Je, MSD na Brig. Gabriel Mhidize, Itawezekana?

Je, MSD na Brig. Gabriel Mhidize, Itawezekana?

Vitengo mnahasira,ngoja tuone mpambano.
Hata iwe global health supply chain

Nothing you spoke represent mtu mwenye uwezo wa kujadili global health supply chain

Zaidi Ni majungu

Hujafanya any analysis iwe ya logistics, modeling , demand etc.

Umemshambulia mtu na watu na majungu

Hujaonyesha chochote chenye depth ya kutambua technical solutions

In short una hasira na watu halafu ukaibeba MSD kwenye hasira zako
.hatujengi nchi kwa mtindo huo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo unayejaribu kumparamia humuwezi sio size yako atakurarua rarua kama tai.
Hapana

Madawa na vifaa tiba Ni essential live saving things

Majadiliano yake na solutions zake zinahitaji depths, capabilities and solutions na sio majungu

Alikua wapi siku zote kuibua mahusiano yasiyofaa ya Hawa viongozi?

We need more

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Si unajua Wahaya tena. Nshomile

Uwe na dharau uwe na elimu. Mwenzie anaitwa Brig. Dr. General......
Yeye anaitwa Bw. Laurean ha ha ha halafu unakuwa na dharau


Mk54
 
MSD INASUMBULIWA NA TARATIBU ZA KIMANUNUZI PAMOJA NA DENI WANALODAI HOSPITAL MBALI MBALI. WEWE MTOA MADA HUJUI KITU. USIFIKIRI HUYO ALIYEINGIA NI JASIRI NA ATAWEZA KUMUDU HAPO KAMA TARATIBU NI ZILE ZILE NA HANA MAMLAKA KUKIUKA. AKIKIUKA AKIJA CIG IMEKULA KWAKE. NI TARATIBU NGUMU SANA, SIO RAHISI HIVYO. HAPAHITAJI DAKTARI KWENYE HII POST, ANATAKIWA MTU ALIYEBOBEA KWENYE PROCUREMENT HIYO NDIO SHIDA YA MSD. LEO KILA MZIGO UNAPITIA GYPSA, SIJAELEEA JESHI LITAFANYA NINI HAPO...KWA KWELI SIJUI KABISA.
UMMY EMEMSINGIZIA BADO ANAIMUDU VIZURI WIZARA ACHENI WIVU
 
MSD INASUMBULIWA NA TARATIBU ZA KIMANUNUZI PAMOJA NA DENI WANALODAI HOSPITAL MBALI MBALI. WEWE MTOA MADA HUJUI KITU. USIFIKIRI HUYO ALIYEINGIA NI JASIRI NA ATAWEZA KUMUDU HAPO KAMA TARATIBU NI ZILE ZILE NA HANA MAMLAKA KUKIUKA. AKIKIUKA AKIJA CIG IMEKULA KWAKE. NI TARATIBU NGUMU SANA, SIO RAHISI HIVYO. HAPAHITAJI DAKTARI KWENYE HII POST, ANATAKIWA MTU ALIYEBOBEA KWENYE PROCUREMENT HIYO NDIO SHIDA YA MSD. LEO KILA MZIGO UNAPITIA GYPSA, SIJAELEEA JESHI LITAFANYA NINI HAPO...KWA KWELI SIJUI KABISA.
UMMY EMEMSINGIZIA BADO ANAIMUDU VIZURI WIZARA ACHENI WIVU
 
MSD INASUMBULIWA NA TARATIBU ZA KIMANUNUZI PAMOJA NA DENI WANALODAI HOSPITAL MBALI MBALI. WEWE MTOA MADA HUJUI KITU. USIFIKIRI HUYO ALIYEINGIA NI JASIRI NA ATAWEZA KUMUDU HAPO KAMA TARATIBU NI ZILE ZILE NA HANA MAMLAKA KUKIUKA. AKIKIUKA AKIJA CIG IMEKULA KWAKE. NI TARATIBU NGUMU SANA, SIO RAHISI HIVYO. HAPAHITAJI DAKTARI KWENYE HII POST, ANATAKIWA MTU ALIYEBOBEA KWENYE PROCUREMENT HIYO NDIO SHIDA YA MSD. LEO KILA MZIGO UNAPITIA GYPSA, SIJAELEEA JESHI LITAFANYA NINI HAPO...KWA KWELI SIJUI KABISA.
UMMY EMEMSINGIZIA BADO ANAIMUDU VIZURI WIZARA ACHENI WIVU

Taratibu za Manunuzi hazina shida. Ipo very clear kijana. Procurement Act imeweka clear manunuzi ya Catalogue Items kwa taasisi zote za Umma sio MSD tu. Procurement Act imeweka wazi Emergency Procurement .

Shida ni kwamba unataka kutumia njia za manunuzi kama za emergency kwa faida yenu. Huwezi kumuweka mtu MSD wa Procurenent kuwa DG ambaye hana Pharmaceutical Knowledge, ni useless kununua dawa sio sawa na kununua mbao. Hilo kosa lilifanywa na kina Sefue kwa kumlaghai Rais, na JPM amekuwa mvumilivu sana kwa 5 years. I am speechless with that patience.

Na kama MSD inachangamoto na Procurement Act na Miongozo ya Manunuzi ya TZ; Je, ilishawahi kuwasilisha changamoto hizo kwa Mkuu na kuomba njia mbadala wanayoamini kwamba wakiifuata wataweza kukidhi mahitaji ya Hospitali. ?

Au mnataka kukwepa miongozo mpate kupiga vizuri. ? Yani hapo ndio mnafuata miongozo hali ipo hivo; mkiwa excluded je ?

Je unajua MSD Inapoteza kiasi gani cha fedha kwa kushindwa kuwahudumia Hospitali kubwa kama BMC , MNH etc etc. ?

MSD ipo kisheria na hizi Hospitali zinatakiwa kisheria kwenda kununua dawa MSD hiyo ni lazima ; kama Dawa hakuna MSD , Hospitali hizi zinatakiwa kuomba ridhaa ya kununua dawa nje ya MSD. Nimefanya kazi Halmashauri najua taratibu zote huna cha kuniambia.

Hamjawahi kupata DG smart ambaye atakuwa na uwezo wa kutackle hizo changamoto.

Suala la GPSA limenza lini ?Mizigo ya MSD kuwa cleared na GPSA imekuja baada ya Doto kuona mnatumia gharama kubwa ku clear mizigo billions of money ambazo zinaweza kununua dawa nyingine; ndiyo hapo Doto James akaamuru GPSA ifanye hiyo kazi of which moja ya kazi ya GPSA kisheria ni Kufanya clearing and forwarding.

Msisingizie GPSA, kabla ya GPSA dawa mlikuwa nazo ; ? au hizo kashfa zenu za upotevu wa hela zimeanza baada ya kuwa na GPSA? Doto aliamua hivyo baada ya kumuonesha Rais gharama mnazotumia na Bwanakunu aliulizwa why this, alijibu nini; did he even give a *** ? He was totally incompetent !

Namoja ya sababu ya special auditing ni gharama za ugomboaji. Leo tukisema tunaomba analysis yenu kabla ya GPSA na baada ya GPSA; je utaweza kuonesha kuwa kabla ya GPSA mlifanya vyema? Kuwa na akili mkuu usikurupuke kama haupo well informed.

Yaani nyie tuwape mandate ya kununua dawa za nchi; hapo hapo mnataka mandate ya kufanya Clearing ? Seriously , GPSA Inakazi gani?

Taasisi za Umma hazifanyi kazi kwa mtindo huo mzee baba ! Ndio maana nasema Bwanakunu was not smart, alikuwa mpiga domo; angekuwa smart angeomba wafanyakazi wa MSD waliokuwa wanafanya clearing wahamishiwe GPSA kufanya kazi ya clearing mizigo ya MSD tu; I know dawa sio mbao hivo angeeleweka sana , did he do that,?

Fafanua Ummy anamudu vipi Wizara ya Afya ? Wewe utakuwa ni mfanyakazi wa MSD huko kwenye ugomboaji; so shut up you are not medical personnel you can’t understand this. It is beyond your brain.


Mk54
 
MSD INASUMBULIWA NA TARATIBU ZA KIMANUNUZI PAMOJA NA DENI WANALODAI HOSPITAL MBALI MBALI. WEWE MTOA MADA HUJUI KITU. USIFIKIRI HUYO ALIYEINGIA NI JASIRI NA ATAWEZA KUMUDU HAPO KAMA TARATIBU NI ZILE ZILE NA HANA MAMLAKA KUKIUKA. AKIKIUKA AKIJA CIG IMEKULA KWAKE. NI TARATIBU NGUMU SANA, SIO RAHISI HIVYO. HAPAHITAJI DAKTARI KWENYE HII POST, ANATAKIWA MTU ALIYEBOBEA KWENYE PROCUREMENT HIYO NDIO SHIDA YA MSD. LEO KILA MZIGO UNAPITIA GYPSA, SIJAELEEA JESHI LITAFANYA NINI HAPO...KWA KWELI SIJUI KABISA.
UMMY EMEMSINGIZIA BADO ANAIMUDU VIZURI WIZARA ACHENI WIVU

Halafu ujifunze kuandika au uende kwenye Forum za Udaku. Hapa sio udaku ni Maslahi ya Taifa wananchi wasiokuwa na Bima hasa wale bibi zako waliokuwa kijijini angalau akipata ajali apate panadol na Drip kwa bure kabisa. Inawezekana huelewi impact ya hii thread.

Unaniandikia maandishi makubwa nimekuambia ninatatizo la Macho. Afisa mzima hujui hata kuandika. Ndiyo haya wanasema mnaajiriwa kwa connection bila sifa.


Mk54
 
Uwe na dharau uwe na elimu. Mwenzie anaitwa Brig. Dr. General......
Yeye anaitwa Bw. Laurean ha ha ha halafu unakuwa na dharau. Kwanza huyo ni muhaya au Mnyarwanda


Mk54
Yaani umepotea mno. Uzi za watu wenye majungu hutaja kabila, dini ya mtu na hata mahusiano. Kuna wakati you have to man up. Hivi kukataa deni wakati lipo sio kupindisha ukweli? Hivi kukiri kwamba Sheria ya manunuzi kupitia taratibu zake ndefu imetengeneza ukiritimba, unapungukiwa nini? Using'ang'ane na chaka la halmashauri. Hata km una chuki zako ni vyema utende haki.
 
Tume maalum iliyoundwa na PS- Hazina imegundua kuwa kuna upungufu wa mtaji wa Tsh 30 Bilion uliosababishwa na MSD kufanya under pricing. Ni Ummy Mwalimu na Bwanakunu waliomdanganya Rais kuwa kununua dawa kwa Distributors kama Salama Pharmaceuticals kunasababisha dawa zinunuliwe kwa bei ya juu kwa vile Distributors wanaweka margin (cha juu).

Kwa hiyo hata kwenye hotuba zake akiongelea mafanikio ya Wizara ya Afya Rais alikuwa anatamka wazi wazi kuwa sasa MSD inanunua dawa VIWANDANI kwa hiyo bei zimeshuka.

Ukweli ni kwamba Distributors hao hao akina Salama Pharmaceuticals, Biocare, Pyramid walibadili anuani badala ya kutumia letter head zao na anuani za Tanzania, wakatumia majina ya manufactures wao wanao wawakilisha. Na MSD kwenye kupanga bei wakateremsha kwa makusudi bei za dawa ili kudhihirisha kwa wananchi kuwa DAWA ZIMETEREMKA BEI. Sasa imekula mtaji kwa Tsh 30 Bilioni.

Je Hizo ni akili au matope?

Kwa nini Ummy Mwalimu bado yuko ofsini kama waziri?
Kwa hiyo hoja hapa ni kwanini huyo DG na Ummy waliwauzia wananchi dawa bei rahisi badala ya ghali?
 
Sasa kama hamjapelekewa pesa mnafanya nini hapo Keko Mwanga Madawa? Fungeni ofisi. Serikali imekuwa ikitoa pesa mara zote; mnapozipeleka mnajua nyie.

Kwanza MSD ni taasisi yenye umri zaidi ya Miaka 20 Na mnauza Dawa bado mnataka serikali iwape pesa kila siku.?

Shida hamjiongezi. Halafu mpunguze politics. Fanyeni kazi. Serikali haidaiwi na MSD na Ngosha alisema amewapa Bil 300 kwa ajili ya dawa; mmepeleka wapi hizo pesa?


Mk54
Serikali inaipa pesa MSD??
 
Toka mwaka wa fedha 2019/2020 uanze na sasa unaelekea mwishoni,kuna fedha za rudhuku za serikali zilizokwisha kwenda msd vya vituo mbali mbali vya serikali vya kutolea huduma ya afya iliyokwisha kutumwa msd?.
Kama ni ndiyo,msd walikwama
Kama siyo,msd hawezi kumudu kusupply commodities wakati hela za vituo vya got haviwekewi pesa,

Jiwe bana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa utambuzi wangu mimi na ufahamu wangu yupo pale kwa sababu maalumu
Then wa Tz wengin wanaon kam mh.Raisi anafany maamuz kwa haraka No.
No mh. Huw anafany vtu(kwasababu za mcng) na kwa faidi na kwa maslai ya Taifa sio kwa faid ya mtu
NB:-mbele tutaelewa hapo pana jambo.
Ni kweli MSD au GPSA sio taasisi rahisi kabisa, ni ngumu na zina temptation nyingi sana na ni rahisi sana kutumika na wanasiasa wa juu. Ikiwemo na Waziri mwenyewe.

Ndio maana wengi wanashauri, kama Bwanakunu ameondolewa, basi kuna haja ya Ummy mwalimu nae kuchunguzwa. Hawa watu walifanya kazi kwa karibu sana: na moja ya findings katika Special auditing iliyofanyika MSD ni uhusiano wao kati ya Bahari Pharmacy, Ummy na Bwanakunu.

Sina shaka na taasisi ya Usalama juu ya kumpatia Rais taarifa sahihi. Ukisoma pia taarifa ya CAG, Assad ya mwaka 2018/19 utaona ameelezea vyema kuwa kuna upotevu wa pesa zaidi ya Bilion 30 ambazo hazijulikani zilipo na wala hazina nyaraka.

JPM ni Rais mwenye akili sana; atakuja kueleweka baada ya kuondoka madarakani. Mambo haya enzi ya JK yalikuwa yanamalizwa kishikaji unless kama umegusa maslaha yake ndio atakuondoa.

Mradi wa Delivery Pack alizokuwa anazitangaza Bwanakunu, ni mradi wa mtu binafsi kwa kushirikiana na Bahari Pharmacy na asilimia 90 ya vituo vya Afya walikuwa hawataki kabisa kununua huo upuuzi lakini ilikuwa ni lazima upewe na utozwe pesa kupitia akaunti yako kwa barua ya Ummy mwalimu.

Aidha, Ummy Mwalim na Bwanakunu na katibu Afya Dr. Zainabu wamefeli sana katika suala la COVID 19. Wao ndio sababu ya Watz kupigwa kwenye Sanitizer na Barakoa.

fikiria; kitu kama Sanitizer MSD imeshindwa kukidhi mahitaji ya wananchi: Nilishangaa sana Bwanakunu alipotangaza kuwa anatoa Sanitizer lita 350, 000 kutoka nje ya nchi.

Unaagiza lita 350,000 kati ya watu milioni 60 na Waziri wa Afya yupo amekaa kimya ! Katibu wa Afya yupo na amekaa kimya, Naibu waziri yupo na amekaa kimya, halafu tunamuona JPM mbaya. Hii safu yote ilipaswa kuondolewa.

Unaagiza Sanitizer nje ya nchi wakati tuna local manufacturers nyingi sana na hata hao MSD wenyewe wangekuwa wamejipanga kwa kushirikiana na Wizara ya Afya wangeweza kutengeneza Sanitizer. Zaidi ya lita Mil 5. Wameajiri Famasia, wanakazi gani

Ummy yupo busy sana; je kuna mtu anajua yupo busy na kazi gani? Mimi sijui.

Nimeridhika na uteuzi wa JPM juu ya Gabriel, kwanza ni Doctor( japo ilitakiwa awe Pharmacist lakini tofauti ni ndogo sana).

Nina elewa kwa undani nidhamu ya wanajeshi, tazama hiyo picha utaelewa ninachomaanisha.

View attachment 1440740

pamoja na hilo Brigedia atambue kwamba haitokuwa rahisi kuongoza taasisi kama MSD, haitokuwa rahisi hata kidogo, MSD ni taasisi yenye malalamiko na utendaji mmbovu kuwahi kutokea. Tangu na Tangu na kabla hata ya Bwanakunu.
View attachment 1440741

Kwa uzoefu wangu wa Global Health Supply Chain, nina mshauri yafuatayo ndugu Brig. General Dr Gabriel Mhidize;

1. Apendekeze kupanguliwa safu ya wakurugenzi, hasa Kurugenzi ya Ugavi, Kurugenzi ya Manunuzi na Kurugenzi ya Rasilimali watu. Akiendelea kufanya kazi na wakurugenzi hao, atatumbuliwa mapema kabisa

2. Akae na wakongwe wa MSD secretly wamsaidie kujua wale wote wanaohusika na dili fake; akishawajua awafanyie auditing pamoja na kuwahamisha au kuwasimamisha kazi.

3. Managers wa kanda, hawa ndio tatizo kubwa; Na hawa hawa ndio ninavyodhani wamemuangusha Bwanakunu,
View attachment 1440743
wachunguzwe Wote ikiwezekana tafuta watu utakaoweza kufanya nao kazi

4. Pata muda wa miezi 6 kusoma supply chain ya MSD, hili ni muhimu sana ili wasije kukuambukiza udokozi

5. Usiwe mtu wa kukaa ofisini tu, Tembelea ghala zote mara kwa mara na uwasikilize kwa makini watendaji wa warehouses, hao ndio wanamajibu sahihi ya MSD.

6. Malalamiko ya watu kuajiriwa kwa kujuana na kwa connections bila kufuata utaratibu wa utumishi usiyapuuze. Ni suala lipo na limelalamikiwa na wadau, rejea uzi hapo chini.

7. Kuwa karibu na Hospitali zote kubwa nchini Tanzania, jua mahitaji yao ya msingi. Kuna pesa nyingi sana zinapotea kwa hizi Hospitali kununua dawa nje ya MSD simply MSD haina uwezo wa kukidhi mahitaji yao.

8. kuwa makini sana na documents. Huenda waliomtoa Bwanakunu ni watu wa Bwanakunu.
View attachment 1440745

9. Weka macho sana warehouse , Finance na Manunuzi. Hiyo ndio MSD .

Ninaamini Utaweza na sina shaka juu ya Uteuzi wa JPM.

Nidhamu yenu huonekana hadi kwenye picha.
View attachment 1440746

Nitumainie kuona mabadiliko ya namna hii yafanyike na GPSA.
View attachment 1440740
Chanzo cha picha- MSD social media, nipashe online.

>>>>>>Nyuzi nyingine hapo chini zenye malalamiko ya muda mrefu kuhusu MSD na uteuzi wa Bwanakunu mwaka 2015 uliopenyezwa na kina Sefue bila ya kuangalia medical knowledge na Pharmaceutical Management skills za huyu bwana. MSD imepata jina sana kipindi cha uongozi wake; lakini ni kipindi ambacho kimekuwa na Great Depression kwenye upatikanaji wa dawa muhimu kuwahi kutokea huku Rais akiwapa dau la Bil 280.

1. Rais Magufuli amteua Brigedia Jenerali Gabriel Sauli Mhidize kuwa Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD)
Rais Magufuli amteua Brigedia Jenerali Gabriel Sauli Mhidize kuwa Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) - JamiiForums

2. Laurean Rugambwa - Mkurugenzi Mkuu wa MSD Mteule wa Rais
Laurean Rugambwa - Mkurugenzi Mkuu wa MSD Mteule wa Rais - JamiiForums


Tarehe 5, Mei 2020.



Mk54

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom