Je, ulinzi shirikishi ni biashara haramu?

MWAISEMBA CR

Member
Apr 21, 2014
86
78
✳️JE ULINZI SHIRIKISHI NI BIASHARA HARAMU!?

🔜JE, NI NANI MWAJIRI WA HAWA POLISI JAMII, NA JE WAPO KISHERIA NA MAFUNZO YAO WAMEYATOA WAPI!?

🔜KWANINI WANANCHI TULIPIE ULINZI SHIRIKISHI WAKATI TUNALIPA KODI!?

🔜NA IKIWA TUNALIPIA, JE POLISI JAMII WATAWAJIBIKA KUTULIPA FIDIA IKIWA WAMESHINDWA KUDHIBITI UHARIFU KATIKA JAMIII!?

Moja ya mambo ya msingi ambayo kama jamii tunatakiwa tuwe makini na tuyahoji kwa ukaribu ni maswala yanayohusu USALAMA WA RAIA NA MALI ZAO PAMOJA NA UHALIFU UNAOTOKEA KATIKA JAMII ZETU ambao kwa msingi wa sheria zetu kwa sasa upo chini ya Jeshi la Polisi ingawa nao wamelirudisha kwa wananchi kwa kuanzisha hivi vikundi vinavyoitwa POLISI JAMII AU POLISI KATA ambao kazi yao mojawapo ni ULINZI SHIRIKISHI unaofanyika katika kila kata na vitongoji wakiwa nia nzuri tu kwamba POLISI KUFANYA KAZI NA WANANCHI KWA PAMOJA

Nimelifualia swala hili, na kutokana na ufahamu wangu mdogo nimeanza kujiuliza maswali kadhaa ambayo nadhanii bado sijayapatia majibu sahihi na ya kuridhisha

SWALI 1️⃣ : Hawa Polisi jamii Ni akina nani ? Ni Polisi waliofuzu mafunzo ya upolisi au Ni wananchi wanaofanya kazi za upolisi katika jamii zao kusaidia Polisi!?

Kama sio mapolisi bali ni mwananchi, basi nani ni mwajiri wao ?Kama wameajiriwa na Serikali au kusaidia Polisi basi walipwe na polisi au serikali yenyewe. Kama ni Wananchi tu wanaoisaidia polisi, Kwanini wanadai walipwe pesa za ulinzi shirikishi kutoka katika kila kaya ya nyumba ikiwa wananchi tayari wanalipa kodi za nyumba kwa serikali?

🔜Je hawa Polisi wa Tanzania kazi yao itakuwa nini!? Haiwezekani Polisi walipwe Mishahara kwa kodi za wanachi ila majukumu yao wanawaachia Wananchi(Polisi jamii) ili wafanye doria mtaa kwa mtaa tena usiku bila kuwa na mafunzo yeyote ya Kujiami!?Hivi hii ni sahihi!?

SWALI 2️⃣: Je, kama wananchi tutajihakikishiaje kuwa na Usalama wa mali zetu katika jamii zetu ikiwa tunalindwa na Polisi Jamii wasio na mafunzo maalum ya Ulinzi au ya upolisi wala wasio na silaha maalum za kujiami za Ulinzi wa kufanya doria katika mitaa na kata zetu!?

Na je wana uhalali gani kisheria na kiutendaji kazi na wanapatikanaje hadi kuingia kufanya kazi ya ulinzi wa raia na mali zao❓Tusije tukawa tuingiza Vibaka au Wezi waliohalalishwa!!!?

Ni kweli wengine wataniambia kuwa dhana ya ulinzi Ni kwa mujibu wa sheria na katiba ambapo, ibara ya 145 na 146 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 Inaeleza Katika majukumu ya Serikali za mitaa , watu wanapaswa kushiriki katika shughuli zote za maendeleo ikiwemo kutekeleza sheria ya ulinzi na usalama katika maeneo yao.

Lakini Je,UTEKELEZAJI WA SHERIA YA ULINZI NA USALAMA KATIKA MAENEO YAO KAMA INAVYOTAKA KATIBA , NI PAMOJA NA WAO KUFANYA KAZI ZA UPOLISI WA MOJA KWA MOJA KWA KUINGIA MSTARI WA MBELE KULINDA MITAA YETU KWA NIABA YA POLISI!?

Dhana ya ulinzi shirikishi ni nzuri sana ikiwa kweli wananchi watashirikiana na mapolisi kuhakikisha wanatokomeza uharifu mitaani kwa kutoa taarifa katika serikali zao za mitaa au kwa mapolisi pale viashiria vinapojitokeza ila dhana hiyo ya ulinzi shirikishi inaweza kuwa hatarishi ikiwa wananchi wasio na mafunzo wala viapo , ndio wanapewa mzigo huu mkubwa na kuaminiwa na jeshi la polisi kwa kufanya doria za ulinzi na za kupambana na waarifu mitaani kwa kupatiwa silaha duni kama torchi, virungu, mapanga na kupewa vitendea kazi vingine kama mabuti, makoti ya baridi ,reflecta.

🔜VIPI IKIWA HAO POLISI JAMII NDIO WAKAGEUKA KUONGOZA KUFANYA UHARIFU KATIKA JAMII WAKISHIRIKIANA NA MAJAMBAZI WA NJE!?
🔜Je hivi ikitokea wanakutana na majambazi wakubwa wanaojua kutumia silaha wataweza kupambana nao!? Au mmewapa kinga gani ya usalama wa maisha yao?
🔜 JE Kufanya hivi Sio kuhatarisha Usalama wa Vijana wetu na wananchi hao wanaojitolea kufanya kazi za Upolisi!?

SWALI 3️⃣: Je Uwajibikaji wa hao Polisi jamii upo kwa nani?Ikiwa wanalipwa Pesa za ulinzi shirikishi maanake tumefanya mkataba nao wa kutulinda, Je watawajibikaje ikiwa wameshindwa kutulinda au kusababisha hasara kubwa za mali za raia kama wizi au uharifu wowote unapotokea kwa uzembe wao?Je kuna fidia yeyote ambayo wao watapaswa kuturejeshea baada ya kushindwa kazi hiyo ya ulinzi kwa aliyepoteza mali hizo!?

⚠️NOTE: Kuna By law ambazo sasa hivi zinatumika ambapo usipochangia Pesa ya Ulinzi shirikishi kwa namna yeyote unapelekwa Polisi na faini yake ni Tsh 300,000.

🔜Je kama wananchi tunakuwa na uhakika gani kuwa sio hawa polisi jamii ndio wanaohusika katika matukio yetu mtaani? maana zipo tuhuma kadhaa kwa jamii dhidi ya hawa polisi jamii na ukingatia watendaji wake weng,i wengine ni vijana tu waliokuwa vijiweni tu hawana kazi maalum za kufanya

🔜Je tujiweke kwenye hatari hii na kutegemea hawa Polisi jamii ndio wawe walinzi wetu?

USHAURI WANGU KWA JESHI LA POLISI NA SERIKALI KUTOKANA NA UFAHAMU WANGU MDOGO

🅰️ Iachane na hii BIASHARA HARAMU YA KUTUMIA POLISI JAMII kufanya ulinzi shirikishi kwa namna hiyo bali kama serikali ikiwa ina uwezo basi inapaswa kuajiri Polisi wa kutosha wenye mafunzo maalum na kuwasambaza katika kila mitaa kufanya doria kwa namna hiyo hiyo wanavyofanya hao polisi jamii

Kumbuka kwa Tanzania yetu inakadiriwa tuna polisi elfu 40 na ushee ambapo kwa wastani Polisi mmoja wa Tanzania anahudumia watu 1000.Hivyo ikiwa Serikali itafanikiwa kuongeza kuajiri idadi ya Polisi nchini wa kutosha hata kufikia viwango vya kimataifa ambayo polisi mmoja ana uwezo wa kuhudumia watu 400 basi tutafanikiwa kwa sehemu kubwa kupunguza wimbi hilo la uharifu mitaani sio kuhamisha majukumu na kuwapatia wananchi

Jeshi la Polisi kuwaruhusu Polisi jamii kufanya kazi linawaweka hatarini raia wake kwa kuwapa majukumu ya kipolisi makubwa ya kiulinzi raia wasio na mafunzo hivyo inaweza kusababisha mauji makubwa pindi watakapokutana majambazi wenye silaha kubwa na ni moja ya jambo la hatari walilowahi kulianzisha ambalo litatengeneza hatari kubwa zaidi hapo mbeleni kama hawataliangalia kwa umakini na kutafuta namna nzuri ya utoaji taarifa za uharifu katika ufanyaji kazi wa ulinzi shirikishi ,na kesi zinaweza kuongezeka zaidi ikiwa tu, watatokea polisi jamii ambao wameaminiwa ila wao sio waaminifu wakaongoza magege ya kufanya uhalifu .

Kazi ya Ulinzi shirikishi umekuwa ni mradi wa Serikali za mtaa kuongeza mapato yao ambao unazidi kuwaongezea wananchi wa kipato cha chini mzigo mkubwa wa kodi mbalimbali wanazozilipia Mfano Pesa ya takataka, Ulinzi shirikishi, kodi ya majengo,bili za maji, bill za umeme n.k Je kweli tulipie ulinzi shirikishi wakati Polisi wapo na tunawalipa kwa kodi zetu?

🅱️Kutokana na kuwepo ulazima na Umuhimu wa kufanya ulinzi shirikishi basi nashauri Serikali au Jeshi la Polisi hata itumie Makampuni ya Ulinzi yenye askari ambao waliokwisha pitia mafunzo mbalimbali ya kiulinzi ndio washirikiane na polisi pamoja na wananchi katika kufanya doria mtaa kwa mtaa wakati wa usiku ili kupunguza uharifu unaojitokeza kuliko kuendelea kuwatumia wananchi(Polisi jamii) moja kwa moja ambao hawana sifa zinazohitajika kuingiq mstari wa mbele mtaani

Ikiwa tutatumia makampuni hayo ya ulinzi yaliyopo na yaliyosajiriwa ni rahisi yakalipwa hata pesa hizo hizo zinazotolewa katika kila kaya na pia ni rahisi kuwawajibisha ikiwa hawatafanya ulinzi ipasavyo.Hii itapunguza risk kubwa ambayo inaweza ikatokea kwa kuwatumia wananchi wasio na maarifa ya kazi za ulinzi....

....Pia natambua juhudi kubwa na kazi kubwa ambayo pia hata sasa kwa sehemu hawa Polisi wamesaidia kuleta hofu katika jamii ambayo imepunguza kwa kiasi uharifu mwingi uliokuwa unajitokeza.Isipokuwa, rai yangu ni kutaka kuona mambo yote yafanyike ki-proffessional.... Am stay to be corrected

🔵Na: Shujaa©️®️Ⓜ️

0712054498

stmwaisembac@gmail.com
 
Polisi Jamii/shirikishi ni nini?
Ni ushirikiano wa ufanyaji kazi pamoja kati ya jeshi la polisi na Jamii husika katika kuzuia na kupambana na uhalifu na viashiria vya uhalifu(according to kipeperushi)

Kwamba Ili huyu bwana polisi Ili afanye kazi yake ya kutulinda raia na mali zetu basi anategemea zaidi huo ushirikiano kutoka kwetu ikiwemo kupata taarifa mbalimbali kutoka kwetu zitakazo msaidia yeye kufanikisha huo ulinzi.
Kama ni kweli polisi mmoja anatakiwa kuhudumia raia 1000 aisee basi polisi shirikishi haikwepeki mana hawatoshi hata theluthi yetu. Lakini kama kuna vijana wamejitolea kulinda mitaa mzee sio mbaya mkiwapa hizo chenji chenji wanunue hata betri za tochi zao tu.
Mapoti hawatoshi kujilinda wenyewe muhimu chief,
 
Bandiko lako sijalisoma lote mjomba wangu. Lakni
Nimekunukuu hapa

"Tusije tukawa tuingiza Vibaka au Wezi waliohalalishwa!!!?"

Wamekamatwa mara nyingi sana wakiiba mfano ni eneo ninalo ishi Mimi.

Narudi kumalizia kusoma na kuweka hapa kisa chote.

Kimradhi
 
Back
Top Bottom