John10
JF-Expert Member
- Aug 13, 2009
- 357
- 11
Mkuu Kibunago I have to say I agree with you. Tatizo la watu kama Sokomoko siyo kwamba wana advocate usawa wa dini zote bali wanacho lalamikia ni kujihisi (kwa sababu siyo fact) kwamba watu wa dini nyingine wapo juu zaidi. Kama kweli Sokomoko angekua ana advocate usawa asinge angalia tu Wakristo na Waislamu bali pia Singa Singa, Wapagani, Wahindu etc. Sasa yeye haoni hizi dini zingine lakini ana taka kutuaminisha kwamba yeye si mdini.
Pili, mimi namuona mtu ambae kafikia hatua ya kuhesabu watu wa dini gani wapo wangapi kwenye baraza ndiyo mdini. Wengi wetu tume kua tukiangalia kama walio wekwa wana faa au laa bila kuzingatia dini ila yeye kaamua kuangalia fulani ni wa dini gani bila hata kujua kwamba jina na dini ni vitu viwili tofauti.
Mimi nishamsoma huyu Sokomoko na watu wa design yake. Wanajua dini ni sensitive issue kwa hiyo wanajua jinsi ya kuprovoke. Huku katika jamii sijawahi kuona wala kusikia Waislamu au Wakristo wakilalamikia uwepo wa udini ila ni humu JF ndiyo una sikia story zote hizi. Mtu ambae haja wahi kukanyaga Tanzania akisoma baadhi ya post humu anaweza akafikiria Tanzania haku kaliki kumbe that is far from the truth.
Dawa nzuri ya kukomesha watu kama hawa ni kuto kujibu post zao kabisa kwa maana mtu mmoja akijibu tu basi mtiririko wa pumba unaanza. Tanzania hamna such thing as udini. Tatizo ni wale wachache ambao kwenye kila ngazi wana taka kuangalia nani ana tokea dini fulani tena siyo hata dini zote bali dini mbili tu na bado mtu ana jiita si mdini.
Mwisho ningependa kuwauliza swali wanaJF. Je kati ya hawa mdini ni nani? Yule anayempinga mtu kutokana na dini yake au yule anayemtetea mtu kutokana na dini yake? Maana humu JF kuna members wana tetea watu kwa ajili wao ni dini moja lakini bado wana nguvu za kuita watu ambao wanampinga huyo mtu kutokana na dini yake kuwa ni mdini. Wote ni wale wale tu!
Unapopinga kwamba TZ hakuna Udini ni kubisha ukweli halisi uliokuwepo TZ. Udini/Mdini ni yule mtu anaeajiri watu, anawabagua watu, anawatukana watu, kwa sababu ya dini zao nk, (Biases). Sasa tuangalie statistic za hizi biases kama kweli zipo TZ.
Tuangalie ktk serikali yetu je ina diversity yoyote? Mfano nchi kama Marekani ina Affirmative action ili kuwapa na nafasi minority ktk serikali, mashuleni.
Sasa ukiangalia vitu kama hivyo basi utaona kwamba serikali yetu haina diversity yoyote ktk serikali; kwa sababu kuna watu wanapeana kazi kwa kujuana na nk. Njia ambayo itaweza kuisadia TZ ktk balaa la vita vya kidini ni kuandaa sheria maalum ya kuwapa watu ruhusa ya kuangalia mfumo mzima wa diversity za kidini ktk kazi serikalini, biashara nk.
Wewe angalia hii Jamii Forum, wanasema kwamba inaendeshwa as secular, lakini inapromote Injili- sasa ni kweli hii JF inaendeshwa as secular? Sasa kama secular mbona kuna Injili tu peke yake? Hivyo ndivyo vitu ambavyo vipo ktk serikali yetu. Serikali inasema haina Udini, lakini action inazofanya zipo ktk biases za kidini.