Watu hawaelewi....! Ngoja niwaambie.
Pole pole ana Back up ya Wazee wa CCM walioshika nafasi za juu kwenye Chama na Serikali, Wazee ambao ikitokea changamoto, Viongozi wa Sasa huwafata kuwaomba Ushauri (Kikwete hayupo).
Polepole ni aina ya Mtu anayeongea sana na Wazee kuliko Vijana, na ana urafiki kabisa na Wazee wengi.
Wakiongea naye Wazee wangemwambia Chama ni Vijana, sisi tumezeeka, Viongozi wangetutafuta pale wao wakituhitaji, Wewe Polepole ni Kijana, amka simama paza Sauti, Ongea, sisi hatuna Nguvu Tena, nenda kaongee, ukishaongea kutatokea sintofahamu, then ndiyo watatufata Wazee, na sisi tutapiga pale pale kwenye Kidonda.
Pole pole asingeweza kuongea akiwa Balozi, na ukumbuke Polepole Hana Cha kupoteza, ameshawahi kushika nafasi za juu sana kwenye Chama na Serikali wastani wa No. 3 Enzi ya Maghufuri, angeweza tu kuendelea kula mafao yake ya Ubalozi, na Kwa Umri wake angeweza kuwa Balozi Kwa zaidi ya miaka 10 mbele, lakini Kila anaongea na Wazee wanamwambia Nchi inapotea huku Vijana mnatizama....!?
Mwisho akaamua kuacha Ubalozi, akashika Sindano na kutoboa Jibu, usidhani kamaliza, anayo mengi ya kusema, Pole pole anayajua mengi kwenye hii Nchi kuliko hata Mawaziri wa kawaida ama Wabunge, so anawasubiri.....! Na huko Kwa nje, Wazee wanawasukuma Vijana wengine, watoke waseme.....!
Tegemea Mabadiriko soon.