Je, JWTZ linaruhusiwa kisheria kufanya msako kwenye nyumba za watu Tanzania?

mmaroroi

JF-Expert Member
May 8, 2008
2,960
544
Hivi karibuni kumekuwa na taarifa ya JWTZ kusema litafanya msako kwenye nyumba za wananchi kutafuta wenye mavazi yanayofanana na za kwako. JWTZ hawajasema kama kuna mali zao zilizoibwa, hivyo hizo wanazotaka kutafuta ni za nani?

Kama kuna yanayomilikiwa na watu yanayofanana na za kwako, nani aliruhusu kuingizwa nchini na kuuzwa? Je, JWTZ hawana kazi ya kufanya hadi kutamani kufanya kazi ya Polisi?

Je, nchini yetu imetangaza hali ya hatari? Je, kwanini ukiukwaji wa sheria unaonekana kufurahiwa Tanzania? Tujadiliane kuhusu hili na kuona nini cha kuishauri serikali yetu sikivu. Wanasheria mtusaidie kuhusu hili. Nawasili.
 
Kisheria, wanaotakiwa kufanya msako ni polisi, unless otherwise, itangazwe nchi iko kwenye hali ya hatari.Hata hivyo, nashauri mipaka I ngelindwa vema, ili mavazi yasiyotakiwa ndani ya nchi kisheria, yasiingizwe.Sasa kwasababu inasemekana mavazi yameingia ndani ya nchi (ingawa sijui yameingiaje, ilhali huwa tunaaminishwa kua mipaka hulindwa usiku na mchana), basi wizara ya mambo ya ndani, kupitia jeshi la polisi, nadhani ndiyo wana jukumu la kufanya upekuzi. Wanaojua kwa usahihi zaidi,watatiririka.
 
Kuna uzi humu unasema hivi sasa jeshi letu limeacha majukumu yake ya msingi na kuingia kwenye biashara, mfano kuna kituo cha kuuza mafuta Ubena Zomozi kinaitwa Air wing kama siyo Air force, kuna Mzinga wana kumbi za mikutano na sherehe na accomodation, kuna wengine wanafyatua matofari ya cement, wengine wanashika kandarasi za kujenga majumba nk
 
Najua ilikuwa hamasa na kama tishio ili watu warudishe nguo zinazofanana na combat yao. Wenzetu wanajua mengi ya kiusalama kuliko sisi. Lakini kusaka nyumba hadi nyumba hilo siyo rahisi kulifanya maana watajivunjia heshima yao iliyotengenezwa kwa muda mrefu na kwakweli JWTZ bado inaheshimika na kuaminika sana kutokana na kazi nzuri za kulinda taifa wanazozifanya. Mungu awabariki sana.
 
Kuna uzi humu unasema hivi sasa jeshi letu limeacha majukumu yake ya msingi na kuingia kwenye biashara, mfano kuna kituo cha kuuza mafuta Ubena Zomozi kinaitwa Air wing kama siyo Air force, kuna Mzinga wana kumbi za mikutano na sherehe na accomodation, kuna wengine wanafyatua matofari ya cement, wengine wanashika kandarasi za kujenga majumba nk
Hizo ni Kazi za jeshi wakati wa amani brother hawawezi kaa wasubiri budget ya serikali ambayo sio tosherevu katika sector nyingi nchini
 
Out the box:nini kimewafanya wacharuke sana kukusanya nguo zinazofanana na za jeshi?
Lakini pia humu JF kuna nyuzi zinadai kusini baadhi ya "sehemu" kunawaka "moto" na "wajomba" baadhi wamepata "pelesu pelesu".

Je kuna uhusiano wowote ktk hayo mambo?
LABDA "wazee wa takbiiiir" mamekua wakitumia sare zinazofanana/au zao kabisa kufanya "infitration" au "ambush" kwa "wajomba"
 
Haya mambo yanakuzwa sana tofauti na uhalisia.

Nitaamini kama kuna mtu ataleta ushahidi hapa kuwa wamegonga mlango kwenye mji wake ili wahakiki kama kwenye kabati lake kuna nguo za jeshi au zinazofanania.
 
Back
Top Bottom