Je, asili ya majini ni ipi?

Je, asili ya majini ni ipi?

Umeukana uislamu hapo, Quran tukufu inasema ndugu wa muislamu ni muislamu mwenzake, kiaje sasa waislamu wasiwe na ushirikiano na mafungamano mkuu?
Kivipi mkuu? Sijakuelewa vyema hapo.
 
Swadaktaaaaaaaaaaaaa!!
Mlitakiwa mseme hamna mafungamano na majini waovu tu si yale mema, haiingii akilini kwa kondoo wa kundi moja na mchungaji mmoja wasiwe na mafungamano. Hata mkijitetea hivyo, ni nini tofauti ya jini jema na ovu? Yote yanaamrisha swala na yote yalioko ktk uislamu, tofauti ni ipi hapo?
 
Hapa ndo nilipokuwa nataka ufike, umefika. Jambo moja tu nakuomba, kuwa mwerevu na punguza munkari tufundishane jambo hapa.

Mi ni mwenyeji wa mikoa ya pwani ya Tz. Kuna vitu tusibishane kwakuwa nimeishi navyo na kuvishuhudia kwa macho tena hata kwa baadhi ya wana ukoo wangu.

Uislamu unafundisha ukristu ni upotofu,, walopotea. Kundi la ushetani. Dhambi ni zao la shetani mkuu.

Majini maovu tu ndo humuingia mwanadamu, ni kauli yako na ya uislamu, na ya waislamu wengi wala we si wa kwanza kunena hivyi.

Swali, kwanini kila jini limuingialo mwanadamu, humtumikisha kuutii uislamu kwa kutimiza yote ya uislamu wakati lenyewe ni ovu la kishetani? Kila mwenye majini lazima aitii ijumaa, ramadhani afunge, akae mbali na pombe, asile nguruwe, aswali swala tano, awashe udi, anene kiarabu (watetezi wanasema si kiarabu bali lugha ya kijini, lakini mashehe na si mapadri wanayoielewa) avae kama wavaavyo waislamu, mida yao ni mida ya swala ktk uislamu, why?

Mi nilitarajia kwakuwa ni maovu na ukristu ni uovu yangefungamana na yakikristu why? Hapa ndipo wakristo wanapodhani Allah ni Lucifer ujuwe? Nifundishe mkuu wangu, nko mweupe kabisa, huru kujifunza kitu kipya, na ntakutumia kwa mengi. Hope sijakukwaza.
Kuna watu wanajifanyisha wana majini,au wamevamiwa na jini.Huwa wana lengo lao fulani.Wapo wanaojifanya wana jini au majini,kwa kujifanya jini anataka pete ya dhahabu au jini ataka niolewe na fulani au jini anataka pombe.Hawa si wa kweli,wanatunga wao wenyewe kwa maslahi yao.
Jini wapo pia wanaongea kimasai,kingido,kiingereza,kijerumani,lakini ukiwa umebobea katika lugha hizo pamoja na hicho kiarabu utakuta lugha inayongelewa ni broken tupu,jaribu kuwa jaribu na hawa wanaosema wana majini utaelewa.
Utasikia jini anasema tuko wengi kwa huyu kiti,ni uongo mtupu,IMA yule mtu anajifanyisha hivyo au pepo mchafu anajifanya wako wengi,kwa kubadilisha sauti na lugha.
 
Huu mjadala utaishia kwa matusi kutokana na yofauti ya Imani.
Waislam wanaamini Mungu ameumba
1. Malaika (ambao hawaasi wao hutii amri tu)
2. Majini na
3. Binadam (majini na binadam wamepewa free will) kwamba wakitaka wafiate ukweli anaoambiwa au waasi)
Wakiasi wanakuwa mashetani na wataadhibiwa kama wakifa hawajatubu.

Wakristo wanaamini
1. Malaika ambao baadhi yao huwa wanaasi na wanakuwa Majini ( contrary na mafundisho ya uislam)
 
Jini mwema hamvamii mtu,anayemvamia mtu ni jini muovu.Katika kila viumbe wapo wema na wabaya.Kama binadamu wapo wema na wabaya.Binadamu mbaya,ndiye anayefanya vitendo vibaya,kama ujambazi,wizi,uporaji nk.Hata wanyama wapo wema na wabaya.Wanyama wabaya ndio wanaoshambulia wengine,na wapo wanyama hawashambulii wengine.
Kaka hapa swali ni kwanini haya majini maovu yafungamane na uislamu na si ukristo waovu wenzao? Yafurahie unywaji pombe, yawaamrishe wale wanaobamba kwenda kanisani, wasali ibada za Kikristu nk, uhalisia ni kinyume na haya, why?
 
Watu wanalishwa majani kama mbuzi kisa roho mtakatifu,watu watu wana nyweshwa hadi sumu kisa roho mtakatifu,wengine wanaambiwa wafanye masturbation kisa roho mtakatifu.

Ebwana huyu roho mtakatifu sasa balaa,maana hapo ndipo mkristo alipokamatwa hana ujanja chochote utakacho mwambia atafanya kwa sababu ya roho mtakatifu.

Si ajabu hata hizi ndoa za jinsia moja akawa ni yeye aliyeruhusu.
Sio kila mtumishi ana roho MTAKATIFU, wengine wanatumia hilo jina kudanganya waumini na nadhani wanaonekana kwa matendo yao
 
Mlitakiwa mseme hamna mafungamano na majini waovu tu si yale mema, haiingii akilini kwa kondoo wa kundi moja na mchungaji mmoja wasiwe na mafungamano. Hata mkijitetea hivyo, ni nini tofauti ya jini jema na ovu? Yote yanaamrisha swala na yote yalioko ktk uislamu, tofauti ni ipi hapo?
Tatizo ni kwamba kuwa muislamu na kuishi kiislamu ni mambo mawili tofauti;iwe kwa majini au wanadamu.
 
Elimu yako inakusaidia nini mkuu maana unasema majini hayaonekani wakati huo huo unadai Waislamu wanaswali na Majini,

Je waislam pia ni majini? mpaka waswali na majini

Je wewe uliyaona vipi hayo majini Kama sio uzushi na kushikiwa akili na wanaokuzidi uwezo wa kufikiri?
Kwa post hii umemaanisha wanaonizidi akili ni waislamu, hawa ndo walotuambia yote yawahusuyo majini. Kinyume na hapo, hakuna majini bali malaika waovu (waasi) na elimu ya Kikristu i prevail. Elimu yote kuhusiana na majini hivi tuijuavyo, wema na wabaya ni ya kiislamu. Uislamu ndo unaotangaza kuwa Suleiman aliyatawala hayo, Ukristu hata hauyajui majini.
 
katika Qurani SuratulAl- Ahqaf, (Kichuguu Cha mchanga) 46:29

“ Na wakumbushe tulivyokuletea kundi la majini kuja kwako kusikiliza Qurani. Basi walipohudhulia walisema (kuambiana: ‘Nyamazeni (msikilizeni maneno ya Mwenyesi Mungu’ na ilipokwiza’ na ilipokwiza somwa walirudi kwa jamaa zao wakiwaonya.”
 
Ndani ya Qurani kuna sura nzima inayoitwa surah ya majini (Mashetani) hiyo ni surah ya 72. katika Surah hiyo inasema 72:1-3, 14 “ Sema: imefunuliwa kwangu ya kuwa kundi moja la majini lilisikia Qurani likasema hakika tumesikia Qurani ya ajabu inaongoza katika uongofu. Kwa hivyo tumeiamini wala hatutamshirikisha yeyeote tena na Mola wetu na kwa hakika utukufu wa Mola wetu umetukuka kabisa. Hakujifanyia mke wala mwana ……

Nasi wamo miongoni mwetu waliosilimu Na wamo waliokengeuka. Waliosilimu hao ndiyo waliotafuta uwongofu.
 
Katika Qurani Suratul al kahf (Pango) 18:50

“ Na kumbukeni tulipowaambia Malaika, Msujudieni Adamu. Basi wakasujudia isipokuwa Ibilisi yeye alikuwa miongoni mwa majini na akavunja amri ya Mola wake ……”
 
Katika Tafsiri ya Qurani ya Imam Jalalaini Uk 6:151 anasema kuhusu majini

“ Hao ni watoto wa Ibilisi”

Hii ndiyo sababu hata Wanawake wa Kiislamu wakiwa katika kipindi cha hedhi hawaendi Msikitini kwa sababu mle ndani kuna majini na chakula cha majini ni damu.
 
Tafakari kwa hiyo sifa ya hayo majini au mashetani kwa ujumla ni kuwa “ hujaribu kwa bidii sana kuwa karibu na waumini (Waislamu) wale wanaosali, kufunga na kusoma Qurani” (Asili ya majini, DK. Ahmed H. Sakr Uk 28) Ndiyo maana baadhi ya Waislamu wao binafsi wasingependa kuwa waislamu lakini majini huwashurutisha kwenda kuswali.
 
Back
Top Bottom