Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 62,735
- 105,419
Kwa nini asiyefanya kazi asile ?Akina nani hao?. Wakati Biblia inasema asiye fanya kazi na asile. Unajikanyaga sana.
Kwa nini asiyefanya kazi asile ?Akina nani hao?. Wakati Biblia inasema asiye fanya kazi na asile. Unajikanyaga sana.
Biblia nimeisoma kuliko hata wewe.Ni hadithi kwako usiye jua Biblia.
Biblia imejaa logical contradictions za kutosha.Kasome na fanya utafiti kuhusu Biblia ndio uje na conclusion kwamba ni hadithi. Kwa mfano amri kumi ni hadithi? Au kuambiwa kuwa watakufa?
Haha, umejitahidi sana kukariri hiyo google definition ya infinite regress lakini unachanganya kitu kimoja kikubwa mno, ulimwengu wetu umeundwa na vitu vinavyobadilika na vinavyotegemea vitu vingine ili viwepo.If nothing comes from nothing.
Hata hicho chanzo cha kwanza cha ulimwengu, Hakiwezi kukwepa kanuni hii.
Hicho chanzo cha kwanza cha ulimwengu hakiwezi kutokea tu from nothing.
Kama chanzo cha kwanza cha ulimwengu kinaweza kukwepa kanuni hii ya " nothing comes from nothing" Basi hata Ulimwengu wenyewe unaweza kukwepa kanuni hii.
Na ulimwengu ukawa ndio mwanzo wenyewe. Bila kuhitaji chanzo kingine.
Lakini tukisimama kwenye kanuni hii ya nothing comes from nothing . Tunarudi kule kwenye infinite regress of causes.
An infinite regress of causes is an endless chain of events where every cause has its own prior cause going back forever. There is no first event, no start, and no uncaused beginning.
Ambapo, Hapapaswi kuwa na chochote kilicho anza chenyewe tu, from nothing.
Hivyo kutakuwa na msururu mrefu wa vyanzo vingi visivyokuwa na mwisho. Pasipo ku stop!
Haha, umecheza vizuri sana na maneno ya google, lakini umejifunga goli lingine la mkono. Kama ukisema hakuna ubaguzi, na kila kitu lazima kitii sheria moja ya kuwa na chanzo kilichokizaa, mbona hapo awali ulidai binadamu na dunia wamekuwepo milele bila mwanzo?Hata Ulimwengu si lazima uwe umeumbwa.
Na wala ulimwengu hauhitaji kuumbwa.
Lakini kama ni lazima ulimwengu uwe uliumbwa, Hata huyo muumbaji wa ulimwengu atahitaji kuumbwa.
Na huyo muumbaji wa muumba ulimwengu atahitaji kuumbwa.
Patakuwa tena na msururu mrefu wa waumbaji wengi, pasipo kukoma.
Kama kuumbwa ni lazima basi ulazima huu itabidi u-apply kwa kila kitu. Including huyo muumbaji mwenyewe.
Kumu exclude huyo muumbaji kwenye "ulazima wa kuumbwa" halafu kufosi vitu vingine viwe viliumbwa ni kufanya logical fallacy inaitwa special pleading fallacy.
The special pleading fallacy happens when someone applies a general rule to everyone else, but claims an unjustified exception for themselves or their topic. It relies on a double standard and changes the criteria mid-argument without a valid reason.
Kwa hiyo kama kuumbwa ni lazima. Basi ulazima huu ni kwa kila kitu. Pasiwepo chochote kile kilicho exist chenyewe bila kuumbwa. Including huyo muumbaji.
We jamaa unajua hata hiyo Pre-Adamite theory ina maana gani kweli?Sasa hii theory yako ina tofauti gani na pre-adamite theory iliyo sehemu ya mleta uzi?😂
Hapa ndo Athieat huwa wanapotea na kukimbia...Na Mama yake.
Viongozi wa dini.Akina nani hao?.
Hao wachungaji na manabii wanafanya kazi gani kama sio utapeli wa kulaghai waumini na kuwadanganya ili wapate ulaji wao?Wakati Biblia inasema asiye fanya kazi na asile. Unajikanyaga sana.
Na bado tunapata sifa za Mwenyezi Mungu kwamba hana mwanzo!Kuna jambo la kuvutia sana katika Mwanzo 1:2 “Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu; na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji.” Aya hii inaweza kutufanya tujiulize swali ambalo mara nyingi tunalipita: nini kilitokea kabla ya hali hii ya ukiwa na utupu? Biblia haitoi maelezo ya moja kwa moja kwamba kulikuwa na vita au viumbe waliokuwa wakiishi duniani kabla ya mwanadamu, lakini ukitazama kwa jicho la udadisi, unaweza kujiuliza ikiwa kulikuwa na tukio fulani lililosababisha hali hiyo ya machafuko. Labda kulikuwa na mabadiliko makubwa, labda machafuko, au hata vita lakini haya ni mawazo ya kutafakari, si ukweli uliothibitishwa na maandiko.
Kama tunaruhusu akili ichunguze zaidi, tunaweza kujiuliza je, “ukiwa na utupu” ilikuwa hali ya mwanzo kabisa, au ilikuwa matokeo ya jambo lililotokea kabla ya simulizi kuanza? Mungu anaonekana kuleta nuru, mpangilio na uhai katika mazingira yaliyoelezwa kuwa na giza na vilindi vya maji. Hii inaweza kutufanya tufikirie uwezekano wa “reset” ya uumbaji si kwamba Biblia inasema Mungu alifanya reset baada ya vita, bali kama hypothesis ya kifalsafa. Huenda kulikuwa na historia ambayo haijaelezwa huenda hakuna kitu kilichokuwepo kabla yake. Pengo hilo ndilo linaloifanya akili iulize.
Udadisi huu unaweza kuonekana hata katika simulizi la baadaye la Adamu, Hawa na Kaini. Baada ya Kaini kumuua Abeli, Kaini anaonekana kuwa na hofu kwamba “kila mtu atakayeniona ataniua,” na baadaye anaenda kuishi katika nchi nyingine na anapata mke. Hapo ndipo maswali yanapoanza: hao watu aliowaogopa walikuwa nani? Mke wa Kaini alitoka wapi? Na kizazi chake kilianzaje? Kuna maelezo mbalimbali ya kitheolojia kuhusu maswali haya, lakini simulizi lenyewe halitoi kila hatua kwa undani. Hii inatukumbusha kwamba Biblia mara nyingi haituelezi kila kitu kuhusu mazingira ya hadithi.
Kwa hiyo, inawezekana kabisa mtu akauliza kwa udadisi: kama kuna mambo ambayo hatupewi maelezo kamili kuhusu dunia baada ya Adamu na Hawa, je, tunaweza kuwa na uhakika kabisa kwamba tunaelewa kila kitu kuhusu hali iliyokuwepo kabla ya Mwanzo 1:2? Labda kulikuwa na machafuko ambayo hatujui chochote kuhusu chanzo chake labda kulikuwa na viumbe au matukio ambayo hayakutajwa au labda “ukiwa na utupu” ilikuwa tu hali ya dunia kabla Mungu hajaiweka katika mpangilio. Hatuwezi kuchagua mojawapo na kuiita ukweli bila ushahidi lakini tunaweza kuiruhusu akili yetu kuiuliza.
Ndiyo maana udadisi ni muhimu. Udadisi hauimaanishi kukataa Biblia unaweza kumaanisha kuisoma kwa kina zaidi na kutambua tofauti kati ya kile maandiko yanasema na kile sisi tunachodhani. Labda kabla ya mwanadamu hakukuwa na vita kabisa; labda kulikuwa na tukio ambalo hatulijui au labda hakukuwa na historia yoyote ya aina hiyo. Lakini swali linabaki ikiwa Mwanzo 1:2 inatupa picha ya dunia ikiwa katika ukiwa, utupu, giza na vilindi vya maji, ni nini kilichotokea kabla ya pazia hilo kufunguliwa? Huenda hatutapata jibu kamili, lakini kuuliza swali hilo kunaweza kutufanya tusome zaidi, tufikiri zaidi, na tutambue kwamba wakati mwingine kutokujua ndiko kunakoanzisha safari ya kutafuta maarifa.
Hiyo akili yako finyu ndiyo inafikiri kwamba kila usichokijua wewe na mwingine hajui.Haha, umejitahidi sana kukariri hiyo google definition ya infinite regress
Ulimwengu unategemea nini ili uwepo?lakini unachanganya kitu kimoja kikubwa mno, ulimwengu wetu umeundwa na vitu vinavyobadilika na vinavyotegemea vitu vingine ili viwepo.
Kitu chochote kinachotegemea kingine hakiwezi kuwa chanzo cha mwanzo, lazima kuwe na chanzo cha kwanza ambacho chenyewe hakitegemei kitu kingine, yani kiwe nje ya sheria za physics ya ulimwengu wetu.
Nilikwambia pale mwishoni kama ulisoma vizuri, Maana najua husomi vizuri kwa ufahamu unakurupuka tu.Haha, umecheza vizuri sana na maneno ya google, lakini umejifunga goli lingine la mkono. Kama ukisema hakuna ubaguzi, na kila kitu lazima kitii sheria moja ya kuwa na chanzo kilichokizaa, mbona hapo awali ulidai binadamu na dunia wamekuwepo milele bila mwanzo?
Kwa hiyo kama SIO lazima kwamba kila kilichopo kinahitaji kuwa na chanzo, Hata Ulimwengu hauna na wala hauhitaji kuumbwa.Mbona hukuwawekea hiyo sheria yako hapo mwanzo? Huoni kuwa wewe ndiye unayefanya special pleading kwa kuilazimisha dunia iwe ya milele wakati sayansi inasema ina mwanzo?
Wajinga wa kale.Nani alitunga hizo hadithi?
Athieat❌️Hapa ndo Athieat huwa wanapotea na kukimbia...
Wewe hata kuandika Atheist hujui.Unaposema maisha yana chanzo nacho ni mama... Unakuwa umedogosha the natural order of energy or vibration
We both know that energy is neither created nor destroyed kwanini tu nadhani complex arrangement of atoms kama mwili wa mwanadamu una chanzo chake?
Kwanini tusijisemee ya kuwa na sisi ni infinite beings.. Yaani hata kama tutaenda extinct siku moja haimaanishi eti tumepotea... Ile spirit ambayo ndo life lenyewe itaendelea ku roam around ila is ipate avatar?
It is only a fool who cares about puctuationAthieat❌️
Atheist✅️
Wewe hata kuandika hujui.
Wewe hata kuandika Atheist hujui.
Una andika Athieat❌️
Unachanganya lugha tu, kwa kuandika pumba na mashudu.
Wala hakuna point yeyote.
Haha, kaka umepaniki hadi ukaenda Google haraka haraka kutafuta jina la Aristotle ili uje hapa na hoja uchwara za kukufanya uonekane na wewe zimo kumbe debe tupu, umefeli vibaya mno.Hiyo akili yako finyu ndiyo inafikiri kwamba kila usichokijua wewe na mwingine hajui.
Kwamba wengine wakijua, hawajui from their understanding but from Google.
Kwamba unavyojua wewe, Google haivijui.
Labda tu nikwambie, kwa sababu najua hujui na ulikuwa hujui, Infinite regress ni hoja iliyoibuliwa na Aristotle.
Kwa sababu akili yako inafikiri kwamba kila unayejadili naye humu anakariri.
Hii ni hoja ambayo iliibuliwa na Aristotle.
Na wala ulikuwa hujui.
Safi sana, unapaswa kuuliza maswali yenye akili kama haya, ulimwengu wetu umeundwa na vitu vinavyobadilika, vinavyoanza na kuisha, kimantiki, kitu chochote ambacho hakina ulazima wa kuwepo hakiwezi kujitegemea chenyewe, lazima kitegemee kitu chenye ulazima wa kuwepo ambacho chenyewe hakina mwanzo wala mwisho.Ulimwengu unategemea nini ili uwepo?
Thibitisha.
Naona bado unakariri ule ule usemi wako wa Google bila kuelewa! Narudia kumuelewesha tena maana unaonekana una dondoo lakini huna uelewa, sheria ya mantiki haisemi kila kilichopo kina chanzo, inasema hivi kila kilichoanza kuwepo kina chanzo, ulimwengu una mwanzo kwahiyo unahitaji chanzo.Nilikwambia pale mwishoni kama ulisoma vizuri, Maana najua husomi vizuri kwa ufahamu unakurupuka tu.
Nilisema hivi...👇
Kama kila kitu kilichopo kitahitaji kuwa na chanzo chake, Hata chanzo cha kila kitu kitahitaji kuwa na chanzo chake kingine.
Hivyo kutakuwa na msururu mrefu wa vyanzo vingi visivyokuwa na mwisho.
Na kama SI lazima kila kilichopo kinahitaji kuwa na chanzo, Hata Ulimwengu na vyote vilivyomo except man-made things, Havina na havihitaji kuwa na chanzo.
👆...Soma hapo juu vizuri uelewe...
Point yako ni ipi haswa hapa ?Ukiachana na dhana za Ki biblical
Dunia Kamwe isingekuwa smooth... Kuna nyakati, kuna hurricanes, kuna tectonic movements.. Kuna vitu vingi tu vya kusababisha machafu ko na hata kiumbe asihusike
Mm naona dini zimewaharibu watu wengi sana
Yale yote ambayo ni nadharia huenda yakawa na ukweli kabisaPoint yako ni ipi haswa hapa ?
Good.Yale yote ambayo ni nadharia huenda yakawa na ukweli kabisa
HakikaGood.
Hili ni swala la knowledge ya kawaida tu, ambapo kila mtu inabidi aelewe kwamba biblia ina Multifaceted complications kwahiyo baadhi ya nadharia znaweza zikawepo kwasababu biblia haijaeleza kilakitu kwa uwazi.
Baadhi ya waumini wa dini huchoka kiakili wanapokutana na vifungu fulani na hivyo kushindwa kuelewa nadharia zilizomo ndani yake pamoja na maana ya kina ya kile kilichoandikwa, kama hao wanao niambia kaini alioa ndugu yake na hawataki kubishiwa na hawana evidence wafia dini ni kazi kweli kweli.Hakika
Na zimetumia lugha ya mafumbo ili tuweze kupambanua spiritual essence ya vitu vilivyo kwisha kuwepo
Biblia imeanza kwa kusema hapo mwanzo(time) M-ngu aliziumba Mbingu(space) na Nchi(matter) sasa swali ni kuwa je kuna kiumbe chochote kinaishi nje ya hayo mambo matatu?Kuna jambo la kuvutia sana katika Mwanzo 1:2 “Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu; na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji.” Aya hii inaweza kutufanya tujiulize swali ambalo mara nyingi tunalipita: nini kilitokea kabla ya hali hii ya ukiwa na utupu? Biblia haitoi maelezo ya moja kwa moja kwamba kulikuwa na vita au viumbe waliokuwa wakiishi duniani kabla ya mwanadamu, lakini ukitazama kwa jicho la udadisi, unaweza kujiuliza ikiwa kulikuwa na tukio fulani lililosababisha hali hiyo ya machafuko. Labda kulikuwa na mabadiliko makubwa, labda machafuko, au hata vita lakini haya ni mawazo ya kutafakari, si ukweli uliothibitishwa na maandiko.
Kama tunaruhusu akili ichunguze zaidi, tunaweza kujiuliza je, “ukiwa na utupu” ilikuwa hali ya mwanzo kabisa, au ilikuwa matokeo ya jambo lililotokea kabla ya simulizi kuanza? Mungu anaonekana kuleta nuru, mpangilio na uhai katika mazingira yaliyoelezwa kuwa na giza na vilindi vya maji. Hii inaweza kutufanya tufikirie uwezekano wa “reset” ya uumbaji si kwamba Biblia inasema Mungu alifanya reset baada ya vita, bali kama hypothesis ya kifalsafa. Huenda kulikuwa na historia ambayo haijaelezwa huenda hakuna kitu kilichokuwepo kabla yake. Pengo hilo ndilo linaloifanya akili iulize.
Udadisi huu unaweza kuonekana hata katika simulizi la baadaye la Adamu, Hawa na Kaini. Baada ya Kaini kumuua Abeli, Kaini anaonekana kuwa na hofu kwamba “kila mtu atakayeniona ataniua,” na baadaye anaenda kuishi katika nchi nyingine na anapata mke. Hapo ndipo maswali yanapoanza: hao watu aliowaogopa walikuwa nani? Mke wa Kaini alitoka wapi? Na kizazi chake kilianzaje? Kuna maelezo mbalimbali ya kitheolojia kuhusu maswali haya, lakini simulizi lenyewe halitoi kila hatua kwa undani. Hii inatukumbusha kwamba Biblia mara nyingi haituelezi kila kitu kuhusu mazingira ya hadithi.
Kwa hiyo, inawezekana kabisa mtu akauliza kwa udadisi: kama kuna mambo ambayo hatupewi maelezo kamili kuhusu dunia baada ya Adamu na Hawa, je, tunaweza kuwa na uhakika kabisa kwamba tunaelewa kila kitu kuhusu hali iliyokuwepo kabla ya Mwanzo 1:2? Labda kulikuwa na machafuko ambayo hatujui chochote kuhusu chanzo chake labda kulikuwa na viumbe au matukio ambayo hayakutajwa au labda “ukiwa na utupu” ilikuwa tu hali ya dunia kabla Mungu hajaiweka katika mpangilio. Hatuwezi kuchagua mojawapo na kuiita ukweli bila ushahidi lakini tunaweza kuiruhusu akili yetu kuiuliza.
Ndiyo maana udadisi ni muhimu. Udadisi hauimaanishi kukataa Biblia unaweza kumaanisha kuisoma kwa kina zaidi na kutambua tofauti kati ya kile maandiko yanasema na kile sisi tunachodhani. Labda kabla ya mwanadamu hakukuwa na vita kabisa; labda kulikuwa na tukio ambalo hatulijui au labda hakukuwa na historia yoyote ya aina hiyo. Lakini swali linabaki ikiwa Mwanzo 1:2 inatupa picha ya dunia ikiwa katika ukiwa, utupu, giza na vilindi vya maji, ni nini kilichotokea kabla ya pazia hilo kufunguliwa? Huenda hatutapata jibu kamili, lakini kuuliza swali hilo kunaweza kutufanya tusome zaidi, tufikiri zaidi, na tutambue kwamba wakati mwingine kutokujua ndiko kunakoanzisha safari ya kutafuta maarifa.
Debe tupu ni wewe zumbukuku.Haha, kaka umepaniki hadi ukaenda Google haraka haraka kutafuta jina la Aristotle ili uje hapa na hoja uchwara za kukufanya uonekane na wewe zimo kumbe debe tupu, umefeli vibaya mno.
Thibitisha kuna huyo unayemwita unmoved mover.Aristotle aliandika kuhusu Infinite Regress, na alifanya hivyo ili kuikataa na kuithibitisha dhana yake ya unmoved mover, yaani unamtumia mwanafalsafa aliyesema lazima kuwe na chanzo cha Kwanza ili kutetea hoja yako kuwa hakuna Chanzo cha Kwanza?
Ulimwengu ulianza kuwepo lini?Safi sana, unapaswa kuuliza maswali yenye akili kama haya, ulimwengu wetu umeundwa na vitu vinavyobadilika, vinavyoanza na kuisha, kimantiki, kitu chochote ambacho hakina ulazima wa kuwepo hakiwezi kujitegemea chenyewe, lazima kitegemee kitu chenye ulazima wa kuwepo ambacho chenyewe hakina mwanzo wala mwisho.
Kama ulimwengu ungekuwa unajitegemea wenyewe, usingekuwa na mwanzo, usingekuwa na mabadiliko, na kusingekuwa na uharibifu wa nishati hii ni basic physics, unaijua?
Naona bado unakariri ule ule usemi wako wa Google bila kuelewa! Narudia kumuelewesha tena maana unaonekana una dondoo lakini huna uelewa, sheria ya mantiki haisemi kila kilichopo kina chanzo, inasema hivi kila kilichoanza kuwepo kina chanzo, ulimwengu una mwanzo kwahiyo unahitaji chanzo.
Hata Ulimwengu haujaanza kuwepo.Chanzo cha Kwanza hakijaanza kuwepo, kipo tangu milele, kwahiyo hakihitaji chanzo kingine, huu utofauti mdogo tu unakushinda kuelewa? Come on, use your brain.
Find someone of your league to parallel your mediocrity.It is only a fool who cares about puctuation
Nilisha kwambia ya kuwa wewe na wenzio mnajiifanya mna logic uchwara, wadanganyeni wengine na mimi nisione
I'll always point out your insignificant objectivity ya uchwara wa kukosoa dini