Ushauri: DCI Kingai zungumza na watendaji unaowasimamia, hali ya uhalifu imeongezeka sana nchini

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
875
4,101
Sijui kama ni Mimi peke yangu ndiye simwelewi DCI Kingai au ni watu wengi? Matukio ya Uhalifu yameongezeka Sana siku za hivi karibuni. Polisi kutunishiana misuli na raia limekuwa Jambo la kawaida lakini kibaya zaidi NI kuongezeka Kwa matukio ya Askari kufanya mauaji Kwa raia kizembe wakati wanatekeleza majukumu Yao.

Haya yote yanatokea wakuu wapolisi WA mikoa ndio wamebaki na dhamana yakujichunguza au kutolea ufafanuzi matukio yaliyotendwa na Askari waliopo kwenye maeneo Yao. Kutoa taarifa siyo tatizo, tatizo kubwa NI Aina ya taarifa wanayotoa. Nimpongeze RPC Rorya ameweza kuweka wazi kwenye taarifa yake kwamba Askari wameua Kwa uzembe na wamekamatwa.

Huko Geita Askari Kwa kushirikiana na wataalam wataalam WA afya wametoa taarifa ya uongo na kupelekea kituo cha polisi kuchomwa Moto na wananchi Kugoma kumzika mpendwa wao. Kwanini polisi walidanganya, nikutokana na ukweli kwamba bado DCI ajataka kujipambanua kama mpenda Haki.

Lakini pia kuonyesha kwamba bado majukumu yake yanapwaya, ameelekezwa na IGP aende Geita kuzungumza na wananchi; hii siyo sawa. Alipaswa yeye mwenyewe kuunda tume ya uchunguzi asubiri kuletewa taarifa akiwa kama bosi WA uchunguzi nchini. Tukio lile linahusu jinai ambayo yeye ndiye mwenye final opinion kwenye uchunguzi WA jinai; anapokwenda field ataepuka vipi kuwa biased kwenye matokeo ya uchunguzi?

Lakini pia katika eneo jingine ninapotaka ayachungulie vyema majukumu yake ni kuhusu wizi uliofanywa kwenye mfuko wa maafa wa Jeshi la polisi. CAG amesema na Mhe Rais akasema; tulitegemea yeye kama mkuu WA upelelezi awe ameanza kuchukua hatua lakini hakuna hatua zilizochukuliwa badala yake mtuhumiwa mmoja anaripotiwa yupo S. Africa eti katoroka.

Wakati mtuhumiwa akiripotiwa kutoroka kamati ya chama tawala chini ya Mwenyekiti ambaye NI Mhe. Rais inatoka na maazimio kwamba hatua zichuliwe Kwa wote walioiba Mali za umma. DCI Kwa kipindi hiki hakupaswa kwenda Geita alipaswa kutuambia NI hatua gani ameanza kuchukua kutekeleza maelekezo ya Mhe. Rais.

Hii nitafakuri yangu naweza nikawa nawaza sahihi au wrong ila nimewaza kumsaidia Kingai kuchanga karata vyema kwenye kiti alichokalia. Wapo wengi wanakimendea hivyo nampa ushauri awe active, professional, leader na aboreshe mahusiano Kati yake na mnyororo mzima WA upelelezi nchini. Awakumbushe watendaji wake Do and Don't itamsaidia Sana kuvuka kiunzi kilichopo mbele yake.

Mwisho, nimwonbe akae vizuri na DPP aliyepo sasa; simfahamu vyema Ila kuna mabadiliko naamini ameyafanya Kwa waendesha mashtaka...kelele dhidi ya Ofisi ya DPP zimepungua Kwa Kasi Sana. Maana yake huyu akiwa ni mdau mkubwa WA wapelelezi basi achote strategy kwake kelele za upelelezi zipungue kwenye jamaa na trust irudi.

Narudia tena, maoni haya siyo binding, nimaoni binafsi kuhusu kuongezeka Kwa Uhalifu, upashanaji habari na uwezo wakurespond Kwa wakati periority issue. Amri ya Mhe. Rais ni kubwa, aangalie wakati na ajifunze kudeligate powers
 
Kosa alilolifanya Mh. Rais linawagharimu Watanzania wote. Haiwezekani Mtu aliyeonyesha uwezo mkubwa wa kubambikia raia kesi apewe Ukuu wa Upelelezi na Uchunguzi nchini. Kosa la mama linaanzia hapo. Waliomshauri kumteua Kingai kuwakomoa wapinzani àmbao Sasa karidhiana nao walimpotosha pakubwa.

Askari wanayofanya yanaendana na Tabia halisi za Mkurugenzi wa Upelelezi, usitegemee akaja na jipya katika uchunguzi wa Geita.

Yeye mwenyewe ni mtaalamu wa kupindisha ukweli, RPC Geita amepita mlemle. Kesi ya Geita ni mwendelezo wa ujinga wa Askari wetu na kama wangekuwa na viongozi wanaojitambua usingeona maigizo ya RPC.

Bodaboda katumwa kupeleka betri chaji, baadaye kaambiwa ifuate. Kwa maelezo yake karudisha jibu Kwa mteja wake kwamba betri haipo. Mteja kaenda kumshitaki Polisi maana yeye ndo kakabidhiwa.

Polisi wamemkamata Bodaboda, Kwa uelewa wangu baada ya kumkamata ingekuwa vizuri wangeanzia alikosema amepeleka betri kichajiwa kujiridhisha kama betri ilifika na Nini kilichopelekea betri kutoonekana. Lakini Polisi wetu wanaanza Upelelezi Kwa torture Hadi Bodaboda anapoteza fahamu.

Uliza thamani ya betri ni Tshs. 150,000 - 200000/-. Dhambi nyingine Polisi wanajitafutia bila sababu. RPC unawezaje kufunika uzembe wa kipuuzi kama huu eti Bodaboda alijisikia vibaya, akawahishwa hospitali, akafa Habari ziwafikie?

Suala la mfuko wa Kufa na Kuzikana nadhani CAG ifike mahali aliache Kwa Askari wenyewe waamue maana hii ni fedha Yao wenyewe na kama wameamua kukaa kimya waachwe maana hii si fedha ya serikali.

Haiwezekani unachangia Kwa Hiari 5000 Kila mwezi halafu fedha yako inaliwa wala hushituki na Hakuna hatua unazochukua ukisubiri CAG. Kwani huo mfuko hauna Kamati ya uendeshaji?

Tuchukulie Kamati ndo imehusika maana ndio kuna signatory, je waliobaki baada ya mmoja kukimbia wamefanywa nini maana si rahisi 4.8b ikaliwa na Askari mwenye cheo cha nyota 2 Peke yake. Huu ni mwendelezo wa Taarifa za kupikwa àmbao Jeshi la Polisi limejitahidi kuzitoa Kila linapotuhumiwa.

Nataka niseme ninachoamini na binafsi naamini ndicho kilichotokea. Fedha hii sehemu kubwa imechotwa Kwa amri ya IG aliyekuwepo maana fedha hii imepotelea Dar es salaam na kanda zake kubwa za Temeke, Kinondoni na Ilala.

Kwa mujibu wa Taarifa ya awali mwenye cheo kikubwa Kati ya watuhumiwa wapatao 8 waliokamatwa awali ni Huyo aliyetoroka akiwa mafunzo ya kuwania nyota ya 3.

Kama wengine waliweza kukamatwa, Nani aliyemshitua huyu aliyekuwa rahisi kupatikana kwenye mazingira ya chuo? Nani alitoa Taarifa eneo la Upelelezi kupeleka chuoni? Kama mpelelezi unajua "King Pin" alipo unaanzaje kukamata dagaa?

Kwa maoni hayo sioni haja ya CAG kuendelea na hili, awaachie Wenye hela zào maana walishazoea kudhulumu Kwa hiyo wakidhulumiwa wanaona Sawa tu.
 
Kwani Kingai ana usafi gani wa kukemea maovu. Huyu ndie alie watungia watu wengi kesi.
Huyu akiwa Arusha ndie alikuwa akiongoza genge la kina Sabaya na yule askari alie muibia profesa kule Usa.
Hizi teuzi za kifalme zina ukakasi mkubwa sana
 
As long as yeye ndiye mwenye taasisi na ameaminiwa nafasi yetu nikumshauri afanye vizuri zaidi........yawezekana Kingai Hana Roho mbaya kama comments zinavyoonyesha Ila regime ya kipindi kile ilimfanya aonekane kama kiumbe katili.

Hizi nafasi za uteuzi za ulimwengu wa tatu zinakulazimisha uishi maisha ya bosi wako kuliko maisha yako
 
Naibu RCO Moro ni mdau wa matapeli wa Ardhi, sijui kama bado yupo, alikuwa analala kwenye moja ya loji za matapeli hao
 
Back
Top Bottom