Je Kikwete ni mdini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je Kikwete ni mdini?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Sokomoko, Dec 3, 2010.

 1. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #1
  Dec 3, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mods, na wana JF,

  Haitakuwa busara kwa thread hii kuipeleka sehemu ya dini, inajulikana sehemu hiyo haifikiwi na watu wengi hapa JF ikiwa mimi mmoja wapo.

  Ni matumaini yangu kuweza kuiaccess hii thread na kuona mijadala ikichangiwa ili kuweza kujua ukweli.


  Sitegemei kuwa JF/Mods wapo kwa ajili ya kuchochea chuki dhidi ya Serikali iliyopo madarakani kwani kama itakuwa ni hivyo basi wanafanya jambo la hatari sana linaloweza kutugharimu. Tumeona ile thread ya OIC ikiachiwa kuchangiwa na kila mtu na mwenye kila tusi dhidi ya dini ya kiisamu na kejeli akiachiwa kwa marefu na mapana. Kwahiyo sioni sababu ya hii thread ya kisiasa zaidi kutupiwa huko kusikojulikana.


  Mwisho napenda kutoa angalizo:

  Sio haki kuhamisha thread ya mtu na kuipeleka sehemu asiyokuwa na access nayo. Hapa JF ni sehemu ya kutoa mawazo na kila mmoja aheshimiwe mawazo yake na sio kufungwa na kutupwa kapuni.

  Kuna tetesi Zimeenea mtaani kuwa baada ya JK kuingia madarakani aligomea ruzuku iliyokuwa ikitolewa na Serikali kuendesha makanisa pamoja na taasisi zinazoendeshwa na makanisa katoliki nchini kama shule, hospitali na vyuo. "The Government shall provide financial assistance to Church institutions and shall seek financial assistance to Church run social services in its bilateral negotiations with foreign governments"

  source
  :The Memorandum of Understanding between the Government of the United Republic of Tanzania and the Tanzania Episcopal Council (TEC) and the Christian Council of Tanzania-page 3 (attached herewith)

  Nasikia JK aliwaambia kuwa nchi hii haina dini na itakuwa ubaguzi kuwapa ruzuku watu wa dini moja na kuwaacha wa dini nyinginezo akatolea mfano kuna waislam, wabudda, masingasinga, wahindu na wasiokuwa na dini je hao hawana haki ya kupewa ruzuku? na serikali ikitoa ruzuku kwa hawa wote itawezaje kujiendesha? Basi bora mkose wote. Hapo naona JK aliona mbali sana ila hakujua kama anajiharibia yeye na chama chake. Na ndio maana kwa kutumia mlango wa nyuma kuna chama kikasimamisha watumishi wa Mungu kwa wingi na kufanikiwa kupenya kila pembe ya Tanzania. Inasemekana Kanisa liliplay part kubwa kwa mafanikio ya chama fulani. Na hizo zilikuwa ni hasira za watumishi wa kanisa.

  KUNA TETESI KUWA WAFUATILIAJI WA MAMBO WAMEITHIBITISHIA SERIKALI UBADHIRIFU MKUBWA WA RUZUKU ILIYOKUWA INATOLEWA NA SERIKALI SAMBAMBA NA MISAMAHA YA KODI. MISAMAHA HII YA KODI NI ILE YA UAGIZWAJI MAGARI NA VITU MBALIMBALI KUPITIA TRUSTEES ZA MAKANISA. NA TANGU KUANZA KUBANWA KUMEKUWA NA UAIGIZAJI WA VITU MDOGO TOFAUTI NA HAPO MWANZO, MAANA INASEMEKANA WAJANJA WALIKUWA WANATUMIA MWANYA HUO KUJINUFAISHA.

  Ukiunganisha picha itaona hapo ndio chanzo hasa cha timbwili hili mnaloliona leo lililo vikwa ngozi ya vyama vya siasa ( upinzani ). Hapo awali Wakristo na CCM walikuwa chanda na pete. Ilikuwa ni kosa la jinai kwa mkristo mwenye imani kuwa upinzani ndio maana hata viongozi wao wengi mwaka 2005 walisema JK "chaguo la Mungu"

  Leo hii ukitia pua tu JF na maeneo mengi kwenye mitandao na mitaani utakutana na shutuma kuwa JK ni Mdini, lakini hawatoi facts za udini wake.

  Je, JK ni mdini?

  Orodha ya Baraza la Mawaziri na Manaibu wa Wizara 26 za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 2010 - 2015

  1. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utawala Bora - Mathias Chikawe (Mkristo)
  2. Waziri wa Nchi, Oisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu - Steven Wassira (Mkristo)
  3. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma - Hawa Ghasia
  4. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Waziri wa Muungano - Samia Suluhu Hassan
  5. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Waziri wa Mazingira - Dk. Terezya Luoga-Hovisa (Mkristo)
  6. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Waziri wa Sera, Uratibu na Bunge - William Lukuvi (Mkristo)
  7. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji - Mary Nagu (Mkristo)
  8. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - George Mkuchika (Mkristo)
  9. Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (i) - Aggrey Mwanri (Mkristo)
  10. Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (ii)Kassim Majaliwa -
  11. Waziri Wizara ya Fedha - Mustapha Mkullo
  12. Naibu Waziri Wizara ya Fedha (i) - Gregory Teu (Mkristo)
  13. Naibu Waziri Wizara ya Fedha (ii) - Pereira Ame Silima
  14. Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi - Shamsi Vuai Nahodha
  15. Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi - Balozi Khamis Suedi Kagasheki
  16. Waziri wa Katiba na Sheria - Selina Kombani (Mkristo)
  17. Waziri Wizara ya Mambo ya Nje - Bernard Membe (Mkristo)
  18. Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje - Mahadhi Juma Mahadhi
  19. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa - Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi
  20. Waziri Wizara yaMaendeleo ya Mifungo - Dk. Mathayo David Mathayo (Mkristo)
  21. Naibu Waziri Wizara ya Maendeleo ya Mifungo - Benedict Ole Nangoro (Mkristo)
  22. Waziri Wizara ya Mawasiliano Sayansi ya Teknolojia - Profesa Makame Mnyaa M'barawa
  23. Naibu Waziri Wizara ya Mawasiliano Sayansi ya Teknolojia - Charles Kitwanga(almaaruf Mawe Matatu) (Mkristo)
  24. Waziri Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi - Profesa Anna Kajumulo-Tibaijuka (Mkristo)
  25. Naibu Waziri Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi - Goodluck Ole Medeye (Mkristo)
  26. Waziri Wizara ya Maliasili na Utalii - Ezekiel Maige (Mkristo)
  27. Waziri Wizara ya Nishati na Madini - William Mghanga Ngeleja (Mkristo)
  28. Naibu Waziri Wizara ya Nishati na Madini - Adam Kighoma Ali Malima
  29. Waziri Wizara ya wa Ujenzi (Barabara na Viwanja vya Ndege) - Dk. John Pombe Magufuli (Mkristo)
  30. Naibu Waziri Waziri Wizara ya wa Ujenzi - Dk. Harrison Mwakyembe (Mkristo)
  31. Waziri Wizara ya Uchukuzi - (Reli, Bandari, Usafiri wa Majini) - Omary Nundu
  32. Naibu Waziri Wizara ya Uchukuzi - Athuman Mfutakamba
  33. Waziri Wizara ya Viwanda na Biashara -Dk. Cyril Chami (Mkristo)
  34. Naibu Waziri Wizara ya Viwanda na Biashara - Lazaro Nyalandu (Mkristo)
  35. Waziri Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi - Dk. Shukuru Kawambwa (Mkristo)
  36. Naibu Waziri Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi - Philipo Mulugo (Mkristo)
  37. Waziri Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii - Dk. Haji Hussein Mpanda
  38. Naibu Waziri Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii - Dk. Lucy Nkya (Mkristo)
  39. Waziri Wizara ya Kazi na Ajira - Gaudensia Kabaka (Mkristo)
  40. Naibu Waziri Wizara ya Kazi na Ajira - Dk. Makongoro Mahanga (Mkristo)
  41. Waziri Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto - Sophia Simba
  42. Naibu Waziri Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto - Umi Ali Mwalimu
  43. Waziri Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo - Emmanuel John Nchimbi (Mkristo)
  44. Naibu Waziri Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo - Dk. Fenela Mukangala (Mkristo)
  45. Waziri Wizara ya Ushirikiano Afrika Mashariki - Samuel John Sitta (Mkristo)
  46. Naibu Waziri Wizara ya Ushirikiano Afrika Mashariki - Abdallah Juma Abdallah
  47. Waziri Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika - Profesa Jumanne Maghembe
  48. Naibu Waziri Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika - Christopher Chizza (Mkristo)
  49. Waziri Wizara ya Maji - Profesa Mark James Mwandosya (Mkristo)
  50. Naibu Waziri Wizara ya Maji - Gerson Lwinge (Mkristo)
  Jumla yote ni 50 kati yao wakristo 32 na waislam 18.

  Wakristo 64%
  Waislam 36%

  Ukiangalia wakuu wa mikoa na wilaya utaona wakristo ni wengi zaidi ya waislam sasa sijui na sifahamu huo udini wa JK upo wapi???

  Mwenye data tafadhali azilete jamvini.


  Kuna habari za hivi punde ni kuwa kuna makampuni zaidi ya 80 ya clearing and forwarding yamefungiwa kwa sababu mbalimbali kubwa hasa ubabu mashi. Inajulikana kwenye sekta hii watu wa kutoka mkoa fulani wameishikilia kwa asilimia zaidi ya 80. Inasemekana sifa ya watu wanaotoka huko ni ujanja mwingi na ni wakwepaji wakubwa wa kodi na walitumia vizuri sana nafasi ya kuwa na udugu kuanzia uwaziri mpaka kamishna wakati wa Che Nkapa.

  Ushauri kwa JK, Mkuu wee endelea kukaza buti watu walipe kodi kwa manufaa ya nchi usijali tunakusapoti kwa maana hawana shukrani Serikali imewaachia wamekula sana kodi kupitia ukwepaji na misamaha hewa lakini wamekuwa mbele kunyea kambi.
   
 2. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #2
  Dec 3, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  4th time unapost the same post UNATAKA BAN?
   
 3. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #3
  Dec 3, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Please do the needful.it is monotonous now
   
 4. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #4
  Dec 3, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mods wanazifuta nadhani kuna kaukweli fulani.
   
 5. AK-47

  AK-47 JF-Expert Member

  #5
  Dec 3, 2010
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Anayeuliza swali anajua zaidi kuliko tunaoulizwa
   
 6. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #6
  Dec 3, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Huyu jamaa ni wakuwekwa kwenye Recycle Bin! Hana fikira zaidi ya ujinga wake na pumba kila siku na habari wanazoziongea kwenye Madrasa al sul
   
 7. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #7
  Dec 3, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mod shoul do the needful to you wait and see
   
 8. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #8
  Dec 3, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Ukiona thread inapelekwa haraka haraka kwenye jukwaa la dini ujuwe wenyewe hawajipenda, na pili kidogo wamekuheshimu otherwise wangeifutilia mbali... pole sana mkuu!
   
 9. Simba Mangu

  Simba Mangu JF-Expert Member

  #9
  Dec 3, 2010
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 351
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  sokomoko Jambo mwanetu, tangu nimekuwa mwanachama wa jf family nimeona post zako nyingi ni za kichokonozi zaidi mijadala yenye manufaa kwa nchi na wananchi,pili kama kuna huo mkataba kati ya wakiristo na serikali sio shida na je? huyu jakaya unayemsemea leo kasomeshwa na nani? sio hawo wakiristo? Je kuna taasisi ya muslim youth wanacho kifanya nisawa? je kwa mwali pekee ndiko kwaliwa? kwa kungungwi je?
   
 10. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #10
  Dec 3, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Will see ikiwa OIC imewekwa kina mtu analijadili na nisuala linalohusu uislam aliepost hakufungiwa basi siku za JF zinahesabika mjue kuna watu wengi wanaifatilia na kujua ukweli na sitatofautisha JF na Ze utamu.
   
 11. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #11
  Dec 3, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Waislam walikuwa na taasisi nyingi na shule nyingi sana tanzania nzima ( Tambaza, Azania, Dodoma Secondary) muulize mhe Hashim Saggaf au Sango Kipozi walisoma Dodoma Secondary ilikuwa shule ya nani. Shule hizi zilikuwa classic. shule hizi zilitaifishwa na serikali na mpaka leo hii zipo chini ya serikali huku serikali ikiwacha kanisa likichanuwa. Ni kweli lakini Kikwete angepata fursa ya kusoma ingekuwa taasisi za kiislamu zingepewa fursa sawa na za kiroma.

  Nyumba nyingi za NHC ni za waislamu zilitaifishwa enzi za uhujumu uchumi ili kukwamisha maendeleo ya waislam ukizungumza ukweli wewe mdini mnataka waislam wakubali kuimba mapambia wakiingia kwenye ofisi za umma maana kuna vinanda vinalia kila ofisi ya serikali na mauwa ya chrismass acheni hizo chuki. Waislam walishakubali siku nyingi ila nyie mnachokonoa waseme...
   
 12. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #12
  Dec 3, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Bange hizi!
   
 13. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #13
  Dec 3, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135

  Wamezifuta kama tatu hivi walivyo ona I keep on posting them wakanijulisha kuwa wanaihamisha kwenye dini. So hiyo heshima unayosema haikufanyika kwanza imefanyika at the end na wanafurahi waislam kutukanwa kwenye ile thread ya kidini ya OIC. Anyway wao ndio wameshika mpini.
   
 14. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #14
  Dec 3, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,855
  Likes Received: 11,977
  Trophy Points: 280
  Tutolee udini wako usio na mbele wala nyuma badala ya kufikiria maendeleo unakazana kupost mambo ya udini utakufa nao ukitaka ondoka Tanzania hamia saudia.
   
 15. S

  Silas A.K JF-Expert Member

  #15
  Dec 3, 2010
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 807
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Wewe sokomoko una akili sawasawa? mbona kama akili yako yote imejaa udini tu! jitahidi ushughulikie mikakati ya kuwasaidia waislamu kielimu na maendeleo kwa ujumla badala ya kulia lia na mambo ya udini hapa.

  Wakati mwingine mnapenda kulalamika hata visivyohusika.
   
 16. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #16
  Dec 3, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Summarize hoja yako.
   
 17. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #17
  Dec 3, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Wenzake wanawaza maendeleo yeye yuko busy na Madarasa.
   
 18. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #18
  Dec 3, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Ukiwapa ukweli wanakimbilia propaganda za kusema kuwa Waislam hawajasoma... Wakati mwingine utasikia ooh nendeni shule kwanza! Propanda zimewachukuwa kiasi wanajiona kuwa wao ndio wasomi peke yao...!
   
 19. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #19
  Dec 3, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,855
  Likes Received: 11,977
  Trophy Points: 280
  Wenzake wanakwenda shule za maana yeye ameng'ang'ania kuwa mwalimu wa madrasa ukimuuliza kamaliza level gani atakuambia alimaliza form 2 kinondoni muslim sec.
   
 20. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #20
  Dec 3, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Acha inferiority complex..wewe na wenzako kama mliona usilamu unatukanwa mlibonyeza kitufe kuwaambia MODS? Mliwaarifu wakakataa kurekebisha ? Sasa kama hamkufanya hivyo kuwalaumu MODS waonekane kama ni maadui wa Usilamu huoni kama ni kuleta mfarakano? Kama wewe na wenzako mnaona JF inapinga usilamu, tangia muanze kulalamika mbona bado mpo? Nyie ni wanafiki wakubwa na ningekuwa MOD mngechezea server ban nyote nyie.
   
Loading...