dubu
JF-Expert Member
- Oct 18, 2011
- 3,496
- 3,461
Shikamoo Rais Samia
Huyu Kingai anaenda kutumaliza, visasi vingi na atahakikisha wabaye wake wanakipata cha mtemakuni.
Kingai haijui hata PGO, atakuwaje Mkurugenzi wa Upelelezi? Twafwa.
Kesi dhidi ya Mbowe ya Ugaidi, nilitegemea imfumbue macho Rais ili ajue waliomzunguka. Naamini rais kashauriwa Vibaya. Tusimlaumu sana sababu bado anayo nafasi ya kubadilisha.
Huu ndo Ushauri Lukuvi anampa rais wetu? Kingai? Huyu wa Kinondoni au yupo Kingai mwingine Jeshini?
Kama Afande Kingai angesoma PGO vizuri, angegundua kuwa SHTAKA linafunguliwa BAADA ya mtuhumiwa KUHOJIWA! Ikibainika "maelezo ya onyo" yanafichua KOSA, ndipo Jalada la Mashtaka HUANDALIWA. Kingai alipoulizwa na Wakili wa Serikali kwanini aliwatoa watuhumiwa Moshi kuwaleta DSM,
alijibu, "huko ndiko mashtaka yao yalipofunguliwa!" Sasa, ilikuwaje ukafungua mashtaka ya hawa Vijana wakati bado hawajakamatwa, na wala KUHOJIWA!
PGO isomwe jamani, tena isomwe vizuri! Mnadhalilisha hili Jeshi.
Kingai alimnyima dhamana mtu aliyehoji kutaka kujua kama Hayati Magufuli anaumwa. Eti hakupasa kuhoji akakamatwa akapigwa na kunyimwa dhamana.
Aloshiriki kumdanganya rais Samia ili amteue Kingai, achukuliwe hatua.