Je, MSD na Brig. Gabriel Mhidize, Itawezekana?

Je, MSD na Brig. Gabriel Mhidize, Itawezekana?

Je ameiweza ?
**** mazuri na madhaifu pia....ila msd ngumu, naona pale hawaheshimu proffesionals na uwezo wa watu, zaidi kuna network za kundi fulani ndio hao hao mawazo yao kusikilizwa na kupandishwa vyeo. idara ya rasimali mmepeleka mkurugenzi pale hamna kitu kabisa, meneja wake dada mmoja hata sijui kama anasaidiaga ile taasisi mawazo mgando sana. wanachofanya ni kufatilia vibali vya kuajiri utumishi kila kukicha, watumieni mlio nao to maximum na motivate them.
 
**** mazuri na madhaifu pia....ila msd ngumu, naona pale hawaheshimu proffesionals na uwezo wa watu, zaidi kuna network za kundi fulani ndio hao hao mawazo yao kusikilizwa na kupandishwa vyeo. idara ya rasimali mmepeleka mkurugenzi pale hamna kitu kabisa, meneja wake dada mmoja hata sijui kama anasaidiaga ile taasisi mawazo mgando sana. wanachofanya ni kufatilia vibali vya kuajiri utumishi kila kukicha, watumieni mlio nao to maximum na motivate them.

Kama hadi Mjeshi amefeli basi shida ipo pale . Kama kuna Mkurugenzi alishawahi kuweza basi iangaliwe aliwezaje

Huyu Mjeshi kwa maneno ya mama ni hakuna kitu
 
Kama hadi Mjeshi amefeli basi shida ipo pale . Kama kuna Mkurugenzi alishawahi kuweza basi iangaliwe aliwezaje

Huyu Mjeshi kwa maneno ya mama ni hakuna kitu
minor reform needed, somebody cosmas aliweza somehow ila aonywe kuhusu ufisadi kama mchechu nhc
 
Kama hadi Mjeshi amefeli basi shida ipo pale . Kama kuna Mkurugenzi alishawahi kuweza basi iangaliwe aliwezaje

Huyu Mjeshi kwa maneno ya mama ni hakuna kitu
Mama Amemkataa Kabisa
 
Ni kweli MSD au GPSA sio taasisi rahisi kabisa, ni ngumu na zina temptation nyingi sana na ni rahisi sana kutumika na wanasiasa wa juu. Ikiwemo na Waziri mwenyewe.

Baada ya katibu mkuu hazina kumng’ata sikio JPM juu ya matumizi mabaya ya fedha za umma katika Bohari kuu ya dawa huku taasisi ikiendeshwa kingono na kuajiri kikanda na kujuana; JPM aka NGUVU , aliamua kufanya special auditing pale BOHARI: na moja ya findings katika Special auditing iliyofanyika MSD ni uhusiano kati ya Bahari Pharmacy, Ummy na Bwanakunu pamoja na wizi wa manunuzi ya dawa unaoitia Taifa hasara ya Billions huku vituo vya afya vikikosa Hata panadol.

Sina shaka na taasisi ya Usalama juu ya kumpatia Rais taarifa sahihi. Ukisoma pia taarifa ya CAG, Assad ya mwaka 2018/19 utaona ameelezea vyema kuwa kuna upotevu wa pesa zaidi ya Bilion 30 ambazo hazijulikani zilipo na wala hazina nyaraka.

JPM ni Rais mwenye akili sana; atakuja kueleweka baada ya kuondoka madarakani. Mambo haya enzi ya JK yalikuwa yanamalizwa kishikaji unless kama umegusa maslaha yake ndio ataondoka

Nimeridhika na uteuzi wa JPM juu ya Gabriel, kwanza ni Doctor( japo ilitakiwa awe Pharmacist lakini tofauti ni ndogo sana).

Nina elewa kwa undani nidhamu ya wanajeshi, tazama hiyo picha utaelewa ninachomaanisha.

View attachment 1440740

pamoja na hilo Brigedia atambue kwamba haitokuwa rahisi kuongoza taasisi kama MSD, haitokuwa rahisi hata kidogo, MSD ni taasisi yenye malalamiko na utendaji mmbovu kuwahi kutokea. Tangu na Tangu na kabla hata ya Bwanakunu.
View attachment 1440741

Kwa uzoefu wangu wa Global Health Supply Chain, nina mshauri yafuatayo ndugu Brig. General Dr Gabriel Mhidize;

1. Apendekeze kupanguliwa safu ya wakurugenzi, hasa Kurugenzi ya Ugavi, Kurugenzi ya Manunuzi na Kurugenzi ya Rasilimali watu ambayo ndio inaongoza kuajiri mabogus kwa minajili ya kujuana na kikanda. Afaham kuwa Akiendelea kufanya kazi na wakurugenzi hao, atatumbuliwa mapema kabisa kwa Sababu watamuangusha. Kwanza kwa nini mtu akae ofisini miaka 10 ? Mtu kama huyo hawezi kuwa na mawazo mapya zaidi ya uzoefu, ondoa hizo takataka zote.

2. Akae na wakongwe wa MSD secretly wamsaidie kujua wale wote wanaohusika na dili fake; akishawajua awafanyie auditing pamoja na kuwahamisha au kuwasimamisha kazi.

3. Managers wa kanda, hawa ndio tatizo kubwa; Na hawa hawa ndio ninavyodhani wamemuangusha Bwanakunu,
View attachment 1440743
wachunguzwe Wote ikiwezekana tafuta watu utakaoweza kufanya nao kazi changanya na wajeshi humo humo

4. Pata muda wa miezi 6 kusoma supply chain ya MSD, hili ni muhimu sana ili wasije kukuambukiza UDOKOZI NA DILI FAKE, NA UKANDA.

5. Usiwe mtu wa kukaa ofisini tu, Tembelea ghala zote mara kwa mara na uwasikilize kwa makini watendaji wa warehouses, hao ndio wanamajibu sahihi ya MSD.

6. Malalamiko ya watu kuajiriwa kwa kujuana na kwa connections bila kufuata utaratibu wa utumishi usiyapuuze. Ni suala lipo na limelalamikiwa na wadau, na ndio chanzo cha utendaji mmbovu MSD, rejea uzi hapo chini.

7. Kuwa karibu na Hospitali zote kubwa nchini Tanzania, jua mahitaji yao ya msingi. Kuna pesa nyingi sana zinapotea kwa hizi Hospitali kununua dawa nje ya MSD simply MSD haina uwezo wa kukidhi mahitaji yao.

8. kuwa makini sana na documents. Huenda waliomtoa Bwanakunu ni watu wa Bwanakunu.
View attachment 1440745

9. Weka macho sana warehouse , Finance na Manunuzi. Hiyo ndio MSD .

Ninaamini Utaweza na sina shaka juu ya Uteuzi wa JPM. Hapa Kazi Tu , JPM ndio Rais wangu na anawakilisha mioyo ya watanzania wengi , JPM aka NGUVU

Nidhamu yenu huonekana hadi kwenye picha.
View attachment 1440746

Nitumainie kuona mabadiliko ya namna hii yafanyike na GPSA.
View attachment 1440740
Chanzo cha picha- MSD social media, nipashe online.



1. Rais Magufuli amteua Brigedia Jenerali Gabriel Sauli Mhidize kuwa Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD)
Rais Magufuli amteua Brigedia Jenerali Gabriel Sauli Mhidize kuwa Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) - JamiiForums

2. Laurean Rugambwa - Mkurugenzi Mkuu wa MSD Mteule wa Rais
Laurean Rugambwa - Mkurugenzi Mkuu wa MSD Mteule wa Rais - JamiiForums


Tarehe 5, Mei 2020.



Mk54

Bado umeridhika na uteuzi wa Brigedia Gabriel mhidize ? au zilikuwa ni mbwembwe za mwenda zake

Nadhani serikali ianze kuangalia namna bora ya kupata Wakurugenzi kuliko kuteua. Huyu mjeshi aliteuliwa vigezo gani , maana kwa jinsi rais alivyoeleza, ni kama vile ameenda kuiua msd
 
Back
Top Bottom