Je, Kulikuwa na Machafuko Kabla ya Mwanadamu?

Biblia imeanza kwa kusema hapo mwanzo(time) M-ngu aliziumba Mbingu(space) na Nchi(matter) sasa swali ni kuwa je kuna kiumbe chochote kinaishi nje ya hayo mambo matatu?
Kama jibu ni hapana basi hakukuwa na chochote hapo kabla ya mwanzo.
Upo sahihi pia,

Lakini nielewe hapa kwamba Mungu amekuwepo tangu enzi, hivyo ukuu na uwezo wake haukuanza na uwepo wetu wala hautaishia kwetu. Kwa hiyo, sioni ugumu kusema kwamba kabla yetu huenda kulikuwepo viumbe wengine. Vivyo hivyo, mwisho wa uwepo wetu haumaanishi mwisho wa uumbaji wa Mungu anaweza kuumba viumbe wengine hata baada yetu. Kwa mtazamo huo, tunaweza kusema kwamba kabla ya kizazi chetu huenda kulikuwepo viumbe zaidi, ingawa hili bado linabaki kuwa nadharia na si jambo lililothibitishwa.

Benoit sijui umepata picha nini najaribu kusema hapa ?
 
Debe tupu ni wewe zumbukuku.

Tabularasa.

Halfwit bastard.

Thibitisha kuna huyo unayemwita unmoved mover.

Sio kufosi imani zako uchwara ulizo aminishwa na kupumbazwa.

Ulimwengu ulianza kuwepo lini?

Hata Ulimwengu haujaanza kuwepo.

Umekuwepo milele.
Hoja huwa haiishi matusi ndugu

Guard your emotions endapo utaona umezidiwa omba ufafanuzi au nenda kajifunze zaidi
 
Debe tupu ni wewe zumbukuku.

Halfwit bastard.
Hahah relax mtoto mdogo.
Thibitisha kuna huyo unayemwita unamoved mover.

Sio kufosi imani zako uchwara ulizo aminishwa na kupumbazwa.
Unaposema imani uchwara unamaanisha Aristotle yule uliyemshupalia mwanzo kuwa unamjua alikuwa na imani uchwara? Baadae nikakuumbua ? Hahaha unafurahisha.
Ulimwengu ulianza kuwepo lini?
Hili swali lako ni la darasa la sita kabisa hahaha, sayansi kupitia setilaiti za Planck na WMAP ilishathibitisha kuwa ulimwengu ulianza takribani miaka bilioni 13.8 iliyopita, Google ipo mikononi mwako lakini bado unashindwa kuitumia kupata basic facts kama hizi? Pole sana kwa wajumbe wanaosoma hoja zako.
Hata Ulimwengu haujaanza kuwepo.

Umekuwepo milele.
Umeamua kuwa mchawi wa sayansi? Yaani unapingana na Edwin Hubble, Albert Einstein, Stephen Hawking, na maelfu ya wanasayansi wa Nasa?

Hueleweki hata upo upande gani maskini.
 
Upo sahihi pia,

Lakini nielewe hapa kwamba Mungu amekuwepo tangu enzi, hivyo ukuu na uwezo wake haukuanza na uwepo wetu wala hautaishia kwetu. Kwa hiyo, sioni ugumu kusema kwamba kabla yetu huenda kulikuwepo viumbe wengine. Vivyo hivyo, mwisho wa uwepo wetu haumaanishi mwisho wa uumbaji wa Mungu anaweza kuumba viumbe wengine hata baada yetu. Kwa mtazamo huo, tunaweza kusema kwamba kabla ya kizazi chetu huenda kulikuwepo viumbe zaidi, ingawa hili bado linabaki kuwa nadharia na si jambo lililothibitishwa.
Hoja yako ina mashiko mkuu.
Ni kweli Yeye yupo nje ya hayo mambo na uwezo wake haupimiki. Sasa basi kama kulikuwa na viumbe vingine hapo kabla ya mwanzo ni dhahiri kabisa viliishi nje ya physical realm na kwa maana hiyo havikuwa na impact yoyote kwa ulimwengu huu tunaoishi sisi maana ulimwengu huu unaishi ndani ya muda, maada na nafasi.
Mfano ni mtu akifa anaondoka katika katika mwili lakini roho yake itaishi milele ila haitakuwa na impact yoyote kwenye ulimwengu huu hadi tu itumie viumbe wengine wenye mwili.
Ninachowaza ni kuwa kama kungekuwa na viumbe viliishi katika physical realm hapo kabla basi biblia isingeanza na hapo mwanzo.
 
Hahah relax mtoto mdogo.
Kakojoe ulale.
Unaposema imani uchwara unamaanisha Aristotle yule uliyemshupalia mwanzo kuwa unamjua alikuwa na imani uchwara? Baadae nikakuumbua ? Hahaha unafurahisha.

Hili swali lako ni la darasa la sita kabisa hahaha, sayansi kupitia setilaiti za Planck na WMAP ilishathibitisha kuwa ulimwengu ulianza takribani miaka bilioni 13.8 iliyopita, Google ipo mikononi mwako lakini bado unashindwa kuitumia kupata basic facts kama hizi? Pole sana kwa wajumbe wanaosoma hoja zako.

Umeamua kuwa mchawi wa sayansi? Yaani unapingana na Edwin Hubble, Albert Einstein, Stephen Hawking, na maelfu ya wanasayansi wa Nasa?

Hueleweki hata upo upande gani maskini.
Rubbish🚮
 
Hoja yako ina mashiko mkuu.
Ni kweli Yeye yupo nje ya hayo mambo na uwezo wake haupimiki. Sasa basi kama kulikuwa na viumbe vingine hapo kabla ya mwanzo ni dhahiri kabisa viliishi nje ya physical realm na kwa maana hiyo havikuwa na impact yoyote kwa ulimwengu huu tunaoishi sisi maana ulimwengu huu unaishi ndani ya muda, maada na nafasi.
Mfano ni mtu akifa anaondoka katika katika mwili lakini roho yake itaishi milele ila haitakuwa na impact yoyote kwenye ulimwengu huu hadi tu itumie viumbe wengine wenye mwili.
Ninachowaza ni kuwa kama kungekuwa na viumbe viliishi katika physical realm hapo kabla basi biblia isingeanza na hapo mwanzo.
Nakupata mkuu. Lakini bado kuna maswali mengi ya kujiuliza Neno mwanzo si lazima limaanishe kwamba kila kitu kilianza kutoka kwenye kutokuwepo kabisa. Kwa mfano, tunaposema hapo mwanzo Mungu aliumba dunia tunaweza kujiuliza dunia iliundwa kutoka kwenye hali gani?

Kwa sababu kwenye maandiko inasema, tayari kuna giza na vilindi vya maji kabla ya uumbaji kuendelea. Hivyo, tunaweza kufikiria kwamba huenda kulikuwa na hali fulani iliyokuwepo kabla, kisha dunia ikachukua umbo tunalolijua kupitia mabadiliko au transformation ya uumbaji wa mungu.

Hii ni nadharia tu lakini inaacha nafasi ya kujiuliza kama dunia iliumbwa moja kwa moja kutoka kutokuwepo, au ilitokana na hali fulani iliyokuwepo awali.
 
Hao watu aliowaogopa Kaini walikuwa wadogo zake, punguza uvivu wa kusoma Mkuu.
Mkuu, kumuita mvivu hakuwezi kuwa msaada.
Ulitakiwa ulete vifungu vya Biblia vinavyo support hoja yako ila aweze kupata utambuzi.
 
Nakupata mkuu. Lakini bado kuna maswali mengi ya kujiuliza Neno mwanzo si lazima limaanishe kwamba kila kitu kilianza kutoka kwenye kutokuwepo kabisa. Kwa mfano, tunaposema hapo mwanzo Mungu aliumba dunia tunaweza kujiuliza dunia iliundwa kutoka kwenye hali gani?

Kwa sababu kwenye maandiko inasema, tayari kuna giza na vilindi vya maji kabla ya uumbaji kuendelea. Hivyo, tunaweza kufikiria kwamba huenda kulikuwa na hali fulani iliyokuwepo kabla, kisha dunia ikachukua umbo tunalolijua kupitia mabadiliko au transformation ya uumbaji wa mungu.

Hii ni nadharia tu lakini inaacha nafasi ya kujiuliza kama dunia iliumbwa moja kwa moja kutoka kutokuwepo, au ilitokana na hali fulani iliyokuwepo awali.
Very interesting mkuu
 
Kama Adamu na Hawa walikuwa chanzo cha wanadamu wote, basi
Kaini alimuoa mmoja wa binti za Adamu na Hawa—yaani dada yake.

Mungu alikuja kukataza hilo baadae kwenye walawi 18.
Huoni kwa maelezo hayo, unam portray Muumba kama kiumbe asiye na msimamo. Leo unaruhusu kitu X, kesho unapiga marufuku kitu X.
 
Mkuu, kumuita mvivu hakuwezi kuwa msaada.
Ulitakiwa ulete vifungu vya Biblia vinavyo support hoja yako ila aweze kupata utambuzi.
Nimezidi kumuelewesha huko mbele, utaona tu mkuu, endelea kusoma.
 
Huoni kwa maelezo hayo, unam portray Muumba kama kiumbe asiye na msimamo. Leo unaruhusu kitu X, kesho unapiga marufuku kitu X.
Logic ni ndogo tu hapa, hivi ukitaka kuanzisha kitu kikiwa absolute zero, sheria za kuanzia zinawezaje kufanana na sheria za kukiendesha kikiwa tayari kimeshakuwa kikubwa na kusambaa?
 
Very interesting mkuu
Ndio mkuu, Biblia ina mambo mengi yanayohitaji kutafakari kwa kina na kuunganisha matukio pamoja ili kupata picha kamili ndiyo maana wakati mwingine inahitaji na usaidizi wa nakala nyingine na vitabu tofauti.

Kwa mfano, kuhusu Shetani, Biblia haisemi kila kitu kuhusu asili yake kwa maelezo ya moja kwa moja Hivyo bado kuna maswali mengi yanayoweza kujiuliza kuhusu maandiko hayo na maana yake halisi.
 
Back
Top Bottom