Je, asili ya majini ni ipi?

Je, asili ya majini ni ipi?

Sijakuelewa pepo msafi ndo una manisha nini kwahiyo kuna shetan mwema na shetan mbaya yaan kuna shetan mcha mungu au mimi sijakuelewa ndugu
Mada ni majini,jini akiwa mbaya ndio anaitwa shetani.Mnaposema pepo mchafu,làzima kutakuwapo na kinyume chake,kwa nini asiitwe pepo tu.
 
Kwani vitabu hivi viwili (Quran na Bible) vinasemaje kumuhusu Shetani? Je vyote vinasema kuwa Shetani ibilisi, hakuwahi kuwa mchamungu? Dhambi gani ilimtoa uchamungu wake?

Je wanajeshi wanaohasi wataendelea tu kuitwa wanajeshi au waasi? Shetani ibilisi=mpinzani muasi.
Huyo jamaa Uhuru jr sijui anauliza maswali kujifunza, kukupima kama unajua au kubishana? Kwa kweli simuelewi huyu jamaa!!
 
Sasa hao wafuasi wake huwa wanaongezeka au wale wale tu aliyoshushwa nao?

Na umesema alijiona anatosha kupambana na mungu kwa sababu ya nguvu alizopewa, je nini hasa alikuwa akikitaka hadi ikafikia kutaka kupambana na mungu?
Nyoka wa kike na wa kiume wakiingialana hutaga mayai na kuangua nyoka, hapo tayar nyoka wameongezeka, na wala nyoka akitaga mayai haangui kunguru

Kama majini huzaana basi hao waasi hawezi kuwa walewale wameongezeka
 
Kama majini huzaana ina maana hao wanaozaliwa nao pia moja kwa moja huwa ni waasi? na cha kunichanganya zaidi ni hiyo asili yao ya kuwa ni malaika.
 
wewe mimi nadhani hata bible ya haswa huisomi, unasikia na wewe unasema bila ya hata kutumia akili yako hata chembe.
ngoja nikupe shule kidogo.
Mwenyezi Mungu aliumba Malaika, majini na binaadamu. Na wote hawa kawaumba kwa ajili ya kumtumikia yeye.
Malaika waliumbwa kwa nuru, Majini kwa moto na binaadamu kwa udongo.
Katika Malaika hawa ni special wameumbwa na hawamuasi Mwenyezi Mungu kamwe, ni wenye kuabudu tuu.
Binaadamu na Majini sisi ndio tulokuwa na Mitihani maana ndio tupo hapa ulimwenguni,
tulichoumbiwa ni kumuabudu Mwenyezi Mungu. Na atakaemuasi ikiwa jini au binaadamu basi Mwenyezi Mungu hatamuacha siku ya mwisho atamuingiza motoni, na ikiwa atafuata maarisho ya Mungu ikiwa jini au binaadamu akitaka mwenyewe Mungu atamuingiza peponi.
Sasa ikiwa jini au binaadamu atamuasi Mwenyezi Mungu huyo ndio anakuwa shaytani. Maisha yao ya kuzaliana kama sisi tunavyozaliana ila tumetofautiana na vyakula vyao na makaazi yao wanayoishi.
Na hawana nguvu yoyote ile ya kusema kuwaogopa, Mtume Suleiman yeye alipewa ufalme wa watu, majini, wanyama, ndege, upepo N.k Ni ulfalme ambao alimuomba Mwenyezi Mungu asijempa yoyote badala yake.
Na walikuwa chini ya amri ya Mtume Suleiman aliwadhibiti sawa sawa.
Haya yamo ndani ya Quran tukufu.
binaadamu hutakiwi kuwaogopa kabisa wao ni viumbe wameumba kama sisi, na wengine huwaogopa binaadamu haswa.
Na binaadamu hatakiwi kuyaingilia katika maisha yao na wao hawatakiwi kutuingilia katika maisha yetu. Ila kama utawaingilia na kutaka kujua zaidi na kuwafatilia utaishia katika shirki ambayo itakupeleka kuunguzwa na Mwenyezi Mungu.

TATIZO BAADHI YA WASIOKUWA WAISLAM WANAKURUPUKA SANA NA KUTOA MAJIBU AMBAYO HATA AKILINI HAYAINGII, BINAADAMU SOMA MWENYEWE UELEWE USIKUBALI KUHADITHIWA TUU.
KWA NGUVU ZA NANI KWA NGUVU ZA NANI TOKA HAMNA KITU HICHO NI KIINI MACHO TUU CHA KUCHEZEWA.
MWENYE UWEZO WA KUMTOA JINI AKIKUSIBU NI MWENYEZI MUNGU PEKEE YAKE.
KUNA VISOMO KATIKA QURAN UNASOMA KAMA AKIKUPATA, NA JINI HAMPATI MTU AMBAE AMEJIWEKA MBALI NA MAMBO AMBAYO MWENYEZI MUNGU AMEHARAMISHA.
KAMA MTU ANASEMA SHEIKH ANA MAJINI NI MUONGO, KUNA BAADHI YA WATU HUWAFUTILIA HAWA MAJINI AMBAO KWA MAJINA WANAITWA WAISLAM ILA UNAKUWA USHAJIVUA KATIKA UISLAM IKIWA WEWE KAZI YAKO KUYAFUGA KWA AJILI YA SHIRKI.
HAKUNA USHIRIKA WOWOTE UNAOHUSIANA UISLAM NA MAJINI, NI KUWA ATI WAISLAM WANATUMIA MAJINI, MSIDANGANYWE MKADANGANYIKA.

NI KATIKA QURAN KILA KITU KIMO WATU WAACHE UVIVU WASOME
Seliselina naomba nikusahihishe kidogo ktk bible hakuna sehemu palipoandikwa kuwa Mungu aliumba shetani,big NO! Ila Mungu aliumba malaika,malaika walipoasi ndo wakaitwa mashetani.....
 
Seliselina naomba nikusahihishe kidogo ktk bible hakuna sehemu palipoandikwa kuwa Mungu aliumba shetani,big NO! Ila Mungu aliumba malaika,malaika walipoasi ndo wakaitwa mashetani.....
Hao hao,aliowaumba ndio walioasi.Kwa hiyo kawaumba Yeye.
 
Mada ni majini,jini akiwa mbaya ndio anaitwa shetani.Mnaposema pepo mchafu,làzima kutakuwapo na kinyume chake,kwa nini asiitwe pepo tu.
Ndugu mimi cha kukushauli ni kitu kimoja acha kusali pamoja na majini maana watenda zambi majini mda mwingine hujifanya malaika ili wakunase na kukuingiza katika mtego wao maana wenyewe hawana tena nafasi ya kutubu lengo lao ni kuudanganya ulimwengu na kuwapotosha wana damu
 
Ni uasi gani hao malaika waliufanya kwa mungu?

Na je,idadi ya hao malaika waliyomuasi mungu huwa haipungui wala kuongezeka?
Kuamin na kujarib kujifananisha na aliewaumba na kukataa kumsujudia binadamu ilihali wanamwona kaumbwa kwa udongo tu wakat wao wameumbwa kwa moto
 
Tofauti ya pepo na shetani... Pepo wanamwabudu shetan yaan ndio kama mungu wake,na pepo hawez kukaa sehem au kusanyiko linalomuhusu mungu,,litaruka ruka tu na kukimbia Ila shetan anaweza kukaa penye kusanyiko fakatifu tena hata hao viongoz wa dini zetu wanaweza kuwatumia shetan kabsa black tatzo na hamtajua,Ila pepo hawez kukaa sehem penye uwepo wa mungu.. N mwoga na dhaifu
 
Hawajielewi tu hao,pale wanaposema PEPO WACHAFU,lazima kutakuwa na kinyume chake PEPO WASAFI.Mbona hawesemi Malaika wasafi,wanasema malaika tu,kwa sababu hakuna kinyume chake.
Kwa hiyo wajuwe,ikiwa wapo Pepo wachafu na Pepo wasafi watakuwako.
Tatizo kitabu chao,kimetafsiriwa kutoka mlolongo mrefu wa lugha ya asili,kila tafsiri inavyoongezeka,ndio vitu vingi vinaachwa,kutegemea na ugumu wa kutafsiri.
Malaika wote ni wajumbe wa mungu,,,na wote wana ubin wa mungu,,, Micha'El,, Gbrie'El hii El ni kifupi cha Eloheem ambapo eloheem ni mungu
 
Hao malaika walimuasi mungu kwa jambo lipi yani ni uasi gani waliyoufanya kwa mungu?

Na kwanini wameitwa majini au mapepo badala ya kuendelea kuitwa tu malaika,kwani neno jini au pepo lina maana gani hadi wakaitwa hivyo?

Na ina maana hao majini wana sifa zote za malaika kama walizonazo malaika wengine ila tofauti yao wao walimuasi mungu tu?
Ndg hao malaika wakiongozwa na mkubwa wao lusifer ni mara baada ya Mungu kumuumba Adamu,akamwambia Adamu ntakuletea msaidizi wa kufanana na ww....Ndipo akamwambia Adamu na tuumbe mtu kwa mfano wetu! Hii kauli haikumpendeza lusifer kwani yy wakati huo alikuwa ndo malaika mkuu,akahoji kwann hakushirikishwa? Ndipo alipotangaza uasi na Mungu kuna wachache waliomfuata na wengine hawakuasi,ndo hao akina Gabriel na wengineo kwa hiyo neno shetani limekuja baada ya uasi lkn walikuwa malaika wazuri tena lusifer alikuwa mkuu wao!
Kuhusu kuwa na nguvu ndio wanazo lkn za giza ndo hawa unakuta mtu ana pepo la ngono,la ulevi nk,naomba niishie hapo!
 
Ndugu mimi cha kukushauli ni kitu kimoja acha kusali pamoja na majini maana watenda zambi majini mda mwingine hujifanya malaika ili wakunase na kukuingiza katika mtego wao maana wenyewe hawana tena nafasi ya kutubu lengo lao ni kuudanganya ulimwengu na kuwapotosha wana damu
Ndio ulivyokaririshwa huko kwenye nyumba zenu za ibada?Jini ni kiumbe,na ni tofauti na binadamu,ataswali vipi na binadamu.Jini anamuogopa binadamu,hawezi kusogea sehemu binadamu yupo.Kama unavyoona wanyama wa porini hawasogei,binadamu walipo,mbali ya kuwa na wao pia ni viumbe.
 
Malaika wote ni wajumbe wa mungu,,,na wote wana ubin wa mungu,,, Micha'El,, Gbrie'El hii El ni kifupi cha Eloheem ambapo eloheem ni mungu
Kwa hiyo malaika ni malaika,lakini pepo wapo wachafu,na wasafi pia wapo.
 
The most common cause of stress is dealing with people who are radical Muslim with terrorism mentality like yours. Burn in hell with your 72 virgins in heaven.

Huwa ndo maana sipendi kujadili mambo ya dini ,end of the day lazma muishie kwenye mazungumzo ambayo si mazuri kama haya .
My advice is ,faith is something personal ,very personal ,so you must be careful in characterizing others faith .
 
Seliselina naomba nikusahihishe kidogo ktk bible hakuna sehemu palipoandikwa kuwa Mungu aliumba shetani,big NO! Ila Mungu aliumba malaika,malaika walipoasi ndo wakaitwa mashetani.....
Neno shetani lina maana gani hadi wakaitwa hivyo?
 
Ndg hao malaika wakiongozwa na mkubwa wao lusifer ni mara baada ya Mungu kumuumba Adamu,akamwambia Adamu ntakuletea msaidizi wa kufanana na ww....Ndipo akamwambia Adamu na tuumbe mtu kwa mfano wetu! Hii kauli haikumpendeza lusifer kwani yy wakati huo alikuwa ndo malaika mkuu,akahoji kwann hakushirikishwa? Ndipo alipotangaza uasi na Mungu kuna wachache waliomfuata na wengine hawakuasi,ndo hao akina Gabriel na wengineo kwa hiyo neno shetani limekuja baada ya uasi lkn walikuwa malaika wazuri tena lusifer alikuwa mkuu wao!
Kuhusu kuwa na nguvu ndio wanazo lkn za giza ndo hawa unakuta mtu ana pepo la ngono,la ulevi nk,naomba niishie hapo!
Neno shetani lina maana gani?
 
Mada ni majini,jini akiwa mbaya ndio anaitwa shetani.Mnaposema pepo mchafu,làzima kutakuwapo na kinyume chake,kwa nini asiitwe pepo tu.
Hivi kumbe shetani ni kila jini mbaya? Eti mimi huwa najua shetani ni shetani na jini ni jini. Kwa hiyo kumbe shetani hawezi kuwepo hadi jini abadilike toka kuwa mzuri na awe mbaya ndio kuwe na shetani?!
 
Back
Top Bottom