Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,194
- 10,929
Katika maadhimisho ya siku mia za vita kati ya Israel na Hamas waziri mkuu wa Israel ameiamrisha Misri ifunge mpaka wake na Gaza na kuiachia Israel kudhibiti eneo lote linalounganisha Gaza na nchi hiyo ya kiarabu.
Kipande hicho cha ardhi ambacho Israel kinakiita Philadelphi Corridor kina urefu wa kilomita 14 sawa na wastani wa maili 8.6 na ndipo mpaka wa Rafah ulipo.
Wakati akihojiwa na vyombo vya habari Netanyahu alisema tunaweza tukawashinda Hamas na kuwanyang''anya silaha lakini baadae zitaingia tena.
Akiendelea na ufafanuzi wa ubabe wake huo, Netanyahu alisema maafisa wameonyesha namna kadhaa ya kufanikisha udhibiti wa kipande hicho na japo njia rasmi haijaamuliwa.
Kilichoamuliwa ni kwamba lazima eneo hilo linalounganisha Misri na Gaza lifungwe.