ndio maana unaamini Mungu bila dalili yeyote.
Hata huyo shetani alifanya dhambi na ndio sababu ya hadi kuitwa shetani ila hakuumbwa akiwa ni shetani.Kwa hiyo tunaweza kusema uwepo wa dhambi hautegemei uwepo wa shetani?
yaani shetani anajitegemea na dhambi inajitegemea?
Kutokujua kwa maana ipi yani unaposema hujui kama Mungu una maanisha nini?
Kutokujua kwa maana ipi yani unaposema hujui kama Mungu una maanisha nini?
Hebu thibitisha kwamba Baba ni mwanaume?Mkuu, kwani kujua ina maana ngapi!?
Kujua ni kuwa na uhakika na kuweza kuthibitisha jambo. Kwa mfano, mimi ninajua kwamba Baba ni mwanaume!!
Sent using Jamii Forums mobile app
Au mwenzangu baba yako ni mwanamke!?[emoji23]Hebu thibitisha kwamba Baba ni mwanaume?
Umezungumzia kuhusu kuthibitisha kwamba umesema kujua ni kuwa na hakika na kuweza kuthibitisha,sasa kuwa na hakika ni kutokuwa na shaka ila hapo kwenye kuthibitisha ndipo nilipotaka kupaelewa.
Sasa kwanini katipa Challenge ilihali sisi ni kazi ya mikono yake!?
Ndio ushangae sasa " ... vitu vingine ni nonsense tu ... ujinga mtupuNimekumbuka yule dogo aliyewashitaki wazazi wake kwa kumzaa mzungu badala ya mweusi
Hivi siku ya kiama haiwezekan kukata rufaa ukihukumiwa kwenda jehanam!?
Kwanza wewe hukuomba uumbwe ila yeye ndio alikuumba kwa malengo yake sasa kosa lako ni nini hadi upelekwe jehanam?
HahahaaMimi tangu nilipo jua MUNGU hua anapiga story na shetani na mazungumzo yao yamekaa kirafiki nikaamua kuacha kumchukia shetani
Hahaaa unamchukia wakati mwenzio anapiga Story na mungu ..siujinga huoUsicheke mkuu mi sahiv nafanya mpango niwe karibu na shetani sina sababu ya kumchukia
HahahaMungu na shetan wanawachora tu uku wanagonga cheers [emoji23][emoji23][emoji23]
Hahaha sasa sianamuonea tuWatakuja kusema sijui kuna freewill wanasahau kuwa mjuzi wa yote, Mpangaji wa yote tayari amepanga na kujua nini utafanya yani Mungu kwa sifa za upangaji na Ujuaji wa yote basi alipanga na kujua kuwa Kiranga hatamuamini na atamchoma moto
DHAMBI NI NINI?Wakuu hamjambo!
Kama kichwa cha Uzi huu kinavyouliza, Mimi nikiri kuwa naamini uwepo wa Mungu mmoja aliyeumba vyote vinavyoonekana na visivyoonekana pia.
Katika vitabu mbali mbali vya dini, tunaelezwa kuwa dhambi ilitokana na uasi alioufanya shetani dhidi ya Mungu, biblia inaenda mbali kwa kudai kuwa vita vilipiganwa huko mbinguni na shetani alishindwa na akatupwa duniani akiwa na theluthi ya malaika wakawa upande wake.
Maswali:
1. Ikiwa kabla ya shetani kuasi hakukuwa na dhambi yoyote ile, tena alikuwa mbinguni kwenye utakatifu wa MUNGU, je shetani alishawishiwa au alitoa wapi mawazo ya uasi Ikiwa hakukuwa na shetani yeyote mwingine?
2. Kama MUNGU hujua mwanzo hata mwisho wa viumbe vyake, INA maana alikuwa anajua kuwa shetani atakuja kuasi baadae na kusababisha dhambi, kwanini alimuumba?
Jambo la kufikiria hapa ni kuona kwamba MUNGU alimuumba shetani/Lucifer ( dhambi) mahususi ili kuja kuwa upande maovu. Dhana hii inadhihirisha kuwa MUNGU ndie aliyeumba dhambi.
3. Je, lengo la MUNGU lilikuwa mwanadamu aishi milele bila kufa?
Hapa kuna mazoea yalishajengeka hasa kwa wakristo na waislamu kuamini kuwa isingekuwa Eva/Hawa kudanganywa na Shetani basi Leo hii wanadamu wasingekuwa wanakufa ( immortal). Hii dhana haina mantiki hasa ukiwaza kuwa wanadamu wangezaliana na kuishi milele bila kufa nadhani dunia ingekuwa imejaa mabara na visiwa vyote.
Hivyo MUNGU akaamua kuleta mauti ili kudhibiti ( control) idadi ya wanadamu duniani isizidi uwezo wa rasilimali zilizopo, fikiri Leo hii watu wanauwana kugombania ardhi je ingekuwaje akina Adam na bibi yetu Eva wangekuwepo wote?
4. Je, Dini ni matokeo ya mwanadamu kumhofia shetani?
Tunaishi katika jamii ambazo kila MTU ana juhudi za kujikwamua kuondokana na shida Kama magonjwa, njaa, vita, ambazo Mara nyingi wanadamu wanahesabu kuwa hayo yote ni sababu ya shetani, na dini wanaona ndio kimbilio ili kumkwepa shetani asiwadhuru.
Lakini wao wanaamini kuwa wanasali ili kumtukuza MUNGU, lakini kiukweli dini ni hofu ( fear of unknown) isiyo na ithibati yoyote.
5. Je, Mungu anawapenda wanadamu? Hapa jibu laweza kuwa ni ndiyo, bahati mbaya sana ukiangalia uhalisia toka zamani kuna ugumu wa kusema ndiyo au hapana.
Tunaambiwa kuwa mbinguni kulikuwa na vita Kali sana, mwaishowe malaika aitwaye Mikaeli alimshinda shetani, Mungu akamtupa ibilisi huyo huyo duniani kwa wanadamu anaowapenda sana. Mungu hakuona sehemu nyingine ya kulitupa hilo joka ila duniani ambako ndio wanadamu aliwaweka. Hii ni sawa na kuwarushia watoto wako furushi lenye nge wengi huku umewafungia chumbani na kuwataka wajikinge wasing'atwe hata kidogo.
Nimekuja kuamini kuwa: MUNGU yupo ila dini zote ni michezo ya kukamata fikra za wanadamu tu, inawezekana kabisa kuwa dini ziluletwa na shetani mwenyewe ili kuwachonganisha wanadamu wasiishi kwa upendo na amani.
Angalia jinsi Palestine na Israel, syria , Iraq n.k wanavyouana kwa misingi ya dini.
Niishie hapo, naomba waumini/maswahaba mje mtueleze hizi hoja.
Cc: Mshana Jr
Cc: Kiranga
Na wanajamvi wote karibuni.
3. Je, lengo la MUNGU lilikuwa mwanadamu aishi milele bila kufa?
Hapa kuna mazoea yalishajengeka hasa kwa wakristo na waislamu kuamini kuwa isingekuwa Eva/Hawa kudanganywa na Shetani basi Leo hii wanadamu wasingekuwa wanakufa ( immortal). Hii dhana haina mantiki hasa ukiwaza kuwa wanadamu wangezaliana na kuishi milele bila kufa nadhani dunia ingekuwa imejaa mabara na visiwa vyote.
Hivyo MUNGU akaamua kuleta mauti ili kudhibiti ( control) idadi ya wanadamu duniani isizidi uwezo wa rasilimali zilizopo, fikiri Leo hii watu wanauwana kugombania ardhi je ingekuwaje akina Adam na bibi yetu Eva wangekuwepo wote?