I do not believe that, at all.Inawezekana Mbowe awe alikuwa na mpango tangu awali wa kujenga CHADEMA tishio kisha kuitumia kama bargaining chip na watawala wa CCM ili apate mafao mazito? Naona wasiompenda Mbowe wanaona alikuwa msaliti toka mwanzo! (I do not believe this)
Mbowe alipitia katika hali ngumu sana, hasa wakati wa Magufuli, sote tunajuwa; na hakutetereka wakati wote ule.
Sasa ukitaka kusikia 'hypothesis' ninayocheza nayo kichwani kuhusu kutetereka kwa Mbowe wakati wa Samia, nitakupa dokezo fupi tu hapa.
CHADEMA ilikuwa inaenda vizuri sana wakati wa Kikwete, Mbowe na Slaa. Na kwa kweli sifa anazopata Mbowe katika kuiimarisha CHADEMA, tuseme ni kuanzia wakati wa Mkapa, kuelekea Kikwete, na huwezi kumwondoa Slaa katika mchango wa wakati huo. Wananchi walikuwa na msisimko; kila mahali CHADEMA wakifanya mikutano. Ni nyakati hizo hizo, chama kilipata wabunge wengi, licha ya faulo za CCM nyakati za chaguzi; kwa sababu wanachama wao walikuwa 'assertive', hawakutaka chama kifanyiwe uonevu. Mahali mbalimbali waliweza kulinda kura zao na wakapata wabunge.
Fast forward; akaja Magufuli wa mabavu ya kutisha. Wananchi wakatishika. Slaa kakengeuka; Lowasa, ujio wake ndani ya chama ukachanganya wengi. Ni wakati huu Mbowe alipokuwa akinyanyaswa kila mahali, na hata viongozi wengine wa chama, uitikio wa wanachama/wapenzi wa chama; na tuseme waTanzania kwa ujumla wetu ukawa 'indifferent'. Watu wakawa kama hawajali kinachotokea kwa viongozi wa CHADEMA. Viongozi wanaumizwa, kama alivyofanywa Tundu Lissu, hakuna hata kuguna toka kwa watu.
Akina Mbowe na viongozi waliovurugwa, pale Kinondoni, na kutokea kifo cha yule msichana Aquilina, na akina Mbowe kukoswakoswa risasi; na hatimae kupelekwa mahakamani kwa kesi mbovu ile...,
Yote hii ni mifano ninayojaribu kujengea hoja kwa nini Mbowe hatimae alianza kuvunjika moyo. Chama kilichokuwa kimeanza kuchemsha damu za wananchi, mara hali inabadilika kiasi kile?
Viongozi hawa wamejitoa kila kitu, kwa nini wananchi hawaoni? WaTanzania hawana shukrani?
Inataka uongozi wa kipekee sana kutokatishwa tamaa na hali ilivyokuwa ikibadilika.
Na fahamu pia, kwamba, moja ya mbinu ya kumdhibiti Mbowe ilikuwa ni kuharibu biashara zake.
Mara, hali ikageuka ghafla. Magufuli hayupo tena kwenye picha. Aliyerithi uongozi, kwa hadaa zake na ulaghai, akaingiza mtindo tofauti na wa yule mtangulizi wake. Hapa ni lazima uwe mwangalifu, kwa sababu huyu mama mwanzo kabisa alitangaza "Kazi na Iendelee", na moja ya kazi kuendelea ni pamoja na kuwasurubu akina Mbowe. Kesi ya ugaidi ikaingia.
Hapa binafsi sijui kama kweli hiyo kesi ilianzia kwa Samia, au ilikuwa tayari imekwishaundwa na Magufuli kuimaliza CHADEMA moja kwa moja.
Mama pamoja na kuyumbayumba kwake wakati huo, akitaka aonekane kuwa mbali na mtangulizi wake, na hapo hapo akitaka "kazi na Iendelee" (kuwapumbaza Sukumagang), ni vigumu kujuwa ni nani mwasisi wa ile kesi.
Mama kakomaa, na kuonyesha 'commitment', ya kummaliza Mbowe. Anasema kesi hiyo ya ugaidi, ni ya kweli, kwani wenzie Mbowe tayari walisha patikana na hatia, wapo magerezani?
Taratibu, kesi mahakamani inaanza kupoteza mwelekeo (kwa hisani ya jopo hodari sana la utetezi).
Mama anayumba. Anataka aonekane kimataifa kuwa kiongozi mwenye busara, mpenda haki,n.k., n.k.,.
ANAIFUNGUA NCHI; na mengi mengine.
Utafunguaje nchi wakati akina Mbowe wako gerezani, kwa kesi isiyokuwa na kichwa wala miguu? FUTA KESI. Msamehe Mbowe!
Ngoja kwanza. Utamwachiaje Mbowe bila ya kumtumia kujiimarisha kisoiasa?
Mpango wa Mazungumzo ya MARIDHIANO ukabuniwa, kama nyenzo ya kumjenga kiuongozi mama kwa kuwa kiongozi mpatanishi.
Nashindwa kuapata njia nzuri ya kuhitimisha nadharia hii kwa ufupi ili nieleweke vizuri.
Ngoja nilazimishe kufikia mwisho:
Mbowe alipata misukosuko mingi hadi wakati wa mpango huu wa maridhiano. Mama ameahidi mengi sana mazuri, ikiwemo kuruhusu shughuli za kisiasa nchini ziendelee, na "KUFANYA MAREKEBISHO MUHIMU" katika shughuli za ucahguzi wa viongozi, na hata uwepo wa KATIBA MPYA.
Mama alikuwa hapendi kelele nyingi zinazotumiwa na viongozi wa CHADEMA; kwa hiyo alihimiza "LUGHA YENYE STAHA" tokea hapo kwenda mbele.
Mama alikuwa na dhamira hizo, za upatanisho, au ulikuwa ni ulaghai na hadaa kwa Mbowe na wengine wote?
Maoni yangu ni kuwa mama alikuwa kadhamiria, alijuwa atajijengea sifa. Lakini usisahau, mama ni kiongozi dhaifu; na pia hana msimamo imara kwa lolote. Wenye maslahi yao ndani ya CCM usiwaweke mbali kwenye maoni yako.
Mbowe aliiamini dhamira njema ya mama juu ya maridhiano; lakini na yeye alijisahau na kutokumbuka CCM kama chama ilivyo ngumu kubadili chochote, hasa kukiwa na kiongozi dhaifu kama aliyekuwa akizungumza naye.
Nimalize kabisa: Mbowe na chama alicho kiongoza kilikuwa na sera alizozipigania kwenye uongozi wake miaka yote.
"UFUNGUZI WA NCHI" alioutangaza Samia haukuwa mbali na alivyo amini Mbowe katika uhai wake wote.
Kumbuka, Mbowe hakuwa mbali sana na Kikwete katika maswala ya uchumi aliouendesha Kikwete. Hapakuwa na tofauti kubwa kati ya Kikwete na Mbowe upande huo; ukiacha pembeni matamanio ya CHADEMA kushika dola.
Sasa yupo Samia, ambaye hana tofauti upande huo, na anataka uelewano, mapatano; wafanye kazi pamoja kupitia kwenye maridhiano.
'Model', tayari ipo ya muundo unaoweza kutengenezwa. Kenya mara kadhaa, kwa sababu zao tofauti wameutumia muundo huo miaka mingi sasa; NUSU MKATE.
Sasa Mbowe kwa nini baada ya mateso yote miaka yote hii, kampata mshirika, ambaye hawatofautiani sana kisera; kwa nini asilifikirie hili?
Lakini katika mipango hiyo yote, naomba usisahau mchango wa Ulaghai/ghiliba/hadaa; na vile vile usiache kuelewa FIDIA kwa hasara alizokwisha zipata Mbowe binafsi kifedha. Mama katika yote hayo anao uwezo wa kuyatimiza; mradi tu Mbowe ahakikishe chama chake kinatua CCM; kumuimarisha samia na kumkinga na wahafidhina wa huko.
Nimemaliza.
Usinilaumu kwa lugha mbovu au kutonyooka kwa maelezo. Huu ni uandishi wa kutiririka tu bila kurudi nyuma.