Jana Pole pole ameingia sehemu ya tatu ya mafunuo yake ya ccm kwa wananchi wa Tanganyika.. Ni wazi kabisa anainyonga ccm kikatili mno... Na hii ndio faraja ya Watanganyika...
Kisu kimekaribia kabisa mfupa .. Na katika hatua hii muhimu ametoa muda ajibiwe kwa weledi na viongozi wa kaliba yake na si "ma laymen" na watu wasiohusika na siasa.
Hizi ndio hoja zake kwa ufupi. Ambazo kama zitafanyiwa kazi vema.. Hatatoa sehemu ya mwisho ya funuo lake ambalo linaweza kuwa kata funua na pigo la mwisho kwa CCM.
1. Wahuni bado wapo( Sana mtandao waliofanikisha ushindi wa JK)
2. Taratibu za kuwapata wagombea katika ngazi zote zimekiukwa (kwa nguvu ya mtandao/wahuni)
3. Rais anahujumiwa.. Pengine hajui na kama anajua kwanini hachukui hatua. Wanaomhujumu ni wana mtandao
4. Rais amezungukwa na wahuni (Sana mtandao)
5. Rais amekuwa "mpole Sana" kuchukua hatua (kwa tafsiri nyingine amekuwa dhaifu) mbele ya wanamtandao (wahuni)
Sehemu hii ya tatu imegusa zaidi kuufahamisha uma wa Tanganyika wahuni ni akina nani.. Kwamba aliowaita wahuni siku zote ni kundi la wanamtandao wa 2010.
Hilo sio kundi la kubeza hata kidogo maana lina ukwasi wa kueleweka
Lina connection ya biashara kubwakubwa kitaifa na kimataifa.
Limeshikilia sehemu muhimu za rasilimali za Tanganyika. Ndio linahusika/limehusika kuuza/kugawa rasilimali za Tanganyika. Lina mitandao ya watu kila eneo nyeti na muhimu nknk
Sasa; je, ukiachana na malengo ya muda mrefu ya kundi hili la kuiteka mazima Tanganyika na kuwa mikononi mwao.. Je, mkandarasi mkuu ni nani? Wajumbe ni akina nani? Wafaidikaji ni akina nani?
Ukisoma riwaya ya Nick Carter ya SLAVE MASTER utaona wazi mbinu zilizotumiwa na makundi ya kimafia kuwaweka viongozi madarakani kwa faida zao binafsi ndio ambazo zinatumiwa na wanamtanfao/wahuni Tanganyika
Wanakuwezesha tangu chini mpaka juu unashika madaraka muhimu ama nafasi nyeti kisha wanaanza kukutumia. Ukijaribu kuwapinga wanakuletea sehemu tu ya mafaili yako tenge unaufyata.
Pole pole anawajua vema na bila backup kubwa na yenye nguvu nyuma yake asingeweza kufika jana!
Kuutaja mtandao (wahuni) na kutoa rai ya kujibiwa ni maandalizi ya kuufumua mtandao wote sasa.. Maana kuna majina ameshaanza kuyagusia.
Jana Mara baada tu ya hotuba yake kuna anayetajwa kama mkandarasi mkuu wa wana mtandao akajitokeza "kumjibu" Polepole kwa vijembe! Alishindwa kabisa kuvumilia .. Sasa ni rasmi keshaingia kwenye mfumo wa Half ray!
Key players wanaoweza kusikika sana wiki hii:
Mzee Butiku
JK
Mzee Warioba
RA
Je hoja zitajibiwa kwa weledi? Before it is too late!? Its a race against time!
View: https://youtube.com/shorts/iTyWE1OqHlI?si=QAZxzBoPopbbIqGc