wewe mimi nadhani hata bible ya haswa huisomi, unasikia na wewe unasema bila ya hata kutumia akili yako hata chembe.
ngoja nikupe shule kidogo.
Mwenyezi Mungu aliumba Malaika, majini na binaadamu. Na wote hawa kawaumba kwa ajili ya kumtumikia yeye.
Malaika waliumbwa kwa nuru, Majini kwa moto na binaadamu kwa udongo.
Katika Malaika hawa ni special wameumbwa na hawamuasi Mwenyezi Mungu kamwe, ni wenye kuabudu tuu.
Binaadamu na Majini sisi ndio tulokuwa na Mitihani maana ndio tupo hapa ulimwenguni,
tulichoumbiwa ni kumuabudu Mwenyezi Mungu. Na atakaemuasi ikiwa jini au binaadamu basi Mwenyezi Mungu hatamuacha siku ya mwisho atamuingiza motoni, na ikiwa atafuata maarisho ya Mungu ikiwa jini au binaadamu akitaka mwenyewe Mungu atamuingiza peponi.
Sasa ikiwa jini au binaadamu atamuasi Mwenyezi Mungu huyo ndio anakuwa shaytani. Maisha yao ya kuzaliana kama sisi tunavyozaliana ila tumetofautiana na vyakula vyao na makaazi yao wanayoishi.
Na hawana nguvu yoyote ile ya kusema kuwaogopa, Mtume Suleiman yeye alipewa ufalme wa watu, majini, wanyama, ndege, upepo N.k Ni ulfalme ambao alimuomba Mwenyezi Mungu asijempa yoyote badala yake.
Na walikuwa chini ya amri ya Mtume Suleiman aliwadhibiti sawa sawa.
Haya yamo ndani ya Quran tukufu.
binaadamu hutakiwi kuwaogopa kabisa wao ni viumbe wameumba kama sisi, na wengine huwaogopa binaadamu haswa.
Na binaadamu hatakiwi kuyaingilia katika maisha yao na wao hawatakiwi kutuingilia katika maisha yetu. Ila kama utawaingilia na kutaka kujua zaidi na kuwafatilia utaishia katika shirki ambayo itakupeleka kuunguzwa na Mwenyezi Mungu.
TATIZO BAADHI YA WASIOKUWA WAISLAM WANAKURUPUKA SANA NA KUTOA MAJIBU AMBAYO HATA AKILINI HAYAINGII, BINAADAMU SOMA MWENYEWE UELEWE USIKUBALI KUHADITHIWA TUU.
KWA NGUVU ZA NANI KWA NGUVU ZA NANI TOKA HAMNA KITU HICHO NI KIINI MACHO TUU CHA KUCHEZEWA.
MWENYE UWEZO WA KUMTOA JINI AKIKUSIBU NI MWENYEZI MUNGU PEKEE YAKE.
KUNA VISOMO KATIKA QURAN UNASOMA KAMA AKIKUPATA, NA JINI HAMPATI MTU AMBAE AMEJIWEKA MBALI NA MAMBO AMBAYO MWENYEZI MUNGU AMEHARAMISHA.
KAMA MTU ANASEMA SHEIKH ANA MAJINI NI MUONGO, KUNA BAADHI YA WATU HUWAFUTILIA HAWA MAJINI AMBAO KWA MAJINA WANAITWA WAISLAM ILA UNAKUWA USHAJIVUA KATIKA UISLAM IKIWA WEWE KAZI YAKO KUYAFUGA KWA AJILI YA SHIRKI.
HAKUNA USHIRIKA WOWOTE UNAOHUSIANA UISLAM NA MAJINI, NI KUWA ATI WAISLAM WANATUMIA MAJINI, MSIDANGANYWE MKADANGANYIKA.
NI KATIKA QURAN KILA KITU KIMO WATU WAACHE UVIVU WASOME