GE2025 Je, hoja za Polepole zinajibika?

GE2025 Je, hoja za Polepole zinajibika?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
359,882
Reaction score
828,453
Jana Pole pole ameingia sehemu ya tatu ya mafunuo yake ya ccm kwa wananchi wa Tanganyika.. Ni wazi kabisa anainyonga ccm kikatili mno... Na hii ndio faraja ya Watanganyika...

Kisu kimekaribia kabisa mfupa .. Na katika hatua hii muhimu ametoa muda ajibiwe kwa weledi na viongozi wa kaliba yake na si "ma laymen" na watu wasiohusika na siasa.

Hizi ndio hoja zake kwa ufupi. Ambazo kama zitafanyiwa kazi vema.. Hatatoa sehemu ya mwisho ya funuo lake ambalo linaweza kuwa kata funua na pigo la mwisho kwa CCM.

1. Wahuni bado wapo( Sana mtandao waliofanikisha ushindi wa JK)

2. Taratibu za kuwapata wagombea katika ngazi zote zimekiukwa (kwa nguvu ya mtandao/wahuni)

3. Rais anahujumiwa.. Pengine hajui na kama anajua kwanini hachukui hatua. Wanaomhujumu ni wana mtandao

4. Rais amezungukwa na wahuni (Sana mtandao)

5. Rais amekuwa "mpole Sana" kuchukua hatua (kwa tafsiri nyingine amekuwa dhaifu) mbele ya wanamtandao (wahuni)

Sehemu hii ya tatu imegusa zaidi kuufahamisha uma wa Tanganyika wahuni ni akina nani.. Kwamba aliowaita wahuni siku zote ni kundi la wanamtandao wa 2010.

Hilo sio kundi la kubeza hata kidogo maana lina ukwasi wa kueleweka
Lina connection ya biashara kubwakubwa kitaifa na kimataifa.

Limeshikilia sehemu muhimu za rasilimali za Tanganyika. Ndio linahusika/limehusika kuuza/kugawa rasilimali za Tanganyika. Lina mitandao ya watu kila eneo nyeti na muhimu nknk

Sasa; je, ukiachana na malengo ya muda mrefu ya kundi hili la kuiteka mazima Tanganyika na kuwa mikononi mwao.. Je, mkandarasi mkuu ni nani? Wajumbe ni akina nani? Wafaidikaji ni akina nani?
Ukisoma riwaya ya Nick Carter ya SLAVE MASTER utaona wazi mbinu zilizotumiwa na makundi ya kimafia kuwaweka viongozi madarakani kwa faida zao binafsi ndio ambazo zinatumiwa na wanamtanfao/wahuni Tanganyika
Wanakuwezesha tangu chini mpaka juu unashika madaraka muhimu ama nafasi nyeti kisha wanaanza kukutumia. Ukijaribu kuwapinga wanakuletea sehemu tu ya mafaili yako tenge unaufyata.

Pole pole anawajua vema na bila backup kubwa na yenye nguvu nyuma yake asingeweza kufika jana!

Kuutaja mtandao (wahuni) na kutoa rai ya kujibiwa ni maandalizi ya kuufumua mtandao wote sasa.. Maana kuna majina ameshaanza kuyagusia.

Jana Mara baada tu ya hotuba yake kuna anayetajwa kama mkandarasi mkuu wa wana mtandao akajitokeza "kumjibu" Polepole kwa vijembe! Alishindwa kabisa kuvumilia .. Sasa ni rasmi keshaingia kwenye mfumo wa Half ray!

Key players wanaoweza kusikika sana wiki hii:

Mzee Butiku
JK
Mzee Warioba
RA

Je hoja zitajibiwa kwa weledi? Before it is too late!? Its a race against time!


View: https://youtube.com/shorts/iTyWE1OqHlI?si=QAZxzBoPopbbIqGc
 
Jana Pole pole ameingia sehemu ya tatu ya mafunuo

Je hoja zitajibiwa kwa weledi? Before it is too late!? Its a race against time!View attachment 3430412
Duh。。。!, ,hoja zote zitajibiwa,tuamuaanda Stivu, Mwijaku na Baba Levo wanamtosha,viongozi wetu wako bize na jambo letu lile,hawana time ya kujibishana na watu wa mitandaoni!, ila kwa hadhi yako na heshima humu,hoja ni za sana,ila picha ondoa!watu wengine tuko very sensitive,ukiangalia picha za vitu fulani,unasikia mpaka harufu!,tutashindwa kupiga Breakfast。
Nakuomba please!
P
 
Polepole amekua ni Kigogo anaeonekana na ndio sababu kuu ya kuacha kazi maana hawezi kusema haya akiwa kazini.

Kwa Nchi zenye weredi ilitakiwa Tume iundwe tena kwa kupitia Bunge wanateuliwa watu wanafanyia kazi hoja za jamaa maana anaweka pia Usalama wa Nchi rehani kwa maneno yake na si ya kuyabeza sema ndio hivyo hakuna mtu anaeweza kutoa mawazo mazuri kwa hao jamaa wakaeleweka vizuri.

Gwajima wasizwa wakaamua kumtoa kwenye reli wakiaminisha Umma kuwa hatakiwi kusema lolote hata huyo Msizwa mwingine ambae yupo Jela ni kwa mapendekezo ya hao hao wasizwa wenye nguvu sasa wanajaribu kuwanyamazisha wapinzani wasiseme kitu kumbe lipo kundi kubwa ndani yake hawapendezewi na jinsi mambo yanavyokwenda maana haya alitaka kuyaongea Gwajima ikaonekana atafutwe mtu mwingine ndio huyo Mzalendo akaona amwage ugali na mboga wacha sisi tuendelee kuwasikiliza wasizwa tu.

Mkuu wa Jeshi la Puerto Rico aliwahi kusema wapo wageni wengi tena wameshika zile nafasi za maamuzi hakuna kitu Wasizwa walifanya zaidi ya kujikita na Uchaguzi kwanza Nchi baadae ndio maana unaona yote haya yanatokea.
Tuhuma nzito kama hizi tunategemea majibu kutoka kwa Manara na Lucas Mwashambwa si utani huo.
 
Duh。。。!, ,hoja zote zitajibiwa,tuamuaanda Stivu, Mwijaku na Baba Levo wanamtosha,viongozi wako bize na jambo letu, ila kwa hadhi yako na heshima humu,hoja ni za sana,ila picha ondoa!watu wengine tuko very sensitive,ukiangalia picha za vitu fulani,unasikia mpaka harufu!,tutashindwa kupiga Breakfast。
Nakuomba please!
P
Kwa heshima na kwa kuheshimu ombi na kujali nimeiondoa picha .. Jambo muktadha wake ulishabihiana na mtazamo wangu kwa njia ya tafakuri ya ulaji.. Kama Tanganyika isingekuwa nono hata wanantandao AKA wahuni wasingehangaika hivi
 
Hoja nzito isiyo na ushahidi.
Huu hapa
1754272077773.jpg
 
Pole pole amekua ni Kigogo anaeonekana na ndio sababu kuu ya kuacha kazi maana hawezi kusema haya akiwa kazini.
kwa Nchi zenye weredi ilitakiwa Tume iundwe tena kwa kupitia Bunge wanateuliwa watu wanafanyia kazi hoja za jamaa maana anaweka pia usalama wa Nchi rehani kwa maneno yake na si ya kuyabeza sema ndio hivyo hakuna mtu anaeweza kutoa mawazo mazuri kwa hao jamaa wakaeleweka vizuri. Gwajima wasizwa wakaamua kumtoa kwenye reli wakiaminisha Umma kuwa hatakiwi kusema lolote hata huyo Msizwa mwingine ambae yupo Jela ni kwa mapendekezo ya hao hao wasizwa wenye nguvu sasa wanajaribu kuwanyamazisha wapinzani wasiseme kitu kumbe lipo kundi kubwa ndani yake hawapendezewi na jinsi mambo yanavyokwenda maana haya alitaka kuyaongea Gwajima ikaonekana atafutwe mtu mwingine ndio huyo Mzalendo akaona amwage ugali na mboga wacha sisi tuendelee kuwasikiliza wasizwa tu.
Mkuu wa Jeshi la Puerto Rico aliwahi kusema wapo wageni wengi tena wameshika zile nafasi za maamuzi hakuna kitu Wasizwa walifanya zaidi ya kujikita na Uchaguzi kwanza Nchi baadae ndio maana unaona yote haya yanatokea.
Tuhuma nzito kama hizi tunategemea majibu kutoka kwa Manara na Lucas Mwashambwa si utani huo.
Bado nchi iko salama maana yuko very selective na maneno yake! Anauchunga vizuri sana mdomo wake japo hiyo part 4 atakapoongea "wasiyopenda kuyasikia" nyoka karibia wote watatoka shimoni
 
Kwa heshima na kwa kuheshimu ombi na kujali nimeiondoa picha ..
Asante sana Mkuu Mshana Jr kwa kuniheshimu,hakuna kitu kizuri kama kumcha Mungu kinafuatiwa na heshima,nidhamu,utii na unyenyekevu。
You command much respect na ingawa tuko in different school of thought,but nakuheshimu sana!
Thanks,
P
 
Asante sana Mkuu Mshana Jr kwa kuniheshimu,hakuna kitu kizuri kama kumcha Mungu kinafuatiwa na heshima,nidhamu,utii na unyenyekevu。
You command much respect na ingawa tuko in different school of thought,but nakuheshimu sana!
Thanks,
P
Pamoja brother 🙏🏿
 
Hizi mila na desturi anazoeleza Kiroboto ni kwanini hazikutungiwa sheria na kuwa katika maandishi. Jamii zetu za ki Afrika zilipoteza mila na desturi nzuri za zamani kwakua utaratibu wa kukabidhiana mila hizi uliharibiwa na biashara ya watumwa .karne hii bado tunategemea kukabidhi kizazi kinachofuata desturi za sumulizi.
 
Bado nchi iko salama maana yuko very selective na maneno yake! Anauchunga vizuri sana mdomo wake japo hiyo part 4 atakapoongea "wasiyopenda kuyasikia" nyoka karibia wote watatoka shimoni
I think,its a bit too little too late,hana Impact yoyote on the ground zaidi ya mitandaoni!

Huwezi kukata tawi la mti uliokalia,likikatika linakwenda na wewe,shuka chini,simama kwa pembeni,ndipo upige hilo shoka moja mbuyu chini.
P
 
I think,its a bit too little too late,hana Impact yoyote on the ground zaidi ya mitandaoni!

Huwezi kukata tawi la mti uliokalia,likikatika linakwenda na wewe,shuka chini, kwa kwa pembeni,ndipo upige hilo shoka moja mbuyu chini.
P
Mkuu usiongee kirahisi hivyo nakumbuka wewe uliwahi kukata mbuyu ukiwa chini kwa pembeni tukakuombea sana ulivyoitwa kwenye Kamati ya Bunge la wakati huo na ulipewa muda mchache sana kufika Dodoma kwa usafiri wako viatu ulivua huku ukijhojiwa tusiwe wepesi wa kusahau kwa matukio yanayotuhusu.
 
Slowslow, kusema kuwa "state imekamatwa" ni kosa kuliko la jamaa Mhe. Tobo la kusema atakinukisha kweli kweli.
Kwa maneno mengine ni kuwa Slowslow na, Gwajiboy wanapaswa kuwa chumba kimoja na Mhe. Tobo huko Ukonga au Segerea kama kweli mnaamini kuwa wanaisema mamlaka bila hiana.

Nawaona Mr. Slowslow na Gwajiboy ni project ya mamlaka ili kuwahadaa ninyi wadanganyika ili Oktoba iende kama ilivyopangwa.

Ukiangalia hata upepo wa NRNE umepoa sana mitandaoni na site kadli tunavyoelekea Okotba lakini kinachosikika sana ni press conferences za Mr. Slowslow.
Na kipindi cha kampeni kikifika kila wiki hizo press conferences za Gwajiboy, Mazishi wa Bunda, Slowslow na wengine wengi zitakuja ili kuendelea kuwapoteza wadanganyika.

Mkijakuzinduka mtamkuta Mr. Slowslow anakunywa juice akiwa na dada poa akijipaka KYJelly huku Gwajiboy akirekodi kitu cha Dume na mkono wa baunsa halafu Mr. Mazishi , akila viazi na samaki mkubwa wa kuchemshwa naye akijirekodi video ili apate content ya kupositi mitandaoni.

Hao wote ni majasusi wapo kazini kuhalalisha uchaguzi hivyo msiwe wajinga.
 
Kudhihirisha wazi kuwa wahuni wamechukia, tayari mmoja wa wahuni wakubwa, usiku usiku imebidi ajitokeze kujibu mapigo dhidi ya Pole pole, bahati mbaya mnoo akashindwa kujibu hoja na zaidi akaishia kutuma vijembe tu.
Trust me hawawezi kujibu kama anavyotaka kwakuwa
1. Itakuwa kuthibitisha tuhuma za muda mrefu
2. Kumpa ushindi utakaompa mileage kubwa.. Then what next? End of era ya wanamtandao... Impact yake ninini? Mapinduzi ama mageuzi makubwa kisiasa na kimfumo yatakayoipumzisha ccm na mwanzo mpya wa mapambano wa kuirudishia Tanganyika kilichoporwa na wahuni
 
Back
Top Bottom