Ni kweli MSD au GPSA sio taasisi rahisi kabisa, ni ngumu na zina temptation nyingi sana na ni rahisi sana kutumika na wanasiasa wa juu. Ikiwemo na Waziri mwenyewe.
Ndio maana wengi wanashauri, kama Bwanakunu ameondolewa, basi kuna haja ya Ummy mwalimu nae kuchunguzwa maana kuna mengi yanasemwa chinichini juu ya wawili hawa. Isipuuzwe hata kidogo.
Mradi wa Delivery Pack alizokuwa anazitangaza Bwanakunu, ni mradi wa mtu binafsi kwa kushirikiana na Bahari Pharmacy na asilimia 90 ya vituo vya Afya walikuwa hawataki kabisa lakini ilikuwa ni lazima upewe na utozwe pesa kupitia akaunti yako kwa barua ya Ummy mwalimu.
Aidha, Ummy Mwalim na Bwanakunu na katibu Afya Dr. Zainabu wamefeli sana katika suala zima laCOVID 19. Wao ndio sababu ya Watz kupigwa kwenye Sanitizer na Barakoa.
Ummy anaonekana yupo busy lakini hajulikan yupo busy na nini!! Kazi ya kuwachunguza maabara amepewa Mwigulu, badala yake yeye Ummy kwa kujihami ndio kaenda kuunda tume . Hii yote ni ishara kwamba huyu mtu sio sahihi kwenye wizara kubwa kama hiyo. Anazunguka. So sad.
Nimeridhika na uteuzi wa JPM juu ya Gabriel, kwanza ni Doctor( japo ilitakiwa awe Pharmacist lakini tofauti ni ndogo sana).
Nina elewa kwa undani nidhamu ya wanajeshi, tazama hiyo picha utaelewa ninachomaanisha.
View attachment 1440740
pamoja na hilo Brigedia atambue kwamba haitokuwa rahisi kuongoza taasisi kama MSD, haitokuwa rahisi hata kidogo, MSD ni taasisi yenye malalamiko na utendaji mmbovu kuwahi kutokea. Tangu na Tangu na kabla hata ya Bwanakunu.
View attachment 1440741
Kwa uzoefu wangu wa Global Health Supply Chain, nina mshauri yafuatayo ndugu Brig. General Dr Gabriel Mhidize;
1. Apendekeze kupanguliwa safu ya wakurugenzi, hasa Kurugenzi ya Ugavi, Kurugenzi ya Manunuzi na Kurugenzi ya Rasilimali watu. Akiendelea kufanya kazi na wakurugenzi hao, atatumbuliwa mapema kabisa
2. Akae na wakongwe wa MSD secretly wamsaidie kujua wale wote wanaohusika na dili fake; akishawajua awafanyie auditing pamoja na kuwahamisha au kuwasimamisha kazi.
3. Managers wa kanda, hawa ndio tatizo kubwa; Na hawa hawa ndio ninavyodhani wamemuangusha Bwanakunu,
View attachment 1440743
wachunguzwe Wote ikiwezekana tafuta watu utakaoweza kufanya nao kazi
4. Pata muda wa miezi 6 kusoma supply chain ya MSD, hili ni muhimu sana ili wasije kukuambukiza udokozi
5. Usiwe mtu wa kukaa ofisini tu, Tembelea ghala zote mara kwa mara na uwasikilize kwa makini watendaji wa warehouses, hao ndio wanamajibu sahihi ya MSD.
6. Malalamiko ya watu kuajiriwa kwa kujuana na kwa connections bila kufuata utaratibu wa utumishi usiyapuuze
7. Kuwa karibu na Hospitali zote kubwa nchini Tanzania
8. kuwa makini sana na documents. Huenda waliomtoa Bwanakunu ni watu wa Bwanakunu.
View attachment 1440745
9. Weka macho sana warehouse , Finance na Manunuzi. Hiyo ndio MSD .
Hapana mapenzi kazini. Ni wazi Bwanakunu alifelishwa pia katika hili
Ninaamini Utaweza na sina shaka juu ya Uteuzi wako.
Nidhamu yenu huonekana hadi kwenye picha.
View attachment 1440746
Nitumainie kuona mabadiliko ya namna hii yafanyike na GPSA.
View attachment 1440740
Chanzo cha picha- MSD social media, nipashe online.
Tarehe 5, Mei 2020.
Mk54