Je, hii 6th Sense ya Mtu Jasusi (Njagu) huwa anakuwa amezaliwa nayo au anafundishwa huko Vyuoni CIA na MOSSAD?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,548
108,882
Nimekuwa nikisikia sehemu mbalimbali (hasa hasa hapa nchini Herzegovina) yalipo Makazi yangu Siku zote kuwa licha ya Wanadamu wote kuwa na Five ( 5 ) Senses, ila kwa wale Majasusi (Manjagu) wao wanatakiwa kuwa na ya Sita (6) pia.

Je, hii ( hiyo ) Sixth ( 6 ) Sense anayotakiwa hasa kuwa nayo Jasusi (Ngagu) hasa wa CIA na MOSSAD ni ipi?

Na kwanini huko CIA na MOSSAD hata kama ukiwa Umefuzu Mafunzo yote ya Kimedani (Kijeshi) ila ukiwa huna hii (hiyo) Sixth (6) Sense huwezi kuwa katika hayo Mashirika yao ya Ujasusi?

Mwisho ni Swali tu je, katika Mashirika mengine ya Kijasusi (Kinjagu) duniani kote nao Watendaji wao wanayo hii Sixth (6) Sense ambayo inawafanya wawe 'Competent' kama hawa wa CIA na MOSSAD?

Na je, huwa inakuwa ni ya Kuzaliwa nayo au labda ni ya Kufundishwa tu huko Vyuoni Kwao nchini Marekani na Israel?

Nasubiri kwa hamu tu 'Utaalamu' wenu.
 
Actually "gut feeling" kila mnyama anazaliwa nayo. Na lengo hasa ni kujizuia na hatari za maisha ila sasa watt wengine wamejifunza kuiheshimu na wengine huwa tunaipuuza

Wale wanaoiheshimu na kuitekeleza wanajikuta wanakua wameimasta kuliko sie tunaoipuuza. Na wanachofanya hao jamaa uliowasema katika mafunzo ni kukuelekeza jinsi ya kuweza kuimasta tu ila ipo kwa kila mnyama
 
Ni karama kama karama nyingine kama umesoma kitabu ama umetazama filamu ya Red sparrow utakubaliana na mimi.

Ila kwa Tanzania yetu maafisa wengi wa usalama ni vilaza na hawashirikishi akili zao vyema katika maamuzi kuanzia spymaster wao and et al wote hakuna kitu kidogo Enzi za Marehemu Apson na Emilio Mzena vijana walikuwa wako fit sio hawa walevi na wapenda malaya.

Hawa wa kwetu eti kuwa na machale ndio wanaita the 6th sense 😔
 
Huwa tunazaliwa nayo mkuu ...mimi kila sehemu ninayokwenda watu huwa wanahisi niko upande ule....na hata nilipokuwa gerezani butimba wafungwa walikuwa wananifuata na kunieleza matatizo yanayokuta kule ndani wakihisi nimetumwa...
Hawakujua we ni kibaka mwenzao
 
ila ukiwa huna hii ( hiyo ) Sixth ( 6 ) Sense huwezi kuwa katika hayo Mashirika yao ya Ujasusi?


Hilo hapo jibu umeshajijibu. Inamaana kule ni training tu ndo mana hawachukui mazezeta, nahisi unapewa kazi kulingana na akili yako inavyokutuma

Wanahitaji watu wa kada tofautitofauti kule, juna wataalam wa lugha, afya, mitambo, kuchakata habari, ujasusi n.k. inategemea utawekwa eneo lipi. Na uzuri wao kuna baadhi ya vitengo vinatangazwa kabisa watu wanaomba wakishindana kwa sifa, vigezo na uzoefu.

Ila kuna baadhi ya vitengo kwa unyeti wake, inahitajika watu wenye uwezo na mafunzo maalum ikiwepo hii anaiongelea super talented, game changer GENTAMYCINE
 
Wanahitaji watu wa kada tofautitofauti kule, juna wataalam wa lugha, afya, mitambo, kuchakata habari, ujasusi n.k. inategemea utawekwa eneo lipi. Na uzuri wao kuna baadhi ya vitengo vinatangazwa kabisa watu wanaomba wakishindana kwa sifa, vigezo na uzoefu.

Ila kuna baadhi ya vitengo kwa unyeti wake, inahitajika watu wenye uwezo na mafunzo maalum ikiwepo hii anaiongelea super talented, game changer GENTAMYCINE
Haya yamejumuishwa kwenye " Akili yako inavyokutuma" mkuu
 
Back
Top Bottom