Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,664
4,876
Chawa walikuja na mbwembwe kwamba karejesha uhuru wa habari na kujieleza. Hila kiuhalisia anadidimiza uhuru wa kujieleza.

Juzi kati Ney Wamitego aliachia ngoma yake, ambayo badae akaitwa BASATA akaitwa na Polisi. Siku kadhaa zimepita Dada wa kule mbeya naye akaachia kibao chake "Mnatuona Nyani". Kibao icho cha kwaya kikamletea Dada huyo kesi iliyosababisha kukamatwa na kulala mahabusu. Ambapo badae mchungaji au baba wa kiroho wa huyo Dada alikuja mtandaoni na kulaani kitendo cha mtumishi wake kuwekwa mahabusu.

Hata hivyo siku ya leo habari imesambaa mitandaoni kwamba Mchungaji huyo aliyekemea kitendo cha mtumishi wake kufungwa mahabusu kisa wimbo. Nae kakutana na Panga ambapo inasemekana amehukumiwa kwenda Jela miaka 3 kwa kuendesha kanisa bila kibali.

Kwa tuliosoma CUBA hii ni njia ya kuwanyima raia uhuru wa kujieleza, kwa kuwatafutia sababu ili uwaadhibu. Wanajenga ofu kwa wananchi, hili tusilalamike juu ya kero zinazosabishwa na kina Bi Tozo
 
Na mkome tuliwaambia rais ni magufuli ambaye analeta maendeleo japo anaminya uhuru kidizaini ili watu wafanye kazi


Sasa mnauzwa,uhuru mnalalamika mnanyimwa,maendeleo mnasema hakuna ,kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake..



Jpm ulale salama hakuna wa kukumbuka Acha tuumie na hili jua safi kbs
 
Back
Top Bottom