Je, hii 6th Sense ya Mtu Jasusi (Njagu) huwa anakuwa amezaliwa nayo au anafundishwa huko Vyuoni CIA na MOSSAD?

Nimekuwa nikisikia sehemu mbalimbali (hasa hasa hapa nchini Herzegovina) yalipo Makazi yangu Siku zote kuwa licha ya Wanadamu wote kuwa na Five ( 5 ) Senses, ila kwa wale Majasusi (Manjagu) wao wanatakiwa kuwa na ya Sita (6) pia.

Je, hii ( hiyo ) Sixth ( 6 ) Sense anayotakiwa hasa kuwa nayo Jasusi (Ngagu) hasa wa CIA na MOSSAD ni ipi?

Na kwanini huko CIA na MOSSAD hata kama ukiwa Umefuzu Mafunzo yote ya Kimedani (Kijeshi) ila ukiwa huna hii (hiyo) Sixth (6) Sense huwezi kuwa katika hayo Mashirika yao ya Ujasusi?

Mwisho ni Swali tu je, katika Mashirika mengine ya Kijasusi (Kinjagu) duniani kote nao Watendaji wao wanayo hii Sixth (6) Sense ambayo inawafanya wawe 'Competent' kama hawa wa CIA na MOSSAD?

Na je, huwa inakuwa ni ya Kuzaliwa nayo au labda ni ya Kufundishwa tu huko Vyuoni Kwao nchini Marekani na Israel?

Nasubiri kwa hamu tu 'Utaalamu' wenu.
Genta!

We jamaa masuali yako huwa ni ya mtego na huwa nayaelewa sana.

Ila nahisi suali lako lina zaidi.

Kwa kifupi hiyo kama walivyosema baadhi hapa "sixth sense" ni Uwezo wa juu kabisa baada ya zile "5 senses".

Hivyo zile 5 senses yaani kunusa, kuonja, kuona, kushika na kusikia zinaungana na ile ya sita yaani akili yaani hisia pamoja na uwezo wa kuamua jambo au decision making capacity.

Mtu aweza kufanya na kutimiza yote yale matano hapo juu lakini akashindwa jambo kubwa sana au kufeli kutokana na kushindwa kudhibiti hisia zake na mwisho, kuchukua hatua au kufanya maamuzi sahihi kwenye sixth sense (decision making capacity).

Wakuta mtu ameepa mambo mengi lakini anakuja kunasa kwenye jambo dogo tu na ajilaumu.

Hivyo sixth sense ni uwezo wa akili katika kufanya maamuzi na ukichanganya na welevu au "intellect".

Ili kupata wanafunzi wazuri yabidi kwenda mashuleni, na kisha ukiwachukua wanafunzi hao wawaendeleza.

Baadae kwa kuwa wafahamu watakwenda chuo kikuu basi wakiingia mwaka wa pili wanakuwa makuruta hadi wanamaliza na kisha wawapeleka chuoni.

Hii kozi yatakiwa miaka mitano maximum na huchanganywa mambo mengi yakiwemo ya kijeshi kiasi cha mtu kuiva na nchi zingine huwa na cheo cha luteni.

Pale hujifunza lugha mbalimbali, zaidi ya kiswahili na kiingereza, historia, mawasiliano na somo la elimu ya jamii au sociology.

Kwenye MI au military intelligence huwa wanachukua pale mfano wa JKT ambapo siku hizi sidhani kama wafanya hivyo.

Pale pana talent pale, na kisha watakiwa kupelekwa Monduli na kisha nje kwenye nchi rafiki ukapate maarifa zaidi.

Ila suali lako ni muhimu sana kuzingatiwa katika Tanzania ya leo.
 
Back
Top Bottom