BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,013
- Thread starter
- #1,021
Shukrani sana Mkuu Mgodo visa kwa kuchangia uzi huu.
Mkuu japo Uzi ni wa muda mrefu, tangu 2009, Nadhani bado ninayo nafasi kuchangia, ili wanachama wenzagu ndani ya JF, wapate kujua ni kwa nini natumia jina/id ya ya Mgodo visa.
Ilikuwa ni 1992, nakumbuka nilikuwa moja ya Madarasa (ningeomba nisitaje) katika shule ya Msingi Kibasila.
Kwa ufupi, nilikuwa ni mtu wa Story nyingi za Vituko na Matukio, nilikuwa ni moja ya watu wachekeshaji na nisie kaukiwa na Vibweka (yote hii ilisababishwa na Mzee wangu kumiliki Runinga mapema).
Siku moja katika Maongezi, ilitokea ndani yake badala ya kutamka neno MDOGO, mimi nikatamka MGODO...
Basi hapo ndipo kama jina lilizaliwa.
Kila mmoja anajua, pale unapo jifanya mjuaji, na bahati mbaya UKACHAPIA..
Jina lilinibamba, watu Mgodo...Mgodo..na wengine wakaongezea neno Visa.. (likazaliwa Mgodo visa)
Bahati nzuri/mbaya nikaenda/nikachaguliwa Elimu ya Sekondari, shule moja na baadhi ya class mate, jina Mgodo visa likaendelea...kutokana na kuendelea na Vituko au mbwembwe.
Wanafunzi wengine wakaona jina hilo limekaa mahala pake....yaani acha tu wana JF, Jina langu halisi, mpaka ndugu zangu wenyewe wameshaa lisahau..but life goes on, jina ni utambulisho tu, no matter ni zuri au baya.
Ndio maana yupo na MASUDI KIPANYA..
kweli wewe mgodo visaNaona Mr Obama kajisahau....yeye ni Mzungu ila anacheka KISWAHILI..!!
Hahaahaa Mshana Jr..
Nipo mkuu.Dah! We mtu ulipotea humu. Ilibidi nihakikishe hili bandiko lako si la miaka chungu nzima iliyopita. Good to see you again Mkuu.
Nipo mkuu.
Nikipata chance huwa nachangia, ila mara nyingi nimegeuka mtazamaji tu.
Hivi zile JF re-union parties hazipogo tena?
Pamoja sana mkuu.
Mapendo,
TANMO.
Id yako kwa kihehe maana yake "Mnakufa"Good thread! Big up Mkuu BAK.
Kwa kuasisi hii thread.
ID yangu inamaanisha MPWA kwa kikabila chetu.
Nimeamua kuwa na hii Id kwa sababu tangu utotoni nimelelewa na my Auncle hadi na kanisapoti kielimu hadi nimefika chuo kikuu.
Auncle akiwa ananitambulisha kwa watu lazima aseme huyu ni Mpwa wangu, kwahiyo nimeamua kuwa na Id ya hivi kama kumkumbuka na kumuenzi kwa fadhila alizonifanyia.
Shukrani kwa kunijuza maana kwa lugha nyingine.Id yako kwa kihehe maana yake "Mnakufa"
Not tru..My real name..
AiseeMimi hamnioni kirahisi lakini muda wote nipo JF...!
We mi nakuonaga mpaka nakinaiAisee