Ugiriki, falme ya Macedonia, Uyunani; mama na kitovu wa nchi za Ulaya, iliyokuwa dola-himaya ya nne ya dunia (4th world hegemony)

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Jun 28, 2016
348
847
UGIRIKI, FALME YA MACEDONIA, UYUNANI; MAMA NA KITOVU WA NCHI ZA ULAYA, ILIYOKUWA DOLA-HIMAYA YA NNE YA DUNIA (4th WORLD HEGEMONY)

Na. Comred Mbwana Allyamtu (CMCA)
Wednesday-14/12/2022
Olasiti Arusha, Tanzania

Ugiriki ni nchi yenye historia ndefu sana duniani, imewahi kuwa Dola kiranja wa 4 wa dunia, yani World hegemony au World Super-Supremancy Empire, yani Baada ya Mesopotamia, Kemet, Umedi na Uajemi ikafuata Ugiriki ntaeleza hilo huko mbeleni.

Nchi ya Ugiriki kwa sasa ni moja ya nchi maarufu sana huko Ulaya hata kupewa jina la "nchi mama balani Ulaya", hii ni kwasababu Ugiriki ni kitovu cha Ustaarabu wa nchi Karibu zote Ulaya mashariki na Ulaya magharibi.

Hii ni kwasababu Ugiriki ndipo zilipoanzia demokrasia hii ya sasa, falsafa ya magharibi ya utawala, nadharia ya fasihi ya sasa, historiografia, sayansi ya siasa, tafiti za sayansi na hisabati, nadharia ya sheria ya sasa na michezo ya Olimpiki.

Nyingi ya elimu hizi zilitokea Kemet (Misri) ya kale, wao ndio asili ya elimu yote duniani, asilimia 75 ya maarifa duniani imetokea Misri yani Kemet.

Ugiriki ndio Nchi mama Ulaya kwasababu ndio dola ya kwanza Bala la Ulaya kuwa taifa kubwa na lenye nguvu (Hegemony) kutokea Ulaya, hii Inamaana kuwa Ugiriki ndio taifa la kwanza Ulaya kushika nafasi ya kutawala dunia, kabla yake dunia ilikuwa Asia na Afrika yani, Umedi na Uajemi, Kemet na mesopotamia.

Hivyo ulaya ilipokea ubwana mikononi mwa Ugiriki, ustaarabu ukaanzia Ugiriki, dunia ya Ulaya ikaanzia Ugiriki.

Ugiriki ilianza kupata nguvu na kuwa Dola-himaya ilipo tawaliwa na Alexander III of Macedon, kwa umaarufu zaidi alifahamika kama Alexander the Great.

Alexander aliunda jeshi lake na kutangaza azma yake ya kutawala dunia akitokea Ugiriki, kwamba dunia nzima ingefuata amri zake, Viongozi wa dola nyingine zote wawe kama magavana, wenye kufuata maagizo na amri zake.

Alexander anabaki kuwa baba wa Ulaya kwasababu ndio aliyefungua njia Ulaya kuitawala Dunia mpaka sasa, ni Alexander the great aliye anzisha tafsiri halisi ya neno Dola-himaya (Hegemony).

Hegemony inamaana kuwa Taifa moja kubwa lenye nguvu kijeshi na kiuchumi linakuwa na mamlaka na ushawishi wa kutawala dunia nzima, na Wakuu wa mataifa mengine wawe wafuata maagizo na amri zake.

Taifa moja linakuwa na nguvu endelevu ya kutawanya mabavu yake ya kijeshi duniani ili kumiliki uchumi na utamaduni wa dunia.

Hivyo basi...

Ugiriki imeanza miaka 3500 iliyopita, Lugha ya Kigiriki inayo andikwa kwa Alfabeti ya Kigiriki imeanza tangu miaka 3000 iliyopita, japo kwasasa lugha yenyewe imebadilika kwa kiasi kadhaa, lakini lugha ya kigiriki ndio lugha kongwe zaidi duniani inayoandikwa ambayo bado inatumika mpaka sasa

Huwezi kuzitaja lugha kongwe duniani bila kuitaja lugha ya kigiriki, zingine ni Kiibrania, kihindi, Kichina, kijapan, Kiarabu na Kiaztec.

Kama nilivyosema huko awali, Ugiriki (Greek kingdom of Macedonia) ilianza karibu miaka 3140 kabla ya karenda ya kawaida (BCE), nchi hiyo ilianzishwa na Mfalme Caranus the Predecessor au Karanos, huyu ndie alikuwa mfalme wa kwanza wa ufalme wa kale wa Ugiriki ya Masedonia kulingana na simulizi za kale za Ugiriki.

Uthibitisho wa kuwa Caranus kuwa ndie baba mwanzilishi wa chimbuko la Dola ya Ugiriki ni Kulingana na simulizi za mwanahistoria mkubwa anaye heshimika Ugiriki anayeitwa Herodotus.

Japo wengine humtaja mfalme wa kwanza wa Ugiriki alikuwa ni Perdiccas I, lakini bado matini na simulizi za kale zimeendelea kuthibitisha kuwa Caranus kuwa ndio mwasisi wa Dola ya Ugiriki ya Macedonia, hilo lipo kwenye simulizi za Theopompus, zinazodai kuwa Caranus ndiye mwanzilishi wa nasaba ya Argead, ambayo ndio nasaba ya kwanza Ugiriki kutawala, japo miaka halisi haifahamiki.

Miliki kubwa ya Dola-himaya ya Ugiriki na falme ya Macedonia Katika kutawala dunia ilianza kipindi cha utawala wa Alexander the great, kabla yake Ugiriki ilikuwa dola ndogo tu katika miji kadhaa ya Athens na Sparta.

Dini kubwa Ugiriki kwasasa ni Ukristo wa Orthodox ambao ni asilimia 93% ya raia wote Ugiriki, zamani walikuwa wakifuata dini zao za asili hasa dini ya Zeus.

Kabla ya Dola-himaya ya Ugiriki na falme ya Macedonia kutawala dunia, Dola-himaya ilio anza ilikuwa ni Dola-himaya ya Mesopotamia, Dola-himaya ya mesopotamia ilipoanguka ndipo Umedi na Uajemi ika rise as Super-power commanding the then world.

Dola ya Wamedi na Waajemi ilidumu hadi alipokuja Alexander the great au Alexander mkuu huyu ndio iliye itoa Ugiriki chini mpaka juu kabisa, aliifikisha Ugiriki kuwa Dola kiranja ya Nne (4) ya dunia Alexander mkuu alikuwa ni mtoto wa mfalme Philip wa Macedonia.

Alexander the great ndio aliye iangusha dola ya Wamedi na Waajemi (Medo-Persian empire).

Wagiriki wakatawala ulimwengu mzima wa enzi hizo, Alexander alifika hadi Misri, mji Alexandria umeitwa kwa jina lake kwa heshima yake, Alexander alifika hadi India akiwa na majeshi yake tishio wakishinda miji kadhaa na nchi kadhaa na kumiliki miji na nchi kadhaa.

Alipotaka kwenda hadi Uchina, wanajeshi wakaasi, ikabidi waanze safari ya kurudi, alikufa akiwa kijana kabisa wa miaka 32, chini ya utalawa wake alipata ushindi mkubwa sana, Alexander mwenyewe alifundishwa elimu na Aristotle.

Katika harakati zake za vitani, Alexander alitumia farasi wake mmoja tu aliyempenda sana aliyeitwa Bucephalus, alipokufa huyu farasi, Alexander akauita mji jina la farasi huyu huko India kwa kumbukumbu ya farasi wake, ntalieleza hili mbeleni kidogo.

Alipokufa Alexander utawala wake ukagawanyika maeneo manne chini ya majemedari wake, ukawa ndio chanzo cha anguko la Dola hiyo, taratibu ukaenda hivyo uki decline hadi Warumi walipoibuka mwaka 168 BC kama Dola kiranja ya 5 ya dunia.

Alexander Mkuu ni nani?...

Jina lake kamili ni Alexander Philip, wazungu wao humuita Alexander the Great (yaani Alexander mwenye nguvu) mtoto wa kwanza wa mfalme Philip II wa Macedonia (Ugiriki) na Malkia Olympias binti wa mfalme Neoptolemus aliyetawala eneo la Epirus (Ugiriki).

Alexander alizaliwa mwaka 356 BC katika mji wa Pella nchini Ugiriki akifuatiwa na dada yake, Cleopatra aliyezaliwa mwaka 355 BC.

Alexander Mkuu alipoifikisha umri wa miaka 13, Baba yake, Mfalme philip II aliamua kutafuta Mwalimu atakayemfundisha mwanaye na hatimaye akamchagua Mmoja wa wanafalsafa nguli kwa jina Aristotle awe mwalimu wa kijana wake.

Kutokana na sababu za kiusalama, Mfamle Philip alitenga eneo maalumu liitwalo Mieza akajenga shule ya bweni ili mwanaye na watoto wengine wa viongozi na watumishi wa mji wa Macedonia waweze kusoma hapo,
Katika shule hiyo, Alexander alifundishwa mambo mengi yakiwemo, kusoma, kuandika, kucheza, kupigana, kuendesha farasi na kupiga zeze la jadi.

Mwanafalsafa Aristotle alimfundisha Alexander the great hadi kufikia umri wa miaka 16 na akawa ameiva kweli kweli.

Wahenga wanasema Nyota njema huonekana asubuhi, naam siku moja Alexander akiwa na miaka 10 baba yake alimuagizia farasi mdogo kutoka kwa mfanya biashara wa mji wa Thessaly ndani ya Macedonia kwa thamani ya talanta 13, Farasi huyo alipofika nyumbani aligoma kabisa kupandwa na Baba yake Alexander akataka kumrudisha,
Lakini Alexander alimsihi baba yake amnunue tu kwani aligundua kuwa farasi yule aligoma kupandwa kwa hofu ya kutazama kivuli chake.

Hivyo akamfundisha na ndani ya saa chache tu farasi akaelewa somo na akakubali kupandwa kisha akampa farasi huyo jina la Bucephalus na akawa ndiye farasi wake aliyemtumia kwa safari zake zote mpaka farasi huyo alipokufa baada ya kuzeeka.

Kitendo hicho cha kishujaa kilimshtua sana Mfalme Philip II na akamkumbatia mwanaye kwa machozi ya furaha huku akimwambia "kijana wangu, nimegundua una akili sana, naona hata huu mji wa Macedonia hautakutosha, hakikisha unatafuta himaya kubwa ya kutawala katika siku zako".

Maneno hayo yalitia chachu ya ujasiri wa Alexander katika makuzi yake kwani daima alijituma sana katika mafunzo yote aliopewa na mwalImu wake hata hivyo alitumia muda mwingi sana kukaa na baba yake ili ajifunze mambo ya uongozi.

Huku akijiandaa kuja kukalia kiti cha enzi baada ya hatima ya Baba yake Mfalme Philip II, ulipofika mwaka 336 BC, Alexander akiwa na umri wa miaka 20 tu, Baba yake mfalme Philip II aliuawa na maadui zake, Hivyo ikamlazimu Alexander kushika hatamu ya Utawala wa Macedonia mara moja akiwa angali kijana mdogo, Na akaitwa Mfalme Alexander II

Mfamle Alexander the Great alipoikamata Macedonia alionekana kuwa na akili, hivyo Macedonia ikawa ndogo sana kuitawala, ikabidi kutanua mipaka ili apate milki kubwa kadri alivyoweza kama baba yake alivyomuasa enzi za uhai wake.

Aliunda jeshi lenye nguvu huku akiwa yeye ndio kamanda muongoza njia katika vita zote alizopigana, Mfalme Alexander na jeshi lake alivamia maeneo mengi ya Dunia huku akisambaratisha tawala zote alizozikuta katika maeno hayo.

Mfano....

Mwaka 330-323 BC alikuwa Mtawala Mkuu wa Asia (Lord of Asia), huku Afrika aliivamia Misri na akafanikiwa kuwa Firauni (Pharaoh of Egypt) kuanzia mwaka 331-323 BC na mwaka 334 aliivamia Persia na kumng'oa Mfalme Darius III akajitwalia Ufalme (King of Persia) kuanzia mwaka 332-323 BC

Vita ya mapigano ya Alexander Mkuu haikukomea hapo kwani alitanua Milki yake hadi kuvuka bahari ya Adriatic na kufika mto Beas Nchini India na kusambaratisha utawala wa Bonde la India (Indus Valley) mnamo mwaka 326 BC.

Mbali na ushujaa wake katika vita, inasemekana kwamba, Mfalme Alexander the Great alichangia sana kuanzisha miji maarufu zaidi ya 20 hapa Duniani, miongoni mwake ni kama, Alexandria ulioko Misri, Alexandria Bucephala uliko nchini Pakistan.

Alexandria Bucephala ulitokana na kifo cha farasi wake (bucephalus) aliyekufa baada ya kuzeeka huko nchini Pakistan na akamua kuliita eneo hilo Bucephala kama sehemu ya kumuenzi farasi wake aliyemtumia tangu enzi za utotoni aliponunuliwa na baba yake.

Mfalme Alexander the Great alifanikiwa kuoa wanawake watatu ambao ni, Stateira, Roxana na Parysatis.

Japo haikufahamika wazi idadi ya watoto alokuwa nao lakini mtoto pekee aliyejulikana ni Lollas ambaye mara nyingi alikuwa anamchanganyia pombe mfalme Alexander II.

Mfalme Alexander II alifariki mwaka 323 BC akiwa na umri wa miaka 32 katika eneo la Babiloni lililokuwa likitawaliwa na mfalme Nebukadneza II.

Tukio hili lilifuata baada ya Mfalme Alexander II aliporejea mapumzikoni nyumbani kwake kutoka India na kafanya karamu kubwa ambayo ilichukua takribani wiki mbili.

Chanzo cha kifo chake kilizua utata wa hali ya juu na kupelekea kuwepo kwa Nadharia kadhaa zinazoelezea ukweli wa chanzo cha kifo chake,
Pamoja na uwepo wa nadharia tofauti zinazoelezea sababu ya kifo chake ila inayoaminika zaidi ni ile inayodai kuwa huenda Alexander the Great alifariki kwa madhara ya sumu iliyochanganywa katika pombe wakati wa ile karamu aliyoifanya kwa takribani wiki mbili.

Nadharia hii huenda mbali na kutoa shutuma kuwa watu wa karibu wanaweza kuwa walihusika na kifo cha Alexander kwa kumchanganyia sumu kwenye pombe, Miongoni mwa watu wanaoshutumiwa ni Bw. Antipater aliyekuwa mtendaji mkuu katika falme ya Macedonia awali kabla ya kuvuliwa wazifa huo.

Kiongozi huyu anahisiwa kumdanganya mtoto wa Alexander aliyeitwa Lollas ambaye ndiye alikuwa mchanganyaji mkuu wa pombe ya Baba yake na akafanikiwa kumpumbaza kisha jamaa akatia sumu hiyo kijanja bila bwana mdogo kushtukia mchezo.

Wengine wanaenda mbali na kudhania kwamba katika hili la sumu, huenda hata mkono wa Mwanafalsafa Aristotle ulihusika kuandaa mpango wa kumuua Mfalme Alexander II.

Watafiti wa Nadharia hii wanadai kuwa zile wiki mbili za karamu ya Alexander alikuwa hoi akiugulia maumivu makali ya tumbo na homa kali kiasi kwamba ilifikia kipindi hakuweza hata kuongea na ilipofika siku ya 12 aliishia kuwapungia mkono wanajeshi wake muda mfupi kabla ya kukata roho.

Nadharia hii ya sumu ilibakia kuwa kitendawili kikubwa akilini mwa watu kwa miaka mingi huku wengine wakifikiria kuwa ni sumu gani hiyo yenye kudumu kwa siku 12 bila kuondosha uhai wa mtu?

Uchunguzi wa baadae uligundua kuwa ni kweli Mfalme Alexander ailiuawa kwa sumu itokanayo na mmea uitwa White Hellebore au Veratrum Album ambao huota maeneo ya Ulaya ikiwemo Ugiriki na sehemu chache za Asia.

Baada ya kifo cha Alexander, majemedari wake walianza kugombanakuhusu nani atawale, miaka 22 baadae ufalme wa kiyunani uligawanyika katika falme nne chini ya majemedari waliojulikana kama DIDOCHI yaani warithi Majimbo haya yalidhoofika siku hadi siku na mwisho wakatawaliwa na UFALME WA RUMI.

Warumi nao wakatawala dunia hadi mwaka 476 AD, ambapo dola yao ilipoanguka, Dola ya Warumi ilipoanguka ndipo zikawa mwisho wa athari ya Dola ya Ugiriki baada ya kuibuka Dola kiranja mpya ya Ottoman.

Ugiriki ilianza kama eneo dogo kutokana na kuungana kwa miji muhimu ya mwanzo, kabla ya hap zilikuwa tawala za miji, kisha baadae wakaungana na kuunda Dola ya Ugiriki na falme ya Macedonia.

Wagiriki walivyokua bado hawajaungana kila Eneo lilikuwa linajitawala, walitumia nguvu zaidi kujiimarisha maana wao hawakugopa kufa waliaamini wao ni viumbe special kutoka kwa baba yao wa uumbaji Zeus.

Majina mengi ya kigiriki yanaishia na "S" hata majina ya watu wa mataifai mengine yanaishia 'S' kwakua ni utamaduni uliotokana na wagiriki.

Yesu pia jina lake laishia na 'S' yaani Jesus sababu ni kwamba wagiriki wanaamini majina yanayoishia na 'S' yanamaanisha ni mwanaume kutokana na Mungu wao wa kiume Zeus jina lake lainshia na 'S'

Walivyoungana na kua kitu kimoja wakaanza kutumia akili na nguvu ili kujiimarisha zaidi kwa kila nyanja wafalme waliwatumia watu wenye uwezo mkubwa wa kufikiri katika kutatua changamoto zinazowakabiri na waliwekea mazingira wezeshi hapa sasa ndio gunduzi zikaanza.

Mfano......

Kipindi fulani Ugiriki ilikua na sherehe ya mavuno hivyo wagiriki walikua wanamsherehekea Mungu wao wa mavuno kuwapatia mavuno mengi, Mfalme kama kiongozi mkuu alitakiwa awepo kwenye sherehe sasa mfalme akampatia dhahabu Muhunzi (Goldsmith) amtengenezee kofia ya kuvaa wakati wa sherehe (Crown), Muhunzi kuona dhahabu kashikwa na tamaa akachakachua dhahabu akaweka dhahabu nusu akaongezea na bronze (shaba) akampelekea mfalme kofia yake.

Mfalme akaangalia kofia akaona hapa kashapigwa cha juu ila hana uhakika.

Akaamua kumuita jamaa mmoja ambae kipindi hicho aliaminika ana akili sana aje amchunguzie kofia yake kama imetengenezwa kwa dhahabu tupu kweli au imechanganywa.

Ila akamwambia asiiharibu wakati wa kuichunguza maana hana kofia nyingine, Jamaa huyo ni "Archimedes"

Archimedes akachukua kofia akaenda maabala kwakwe akachunguza wee akashindwa kupata majibu kichwa kikawaka moto hajui afanye nini, akamuagiza mfanyakazi wake amuwekee maji ya kuoga bafuni kwenye Jacuzzi.

Akaenda bafuni akavua nguo akaingia kwenye Jacuzzi maji yakamwagika nje alivyoona hivo akatoka nje akikimbia uchi huku anapiga kelele hadi ikulu.

Alipomfikia mfalme akaanza kusema haraka haraka "When a body is totally or partially immersed in a fluid is subjected to an upwards force equal to the weight of the displaced fluid" ila kwa kiyunani.

Mfalme akamwambia unamaanisha nini wewe mbona sikuelewi,
Ndio mzee baba akaanza kumuelezea vizuri sasa, Akachukua vipimo vyake akapima uzito wa dhahabu na Shaba kisha akapima uzito wa Ile kofia ikaonekana muhunzi aliiba dhahabu.

Na hapo ndio tukapata Law pedwa ya Archimedes principle na law of floatation inayohusu Density.

Kupitia law hizo tumepata Meli mbalimbali..

Sio hivyo tu Archimedes alisaidia sana kwenye vita, alikua anatengeneza vifaa vya kivita au anatumia vioo kuunguza meli za maadui wanakuja kuvamia nchi yake.

Ugiriki ya Kale ilipanuka katika eneo kubwa la Mediteranea na Bahari Nyeusi, na kudumu kwa karibu karne moja, hadi Ukristo ulipoanza baada ya kuibuka Dola ya Roma.

Ugiriki ndio mwanzilishi wa utamaduni anzilishi wa ustaarabu wa magharibi mpaka sasa, Utamaduni wa Kigiriki ulikuwa na nguvu kubwa ya ushawishi katika Dola ya Roma, ambayo ilibeba sehemu ya utamaduni huo katika sehemu nyingi za Ulaya.

Ustaarabu wa Ugiriki ya kale umeathiri pia lugha, siasa, mifumo ya elimu, falsafa, sayansi, sanaa, ufundi sanifu wa dunia ya sasa.

Bila kusahau jina Ulaya au Europe la bara la Ulaya limetokana na jina la mama yake mfalme Minos wa Crete aliye itwa Europa.

Ugiriki pia ndio watu wa kwanza kutumia kondom ambazo zilitokana na utumbo mpana au vibofu vya wanyama kama ng'ombe, mbuzi, kondoo nk.

Historia inaonyesha pia Demokrasia kitovu chake ni Ugiriki ambapo karne ya 5 binadamu wa huko waliibuka taratibu na wazo la maamuzi ya serikali na uongozi unaotokana na ridhaa ya watu wengi badala ya uimla.

Mifumo ya kidemokrasia ilitumika kiasi fulani kwa tawala kama himaya za Roma ya kale, karne ya 14 mabwanyenye wa Waingereza walimlazimisha mfalame wao kusaini mkataba wa Magna Carta ambao uliweka rasmi mfalme na Serikali ya kifalme hauko juu ya sheria, ulianzisha bunge na kuweka sheria za kulinda haki na mali binafsi za watu. Karne ya 18 yakaja mapinduzi na uhuru wa makolini ya Marekani dhidhi ya utawala wa kifalme wa Uingereza, yakaja na mfumo wa Urais na demokrasia kutumika kwa upana zaidi.

Tangu wakati huo demokrasia ikasambaa duniani na mataifa mengi Ulaya na nje ya Ulaya yakaiga hiyo mifumo ya utawala wa UK na US, Baadhi kama Ufaransa yakauondoa kabisa utawala wa kifalme na kusimika jamuhuri mengi yakazidhibiti nguvu za tawala zao za kifalme.

Demokrasia kama mojawapo ya utamaduni wa ulimwengu wa magharibi umeendelea kusambaa au kusambazwa katika sehemu mbalimbali za ulimwengu kama sehemu ya athari ya Ugiriki.

Mambo mengi kuhusu Ugiriki ya leo na ile Ugiriki na falme ya Macedonia ya kale...

Nchi ya ugiriki/Uyunani inapatikana upande kusini mashariki mwa bara ka ulaya, nchi hiyi imepakana na nchi ya Albania, Macedonia kaskazini, Uturuki na Bulgaria na pia imepakana na bahari ya Mediterranean.

Nchi ya Ugiriki ulipata uhuru wake wa pili mwaka 1821 kutoka Himaya ya Ottoman, Ottoman iliwahi kuikalia Ugiriki kwa Karibu miaka 200, Ugiriki pia imeitawala Uturuki kipindi cha kale na kabla ya vita ya kwanza ya dunia.

Kwasasa sensa ya mwaka 2017 inaonesha Ugiriki ina watu milion 10, mji mkuu wa nchi hii unaitwa Athens na asilimia kubwa ya ardhi ya nchi hii ni milima.

Kauli mbiu ya nchi hii ni "UHURU AU UMAUTI".

Ugiriki ndio nchi inayoongoza duniani kwa raia wake kufanya mapenzi sana yaani namba moja Ugiriki ikifuatiwa na Brazil.

Lugha ya kigiriki ndio lugha kongwe zaidi duniani inayoandikwa ambayo bado inatumika, Lugha hii ya kigiriki imetumika zaidi ya miaka 5000 iliyopita lakin bado inatumika hadi leo katika maandishi.

Jina halisi la ugiriki ni UYUNANI kwa hiyvo Ugiriki sio jina halisi la nchi ya Ugiriki.

Michezo ya olimpiki ilianzia nchini Ugiriki.

Neno ''Music" limetokana na neno jina 'Muses' ambalo ni jina la Mungu wa sanaa katika imani za wagiriki wa kale.

Watalii wanaotembelea nchi ya Ugiriki kwa mwaka ni wengi kuliko raia wenyewe, raia wa Ugiriki ni milion 10 lakini kwa mwaka wanapokea watalii milion 16.

Raia wa ugiriki ni lazima kupiga kura wala sio hiyari kama ilivyo nchi zingine.

Ugiriki ni miongoni mwa nchi zinazozalisha mafuta ya mzeituni kwa wingi duniani, na kuna mizeituni iliyopandwa tokea karne ta 13 hadi leo bado inatumika kuzalisha mafuta

Mji mkuu wa Ugiriki ndio mji mkongwe zaidi Ulaya, ulianza kukaliwa na watu miaka 7000 iliyopita na ndio kitovu cha ustaarabu wa Ulaya siasa, falsafa, michezo, hesabu, fasihi, historia na nadharia mbali mbali

Ugiriki ina visiwa zaidi ya 2000 lakini ni visiwa 170 tu ndio vinakaliwa na watu

Archimedes, Pythagoras, Apollonius, Plato, Aristotle, Hypocritos, Euclid wote hawa ni wataalamu wa Ugiriki walioacha athari kubwa duniani.

Alexander The Great ndio kiongozi wa kwanza wa kigiriki kuweka sura yake kwenye sarafu ya Ugiriki, kabla ya hapo waliweka sura ya miungu yao

Nchi ya Ugiriki ndio ina kiwango kidogo cha talaka barani Ulaya na pia ndio nchi yenye kiwango kikubwa cha utoaji mimba kwa bara la Ulaya.

Ugiriki ndio nchi ya kwanza kutengeneza majalala ya manispaa, hayo yalifanyika miaka 500 kabla ya kuzaliwa yesu kristo.

Ugiriki ni nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya tangu 1981.

Hii ndio Ugiriki, Dola kiranja ya 4 ya dunia ambayo ndio mama wa Ulaya...

Kwa kupata makala Zaidi wasiliana na Mimi WhatsApp 0679555526/0765026057 uungwe group la Maktaba Kuu kwa gharama ya Tsh 3000/=.

Ukinakili kazi zangu kumbuka kufanya acknowledgment.
Wako Mjoli wa Historia na diplomasia ya ulimwengu.

Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu
Copyrights of this article reserved
written by Comred Mbwana Allyamtu
•Napatika Kwa mawasliano
Comred Mbwana Allyamtu

Kwa Tanzania
+255679555526 (WhatsApp).
+255765026057(Whatsapp).
Email-mbwanaallyamtu990@gmail.com

Copyright 2022, All Rights Reserved.

Maktaba Kuu.View attachment 2446823View attachment 2446821View attachment 2446820View attachment 2446822View attachment 2446824View attachment 2446825View attachment 2446827View attachment 2446826
FB_IMG_1671030131303.jpg
 
... ilikuwa nchi ya miungu haswa; haikutofautiana sana na Rumi na makureshi wa Makkah wakiabudu miungu nyakati hizo. Mungu wa kweli aliabudiwa na wana Israel tu.
Na pia inadaiwa miungu huabudiwa hadi sasa. Ndio maana pale Athens ukifika Kuna sanamu nyingi sana karibia Kila public building au sehemu za makutano ya barabara na zikiwa na maana yake spesho
 
Enzi ya utawala wa ottoman, sehemu walizotawala wameacha athari ya dini ya kiislamu,imekuwaje ugiriki ambayo pia imetawwliwa na Ottoman kusiwepo na hiki kitu? Umeelezea 93% Ni wakristo was dhehebu la Orthodox. Wajuzi naomba majibu.

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Enzi ya utawala wa ottoman, sehemu walizotawala wameacha athari ya dini ya kiislamu,imekuwaje ugiriki ambayo pia imetawwliwa na Ottoman kusiwepo na hiki kitu? Umeelezea 93% Ni wakristo was dhehebu la Orthodox. Wajuzi naomba majibu.

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
Hili swali linafikirisha Sana,au wenyewe kwenye strategy zao kiutawala suala la kusambaza dini yao haikuwa kipaumbele.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom