Je, majukumu ya DCI ni yapi? Asiyeijua PGO awezaje kuwa DCI?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
116,472
215,294
Baada ya kusikia uteuzi wa Ramadhan Kingai kuwa DCI, Akichukua nafasi ya Wambura , ambaye amepandishwa na kuwa IGP, watu wengi wamehoji UADILIFU wa Mamlaka ya uteuzi.

Wananchi kuhoji uteuzi huu si jambo la kushangaza, hii ni kwa sababu DCI ni Mtumishi wa umma , uteuzi wake unaweza kushangiliwa, kupuuzwa ama kuhojiwa, kuhoji uteuzi ama ajira yoyote ya mtumishi wa Umma haijawahi kuwa kosa kisheria na ndio maana Uteuzi wa Abdallah Zombe kuwa RPC Songwe ulihojiwa na hatimaye akakamatwa na kufunguliwa kesi ya aibu Mahakamani.

Kingai aliyekuwa RPC wa Kinondoni anafahamika kama Mmoja wa Maofisa wa Juu wa Jeshi la Polisi Tanzania ambaye hafahamu chochote kuhusu PGO, kwa Wasiofahamu PGO ndio mwongozo wa Jeshi la Polisi Tanzania katika utekelezaji wa Majukumu yake, PGO ndio Msahafu wa Jeshi la Polisi, asiyeifahamu hatakiwi si tu kuwa DCI, bali hatakiwi kuwa hata Konstebo, hili lilithibitika kwenye kesi ya Uongo aliyotumwa kuiandaa iliyoitwa Kesi ya Ugaidi ya Mbowe na wenzake watatu.

Kingai akishirikiana na Mtoto wa Mahita (IGP WA ZAMANI) Walihusika kuanzia kumkamata Freeman Mbowe na kupekua nyumbani kwake, ambako ALINUKULIWA AKIMWAMBIA MBOWE KWAMBA SAFARI HII HUTOKI NA TUNAKUPA KESI YA UGAIDI (Hakuwahi kukanusha), hata hivyo Mbowe alitoka na yuko huru, mtu wa namna hii kumpa cheo cha DCI ni kichekesho na kituko kikubwa na ni dharau kubwa sana kwa Watanzania kulikofanywa na Mamlaka ya Uteuzi kwa sababu ya kulewa madaraka.

Labda sasa tuambiwe MAJUKUMU MAPYA YA DCI, bali kama ni yale yanayofahamika siku zote KINGAI HAFAI NA AONDOLEWE HARAKA, Kuanza upya siyo Ujinga.
 
hili lilithibitika kwenye kesi ya Uongo aliyotumwa kuiandaa iliyoitwa Kesi ya Ugaidi ya Mbowe na wenzake watatu , Kingai alihusika...
Mbowe ashawambieni siasa za majitaka achaneni nazo, ila hamtaki usikia. Ukute Mbowe mwenyewe ashampigia mama kumpongeza kwa uteuzi huu, afu chawa from nowhere unakuja kujifanya una uchungu nae sana kuliko anavyojionea uchungu mwenyewe.

Hii ni aibu kubwa, siasa za namna hii hazina afya tena kwenye taifa letu, haswa baada ya wale waliokuwa viongozi wa chawa kulambishwa asali na mwenye mzinga.

Screenshot_20220605-082514_1.jpg
 
Mbowe ashawambieni siasa za majitaka achaneni nazo, ila hamtaki usikia. Ukute Mbowe mwenyewe ashampigia mama kumpongeza kwa uteuzi huu, afu chawa from nowhere unakuja kujifanya una uchungu nae sana kuliko anavyojionea uchungu mwenyewe. Hii ni aibu kubwa, siasa za namna hii hazina afya tena kwenye taifa letu, haswa baada ya wale waliokuwa viongozi wa chawa kulambishwa asali na mwenye mzinga.
Uzi huu ni kwa Maslahi ya Taifa
 
PGO gani mkuu unafikri yale ya kijinga ya wanasheria ndoo yanaweza mfanya asiwe mwelewa kwa taarifa yako Ramadhan kingai alikuwa Rco mkoa arusha mkoa huo siyo lelemama huyo jamaa yupi vizuri sana kesi ya mbowe mnaona kama hafai kwa kuwa huruma ya samia mbowe alitoka mahabusu lakini juwa angewaka mvua kesi nyingi zilizopita kwa kingai nyingi zinamafinikio huyo jamaa siyo wa mchezo
 
Huna lolote wewe chawa , endelea kuishi kwa hisani
 
Baada ya kusikia uteuzi wa Ramadhan Kingai kuwa DCI, Akichukua nafasi ya Wambura , ambaye amepandishwa na kuwa IGP , watu wengi wamehoji UADILIFU wa Mamlaka ya uteuzi.

Wananchi kuhoji uteuzi huu si jambo la kushangaza, hii ni kwa sababu DCI ni Mtumishi wa umma , uteuzi wake unaweza kushangiliwa, kupuuzwa ama kuhojiwa, kuhoji uteuzi ama ajira yoyote ya mtumishi wa Umma haijawahi kuwa kosa kisheria na ndio maana Uteuzi wa Abdallah Zombe kuwa RPC Songwe ulihojiwa na hatimaye akakamatwa na kufunguliwa kesi ya aibu Mahakamani.

Kingai aliyekuwa RPC wa Kinondoni anafahamika kama Mmoja wa Maofisa wa Juu wa Jeshi la Polisi Tanzania ambaye hafahamu chochote kuhusu PGO, ambao ndio mwongozo wa Jeshi hilo, hili lilithibitika kwenye kesi ya Uongo aliyotumwa kuiandaa iliyoitwa Kesi ya Ugaidi ya Mbowe na wenzake watatu, Kingai alihusika kuanzia kumkamata Freeman Mbowe na kupekua nyumbani kwake, ambako ALINUKULIWA AKIMWAMBIA MBOWE KWAMBA SAFARI HII HUTOKI NA TUNAKUPA KESI YA UGAIDI, hata hivyo Mbowe alitoka na yuko huru, mtu wa namna hii kumpa cheo cha DCI ni kichekesho na kituko kikubwa na ni dharau kubwa sana kwa Watanzania kulikofanywa na Mamlaka ya Uteuzi kwa sababu ya kulewa madaraka .

Labda sasa tuambiwe MAJUKUMU MAPYA YA DCI , bali kama ni yale yanayofahamika siku zote KINGAI HAFAI NA AONDOLEWE HARAKA, Kuanza upya siyo Ujinga.
Acha ujinga Erythrocyte kuna maeneo mawili nchi hii kuyafanyia kazi sio lazima uwe na akili na chamsingi uwe mbumbumbu. Maeneo hayo ni haha;

1. CCM
2. POLICE
 
Baada ya kusikia uteuzi wa Ramadhan Kingai kuwa DCI, Akichukua nafasi ya Wambura , ambaye amepandishwa na kuwa IGP , watu wengi wamehoji UADILIFU wa Mamlaka ya uteuzi.

Wananchi kuhoji uteuzi huu si jambo la kushangaza, hii ni kwa sababu DCI ni Mtumishi wa umma , uteuzi wake unaweza kushangiliwa, kupuuzwa ama kuhojiwa, kuhoji uteuzi ama ajira yoyote ya mtumishi wa Umma haijawahi kuwa kosa kisheria na ndio maana Uteuzi wa Abdallah Zombe kuwa RPC Songwe ulihojiwa na hatimaye akakamatwa na kufunguliwa kesi ya aibu Mahakamani.

Kingai aliyekuwa RPC wa Kinondoni anafahamika kama Mmoja wa Maofisa wa Juu wa Jeshi la Polisi Tanzania ambaye hafahamu chochote kuhusu PGO, kwa Wasiofahamu PGO ndio mwongozo wa Jeshi la Polisi Tanzania katika utekelezaji wa Majukumu yake , PGO ndio Msahafu wa Jeshi la Polisi , asiyeifahamu hatakiwi si tu kuwa DCI , bali hatakiwi kuwa hata Konstebo , hili lilithibitika kwenye kesi ya Uongo aliyotumwa kuiandaa iliyoitwa Kesi ya Ugaidi ya Mbowe na wenzake watatu, Kingai akishirikiana na Mtoto wa Mahita ( IGP WA ZAMANI ) Walihusika kuanzia kumkamata Freeman Mbowe na kupekua nyumbani kwake, ambako ALINUKULIWA AKIMWAMBIA MBOWE KWAMBA SAFARI HII HUTOKI NA TUNAKUPA KESI YA UGAIDI, ( Hakuwahi kukanusha ) , hata hivyo Mbowe alitoka na yuko huru, mtu wa namna hii kumpa cheo cha DCI ni kichekesho na kituko kikubwa na ni dharau kubwa sana kwa Watanzania kulikofanywa na Mamlaka ya Uteuzi kwa sababu ya kulewa madaraka .

Labda sasa tuambiwe MAJUKUMU MAPYA YA DCI , bali kama ni yale yanayofahamika siku zote KINGAI HAFAI NA AONDOLEWE HARAKA, Kuanza upya siyo Ujinga.
Watu wengi tumeshangaa mamlaka za uteuzi kufanya haya, labda ni Asante kwa kufanya aliyotumwa! Labda ni kusikiliza mamlaka kwa Kila anapopokea maagizo Toka juu hata kama hayana impact! Inatufanya tuamini sasa kwamba asali ya nchi hii inalambishwa kwa watu wa aina Moja tu? Na hili lisipopigiwa kelele huko tuendapo litaleta shida, nchi hii iswe ni ya aina ya watu wanaomfurahisha Alie juu tu, Tusifikia kama ya wahutu na watusi, tukaaminishwa Walamba Asali ni watu wa aina Fulani tu, na wengingine ni Walamba Simu. Mamlaka Angalieni Hili, wananchi hatupendezwi na hili!!
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom