Je, Kulikuwa na Machafuko Kabla ya Mwanadamu?

Je, Kulikuwa na Machafuko Kabla ya Mwanadamu?

Kiasili hadithi ya Lilith sio Biblia, kuna mada Mshana Jr alileta jukwaani kuhusu yeye, ina nyama nyama kidogo, kama ataona haya maoni itakuwa vizuri akiattach ukasome mule wadau wamejitahidi kwenda deep sana
Wewe ulivyosoma uliona kuna uhusiano wa Lilith na Adam?

Je, Biblia inasemaje kuhusu tofauti za skin colours miongoni mwa wanadamu ukizingatia kwamba wazazi wa kwanza walikuwa Adam na Eve kama kweli hiyo stori haina makandokando?
 
Kaini alioa dada zake ni sawa kabisa kwahyo hata hao aliowaogopa ni ndugu zake biblia inaangalia wahusika wakuu tu watukio husika
 
Wewe ulivyosoma uliona kuna uhusiano wa Lilith na Adam?

Je, Biblia inasemaje kuhusu tofauti za skin colours miongoni mwa wanadamu ukizingatia kwamba wazazi wa kwanza walikuwa Adam na Eve kama kweli hiyo stori haina makandokando?
Kumbuka ni vitabu 66 tu ndio vilijumuishwa kuunda Biblia, kitabu kama Enoko kimejitahidi kuchimba hayo yote kiundani, mimi si mwandishi mzuri lakini ikikupendeza tafuta Biblia ya kiorthodox kupata maarifa zaidi.

Unaweza pia kutafuta kitabu cha Jubilees kinawazungumzia vizuri sana Shem, Ham na Yafeth
 
Wapinzani wa RC ndio wanatumia 66
Wakatoliki miaka yote wanatumia vitabu 72 kama sio 73.

Ki msingi nina hiyo Bible version inayogusia habari za Lilith, ni vile tu sijajipa muda wa kuisoma kwa kina.
 
Kabla ya wanadamu dunia ilikaliwa na majini baada ya kufanya uharibifu mkubwa......ikasafishwa na kuletwa mwanadamu.

Qur’an inasema:
“Hakika Mimi nitaweka Khalifa katika ardhi.”
— Al-Baqarah 2:30

Quran.com
Malaika wakasema: “Je, utaweka humo atakayefanya uharibifu na kumwaga damu?”
Hapa wanazuoni wa tafsiri wameeleza namna kadhaa walivyoweza kujua kwamba kutakuwa na umwagaji damu. Maelezo mashuhuri katika baadhi ya tafsiri ni kwamba majini waliishi ardhini kabla ya Adam (A.S.), wakafanya uharibifu na kumwaga damu. Ibn Kathir ananukuu riwaya zinazosema hivyo.
Nyie wote mmechanganyikiwa 😁😁😁😁

Majini yalileta uharibifu mkubwa so ambacho hakifanyi binaadamu kuhusu huo uharibifu ni kipi binaadamu wanauana Kila kukicha

Hivyo vitabu vyenu vimewajaza upumbavu

Mfano mdogo tu ni vita ya crusade Ulaya huko watu walikuwa wanachinjwa kama kuku wanavyo chinjwa soko la manzese mahakama ya ndizi ,

So kama huyo mungu aliwaondoa hao majini duniani kisa walileta uharibifu halafu akawaleta binaadamu Akidhani kwamba hawato fanya uharibifu basi huyo mungu Akili Hana na hayupo maana hakuwa anajua kwamba hao binaadamu they're more than a worse thing

Mfano mdogo tu ni kile alicho kifanya Bi-msumi October 29 una kizungumziaje !?

Bado tu una yaamini hayo maandiko ya kutungwa !?

Ifikage Mahala muwe mnawaza
 
Na waswahili wakasema..

"Hakuna jipya chini ya Jua"

kwa akili yako fupi na ndogo kama punje ya haladali unaweza ukaunyambua huu msemo.

Apa hatuzungumzii siasa......Jikite kwenye mada
 
Kuna jambo la kuvutia sana katika Mwanzo 1:2 “Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu; na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji.” Aya hii inaweza kutufanya tujiulize swali ambalo mara nyingi tunalipita: nini kilitokea kabla ya hali hii ya ukiwa na utupu? Biblia haitoi maelezo ya moja kwa moja kwamba kulikuwa na vita au viumbe waliokuwa wakiishi duniani kabla ya mwanadamu, lakini ukitazama kwa jicho la udadisi, unaweza kujiuliza ikiwa kulikuwa na tukio fulani lililosababisha hali hiyo ya machafuko. Labda kulikuwa na mabadiliko makubwa, labda machafuko, au hata vita lakini haya ni mawazo ya kutafakari, si ukweli uliothibitishwa na maandiko.

Kama tunaruhusu akili ichunguze zaidi, tunaweza kujiuliza je, “ukiwa na utupu” ilikuwa hali ya mwanzo kabisa, au ilikuwa matokeo ya jambo lililotokea kabla ya simulizi kuanza? Mungu anaonekana kuleta nuru, mpangilio na uhai katika mazingira yaliyoelezwa kuwa na giza na vilindi vya maji. Hii inaweza kutufanya tufikirie uwezekano wa “reset” ya uumbaji si kwamba Biblia inasema Mungu alifanya reset baada ya vita, bali kama hypothesis ya kifalsafa. Huenda kulikuwa na historia ambayo haijaelezwa huenda hakuna kitu kilichokuwepo kabla yake. Pengo hilo ndilo linaloifanya akili iulize.
Mwanzo 1:2 haisemi moja kwa moja kwa nini nchi ilikuwa “ukiwa na utupu”; inaeleza tu hali iliyokuwepo wakati huo.

Kwa hiyo kuna tafsiri kuu mbili:

1. Tafsiri ya kawaida
Mwanzo 1:1–2 inaeleza mwanzo wa uumbaji, “ukiwa na utupu” ni hali ya Dunia kabla Mungu hajaiweka katika mpangilio.

2. Tafsiri ya “gap”
Baadhi ya wafasiri huona kunaweza kuwa na kipindi au tukio kati ya Mwanzo 1:1 na 1:2 yaani kitu kilitokea kabla ya Dunia kuonekana ikiwa ukiwa na utupu. Lakini hii ni tafsiri ya kitheolojia, si jambo ambalo Biblia inathibitisha wazi.

Neno la Kiebrania “tohu va-bohu” (תֹהוּ וָבֹהוּ), linalotafsiriwa “ukiwa na utupu,” linaweza kueleweka zaidi kama hali isiyo na mpangilio/haijawa tayari, si lazima Dunia iwe ilikuwa imeharibiwa baada ya tukio fulani.
 
Udadisi huu unaweza kuonekana hata katika simulizi la baadaye la Adamu, Hawa na Kaini. Baada ya Kaini kumuua Abeli, Kaini anaonekana kuwa na hofu kwamba “kila mtu atakayeniona ataniua,” na baadaye anaenda kuishi katika nchi nyingine na anapata mke. Hapo ndipo maswali yanapoanza: hao watu aliowaogopa walikuwa nani? Mke wa Kaini alitoka wapi? Na kizazi chake kilianzaje?
Biblia inaacha mapengo ya simulizi ambayo hayajaelezewa moja kwa moja. Na pale ambapo maandiko hayajasema, tunapaswa kutenganisha ukweli wa maandiko na tafsiri zetu.
 
Back
Top Bottom