Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,768
- 218,389
Baada ya kusikia uteuzi wa Ramadhan Kingai kuwa DCI, Akichukua nafasi ya Wambura , ambaye amepandishwa na kuwa IGP, watu wengi wamehoji UADILIFU wa Mamlaka ya uteuzi.
Wananchi kuhoji uteuzi huu si jambo la kushangaza, hii ni kwa sababu DCI ni Mtumishi wa umma , uteuzi wake unaweza kushangiliwa, kupuuzwa ama kuhojiwa, kuhoji uteuzi ama ajira yoyote ya mtumishi wa Umma haijawahi kuwa kosa kisheria na ndio maana Uteuzi wa Abdallah Zombe kuwa RPC Songwe ulihojiwa na hatimaye akakamatwa na kufunguliwa kesi ya aibu Mahakamani.
Kingai aliyekuwa RPC wa Kinondoni anafahamika kama Mmoja wa Maofisa wa Juu wa Jeshi la Polisi Tanzania ambaye hafahamu chochote kuhusu PGO, kwa Wasiofahamu PGO ndio mwongozo wa Jeshi la Polisi Tanzania katika utekelezaji wa Majukumu yake, PGO ndio Msahafu wa Jeshi la Polisi, asiyeifahamu hatakiwi si tu kuwa DCI, bali hatakiwi kuwa hata Konstebo, hili lilithibitika kwenye kesi ya Uongo aliyotumwa kuiandaa iliyoitwa Kesi ya Ugaidi ya Mbowe na wenzake watatu.
Kingai akishirikiana na Mtoto wa Mahita (IGP WA ZAMANI) Walihusika kuanzia kumkamata Freeman Mbowe na kupekua nyumbani kwake, ambako ALINUKULIWA AKIMWAMBIA MBOWE KWAMBA SAFARI HII HUTOKI NA TUNAKUPA KESI YA UGAIDI (Hakuwahi kukanusha), hata hivyo Mbowe alitoka na yuko huru, mtu wa namna hii kumpa cheo cha DCI ni kichekesho na kituko kikubwa na ni dharau kubwa sana kwa Watanzania kulikofanywa na Mamlaka ya Uteuzi kwa sababu ya kulewa madaraka.
Labda sasa tuambiwe MAJUKUMU MAPYA YA DCI, bali kama ni yale yanayofahamika siku zote KINGAI HAFAI NA AONDOLEWE HARAKA, Kuanza upya siyo Ujinga.