Kuna jambo ambalo huwa nashindwa kuelewa kwanini watu wanasoma halafu hawatafakari mambo kisayansi. Dini na haswa katika nchi kama Tanzania siyo kitu cha kuringia. Kwanza kabisa hakuna aliye na uthibitisho kuwa dini yake ni bora kuliko nyingine. Pili sidhani kwamba kuna didni inayofundisha (kutoka maandishi ya mitume) kuwa umchukie mwenzako, jirani yako, kuikashifu dini yake, kuidharau dini yake, kujenga chuki hadi kumtoa roho kwa sababu ni dini tofauti na yako. Baada ya kusema hayo sidhani kuwa anayeweza kuandika kashfa kwa dini nyingine anaifahamu dini yake vyema. Anajifanya tu na ni kibaraka wa watu wenye kutafuta watu walio na akili nyepesi kufuata matakwa yao tena kwa kudanganywa na pesa kidogo tu. Ni jambo la kusikitisha kuwa hatufiki mahali tukakubali kuwa hata kama dini moja katika nchi na haswa kama Tanzania kuizidi dini nyingine hilo siyo jambo la kuanzia mipango ya uadui. Badala yake ingekuwa ni changamoto ili kila mwenye dini ya kweli rohoni ajitahidi kuingia kwenye ushindani kielimu na kiuchumi ili kuyamudu maisha na bila kulewa chuki na jirani yake. Dini, mtu hukaa nayo moyoni mwake ikifanya kazi ndani yake na matendo yake ndiyo yanayoonyesha kitu au hazina aliyo nayo moyoni mwake. Na jamii iliyomzunguka hutambua hilo kirahisi kabisa.
Jambo la muhimu kujiuliza ni je huoni kuwa ulizaliwa huna dini yoyote na ungeweza kuwa dini yoyote wakati unalelewa na wale waliokulea? Au waliokuelimisha?? Sasa iweje leo hii imechukua hata jukumu la kuikashifu dini ya jirani yako? Mtu yeyote mwenye akili timamu aliyeelimika na hswa Mtanzania anatakiwa kuelewa kuwa udini hauna nafasi dunia ya leo na tunaomba aliye na hisia hizo ajifunze na kuacha mara moja kupima wenzake kwa vigezo vya aina hiyo. Ajipime yeye mwenyewe kwanza na ajielimishe kistaarabu. Halafu arudi atuandikie mambo mema zaidi hapa JF. Hatuna muda mwingi wa kupoteza!