"...cult...". Hili umelitowa wapi wewe!
Tatizo lako toka mwanzo mkuu 'Fundi', huna kumbukumbu yoyote unapoandika humu na kupanga makundi kichwani mwako.
Itakuchukua muda mfupi sana ukijaribu kutazama tu kilicho andikwa huko nyuma, humu humu JF; na kujiridhisha mwenyewe juu ya misimamo ya baadhi ya watu humu.
Hata siwezi kueleza ni 'likes' ngapi tulizogawana kati yetu wewe na mimi miaka miwili mitatu tu iliyopita. Leo hii tayari unatuweka kwenye "cult..."?
Wewe ulikuwa kwenye 'cult' wakati huo; na bado unaendelea na hiyo ya kwenu?
Sasa ni hivi, mkuu, nimalizane na wewe juu ya hili la kurusha rusha tu tope hovyo:
Ukitaka kujuwa "cult" inayo nihusu mimi, hiyo moja tu, inayohusu maslahi ya nchi yetu Tanzania na wananchi wake, basi. Hakuna "cult" nyingine yoyote zaidi ya hapo.
Nenda kamwambie Samia na genge lake lote. Akibadilika leo na kuwapa waTanzania haki ya kuwachagua viongozi wanaowataka wenyewe; na achaguliwe yeye na akaacha ushetani mwingine aliozoea, njoo hapa uniite kuwa ni mfuasi wa "cult" anayoiendesha Samia!
Sasa kama bado hunielewi maelezo yangu haya, sijui nijieleze vipi tena uweze kuelewa.