Je, MSD na Brig. Gabriel Mhidize, Itawezekana?

Mk54

JF-Expert Member
Dec 29, 2016
1,997
3,933
Ni kweli MSD au GPSA sio taasisi rahisi kabisa, ni ngumu na zina temptation nyingi sana na ni rahisi sana kutumika na wanasiasa wa juu. Ikiwemo na Waziri mwenyewe.

Baada ya katibu mkuu hazina kumng’ata sikio JPM juu ya matumizi mabaya ya fedha za umma katika Bohari kuu ya dawa huku taasisi ikiendeshwa kingono na kuajiri kikanda na kujuana; JPM aka NGUVU , aliamua kufanya special auditing pale BOHARI: na moja ya findings katika Special auditing iliyofanyika MSD ni uhusiano kati ya Bahari Pharmacy, Ummy na Bwanakunu pamoja na wizi wa manunuzi ya dawa unaoitia Taifa hasara ya Billions huku vituo vya afya vikikosa Hata panadol.

Sina shaka na taasisi ya Usalama juu ya kumpatia Rais taarifa sahihi. Ukisoma pia taarifa ya CAG, Assad ya mwaka 2018/19 utaona ameelezea vyema kuwa kuna upotevu wa pesa zaidi ya Bilion 30 ambazo hazijulikani zilipo na wala hazina nyaraka.

JPM ni Rais mwenye akili sana; atakuja kueleweka baada ya kuondoka madarakani. Mambo haya enzi ya JK yalikuwa yanamalizwa kishikaji unless kama umegusa maslaha yake ndio ataondoka

Nimeridhika na uteuzi wa JPM juu ya Gabriel, kwanza ni Doctor( japo ilitakiwa awe Pharmacist lakini tofauti ni ndogo sana).

Nina elewa kwa undani nidhamu ya wanajeshi, tazama hiyo picha utaelewa ninachomaanisha.

IMG_1959.JPG


pamoja na hilo Brigedia atambue kwamba haitokuwa rahisi kuongoza taasisi kama MSD, haitokuwa rahisi hata kidogo, MSD ni taasisi yenye malalamiko na utendaji mmbovu kuwahi kutokea. Tangu na Tangu na kabla hata ya Bwanakunu.
IMG_1955.JPG


Kwa uzoefu wangu wa Global Health Supply Chain, nina mshauri yafuatayo ndugu Brig. General Dr Gabriel Mhidize;

1. Apendekeze kupanguliwa safu ya wakurugenzi, hasa Kurugenzi ya Ugavi, Kurugenzi ya Manunuzi na Kurugenzi ya Rasilimali watu ambayo ndio inaongoza kuajiri mabogus kwa minajili ya kujuana na kikanda. Afaham kuwa Akiendelea kufanya kazi na wakurugenzi hao, atatumbuliwa mapema kabisa kwa Sababu watamuangusha. Kwanza kwa nini mtu akae ofisini miaka 10 ? Mtu kama huyo hawezi kuwa na mawazo mapya zaidi ya uzoefu, ondoa hizo takataka zote.

2. Akae na wakongwe wa MSD secretly wamsaidie kujua wale wote wanaohusika na dili fake; akishawajua awafanyie auditing pamoja na kuwahamisha au kuwasimamisha kazi.

3. Managers wa kanda, hawa ndio tatizo kubwa; Na hawa hawa ndio ninavyodhani wamemuangusha Bwanakunu,
IMG_1957.JPG

wachunguzwe Wote ikiwezekana tafuta watu utakaoweza kufanya nao kazi changanya na wajeshi humo humo

4. Pata muda wa miezi 6 kusoma supply chain ya MSD, hili ni muhimu sana ili wasije kukuambukiza UDOKOZI NA DILI FAKE, NA UKANDA.

5. Usiwe mtu wa kukaa ofisini tu, Tembelea ghala zote mara kwa mara na uwasikilize kwa makini watendaji wa warehouses, hao ndio wanamajibu sahihi ya MSD.

6. Malalamiko ya watu kuajiriwa kwa kujuana na kwa connections bila kufuata utaratibu wa utumishi usiyapuuze. Ni suala lipo na limelalamikiwa na wadau, na ndio chanzo cha utendaji mmbovu MSD, rejea uzi hapo chini.

7. Kuwa karibu na Hospitali zote kubwa nchini Tanzania, jua mahitaji yao ya msingi. Kuna pesa nyingi sana zinapotea kwa hizi Hospitali kununua dawa nje ya MSD simply MSD haina uwezo wa kukidhi mahitaji yao.

8. kuwa makini sana na documents. Huenda waliomtoa Bwanakunu ni watu wa Bwanakunu.
IMG_1938.JPG


9. Weka macho sana warehouse , Finance na Manunuzi. Hiyo ndio MSD .

Ninaamini Utaweza na sina shaka juu ya Uteuzi wa JPM. Hapa Kazi Tu , JPM ndio Rais wangu na anawakilisha mioyo ya watanzania wengi , JPM aka NGUVU

Nidhamu yenu huonekana hadi kwenye picha.
28843aeb-f678-43d7-af08-d5457ee7b1db.jpg


Nitumainie kuona mabadiliko ya namna hii yafanyike na GPSA.
IMG_1959.JPG

Chanzo cha picha- MSD social media, nipashe online.

>>>>>Nyuzi nyingine hapo chini zenye malalamiko ya muda mrefu kuhusu MSD na uteuzi wa Bwanakunu mwaka 2015 uliopenyezwa na kina Sefue bila ya kuangalia medical knowledge na Pharmaceutical Management skills za huyu bwana. MSD imepata jina sana kipindi cha uongozi wake; lakini ni kipindi ambacho kimekuwa na Great Depression kwenye upatikanaji wa dawa muhimu kuwahi kutokea huku Rais akiwapa dau la Bil 280.

1. Rais Magufuli amteua Brigedia Jenerali Gabriel Sauli Mhidize kuwa Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD)
Rais Magufuli amteua Brigedia Jenerali Gabriel Sauli Mhidize kuwa Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) - JamiiForums

2. Laurean Rugambwa - Mkurugenzi Mkuu wa MSD Mteule wa Rais
Laurean Rugambwa - Mkurugenzi Mkuu wa MSD Mteule wa Rais - JamiiForums


Tarehe 5, Mei 2020.



Mk54
 
Umeficha Id, bado unaumauma maneno why?

Bwanakunu na Umy wapo vipi kimahusiano pamoja na mengine yenye kuchefua ofisi za umma, mwaga mtama hadharani kila njiwa aokoteze.

Na hii tumbuambua imekuwa ni tumbua ya kuuma na kupuliza, maana haing'oi shina, ama ikiling'oa kumbe ni kwa ajili ya kujaza mbolea kwenye shimo kwa ajili ya ustawi na kisha kulirejesha shina hilohilo!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeficha Id, bado unaumauma maneno why?

Bwanakunu na Umy wapo vipi kimahusiano pamoja na mengine yenye kuchefua ofisi za umma, mwaga mtama hadharani kila njiwa aokoteze.

Na hii tumbuambua imekuwa ni tumbua ya kuuma na kupuliza, maana haing'oi shina, ama ikiling'oa kumbe ni kwa ajili ya kujaza mbolea kwenye shimo kwa ajili ya ustawi na kisha kulirejesha shina hilohilo!

Sent using Jamii Forums mobile app

Ukweli ndio huo kaka. I wish Aje staff wa MSD humu atupe kile kinachosemwa ndani ya taasisi.




Mk54
 
Sio Rahisi. Anatakiwa kuwa very careful. Mimi nashauri ile Bodi ya wakurugenzi ivunjwe halafu aangalie watu ambao atafanya nao kazi.


Mk54
Hata umpeleke mtume pale, kama serikali hailipi madeni yake ni bure tu!! Wewe unachukua vifaa/madawa karibia ya bilioni 250,hutaki kulipa taasisi itajiendesha vipi? Mwisho wa siku unatafuta mtu wa kumtoa kafara!! Ndio maana licha ya panga pangua ya kila siku bado hakuna ufanisi wowote, sehemu nyingi!!
 
Mmm huyu kapelekwa ili kwanza Mkulu anataka control infomation kwa kuwa kwa kuweka mtu ambaye sio mtu wake hawezi kuendana na matakwa yake,naota tu .Ila kingine kwa historia ya Bwana Kunu aliyeondoka ,yeye amefanya kazi sana na mabeberu na mkuu hataki mtu ambaye ameshafanya kazi na mabeberu .Naota pia.So sasa atafanya kazi anachotaka aisee.Mfano si unaona Bunge chini ya Ndungai yaani anamuistract asiwape wabunge wasiohudhuria posho wakati bunge ina taratibu zake na kiongozi yake na sio Amri kutoka juu.Nawaza sana jinsi maisha ya watu yanavyoendeshwa na mtu mmoja bila sheria saa nyingine kufuatwa
 
Mmm huyu kapelekwa ili kwanza Mkulu anataka control infomation kwa kuwa kwa kuweka mtu ambaye sio mtu wake hawezi kuendana na matakwa yake,naota tu .Ila kingine kwa historia ya Bwana Kunu aliyeondoka ,yeye amefanya kazi sana na mabeberu na mkuu hataki mtu ambaye ameshafanya kazi na mabeberu .Naota pia.So sasa atafanya kazi anachotaka aisee.Mfano si unaona Bunge chini ya Ndungai yaani anamuistract asiwape wabunge wasiohudhuria posho wakati bunge ina taratibu zake na kiongozi yake na sio Amri kutoka juu.Nawaza sana jinsi maisha ya watu yanavyoendeshwa na mtu mmoja bila sheria saa nyingine kufuatwa
bado haujajua nchi kwa sasa inaendeshwa kijeshi......
 
Mkuu Mk54 ulistahili upewe meeting ana kwa ana na Brigedia . Umetoa ushauri mzuri sana kupita maelezo.

Katika hoja yako nimependa pale uliposema " Ummy anaonekana yuko busy" Lakini haijulikani yuko busy na nini? Swali hili huwa watu wengi wanajiuliza hasa tukiona kwa Cs Mugai kagwe wa Kenya alivyo busy na juzi wakenya wamefanya Auditing ya pesa ya corona kutoka World Bank wanamtaka akae pembeni pamoja na u busy wote.

Ikimpendeza aseme yuko busy na nini zaidi japo tunajua wizara ya afya ni kubwa sana na ina miradi mingi ambayo iko very tempting penye pesa tamaa huingia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom