Sangomwile
JF-Expert Member
- Aug 17, 2012
- 3,195
- 1,021
Ni kweli,andika tu 'Kesi ya uhaini 'mambo yanakuja,imedadavuliwa kwa kina.Nadhani kuna uzi humu ulishawahi kuletwa kuhusiana na suala hili la uhaini. Tuutafute
Ni kweli,andika tu 'Kesi ya uhaini 'mambo yanakuja,imedadavuliwa kwa kina.Nadhani kuna uzi humu ulishawahi kuletwa kuhusiana na suala hili la uhaini. Tuutafute
Movie atacheza Ray Kigosi akiwa na hangover ya kutosha ya maji pipa tisaNashukuru kwa tipp yako na maelezo yako. Ndio najua ile mission ilikuwa baab kubwa. Kungekuwa na uwezekano wa kuiona film yake, basi we acha tu.
Waliokuwa Dar enzi zile ndio walifaidi. Sisi wa mbali kaskazini basi ni kusikia sikia tu wakubwa enzi hizo wakipiga soga kijiweni. Ukiwakaribia wanakufukuza eti sio genge lako hili . Gazeti huna hela ya kununua. Mjomba ananunua daily news na sunday new ili asiombwe. Redio ipo kwa babu tu na balozi wa nyumba kumi kumi. Huitoa j'mosi mechi simba na yanga. Basi tabu tupu
Wahitaji wakiwa wengi nitawaletea .
Fafanua kidogo gazeti la rai la liniIlikuwa 1984/5. Tafuta simulizi yake katika gazeti la rai iliandikwa na kapt Eugene Maganga.
Ndiyo pale mkwajuni alipojaribu kuwatoroka maafisa usalama kwa kudadia pickup iliyokuwa ikitokea magomeni. Mtafute Mfalingundi ambaye alikuwa mkuu wa kituo cha salender bridge kwa maelezo zaidi. Bahati mbaya afisa aliyempiga kept Tamimu sasa ni matehemu.Tamim, nadhani aliuawa pale KINONDONI, au siyo?
Vijana wa zamani tulikuwa madhubuti..Pia vijana walifanikiwa kuteka ndege toka dar mpaka London...enzi hizo ....tofauti na hawa wa Dar.Mabibi na Mabwana,
Ningependa sana kupata historia na maelezo juu ya ile kesi ya uhaini. Siukumbuku mwaka ila nadhani ilikua 1982 nilikuwa msingi darasa la tatu hivi. Enzi zile ilikuwa vigumu kuuliza uliza maswali kwa kuogopa unaweza kukamatwa.
Sasa kwa vile sasa mambo yamebadilka ningependa kukumbushwa kidogo pale pamoja na mjadala hapa JF.
Shukran
Na moja wa maafisa usalama aliyekuwepo kwenye hizo kashikashi za kuwakamata makondoo wa jwtz ni Mabere Marando huyu wa chadema, alikuwa ni moto wa kuotea mbaliKomando kapten Tamim hakuuwawa na makomandoo wenzake bali na maafisa usalama baada ya zoezi la kumkamata mchana kweupe barabarani kuonekana linaelekea kushindwa na jamaa anaweza kutoweka
Hii ilikuwa kazi ya Mabere MarandoTamim, nadhani aliuawa pale KINONDONI, au siyo?
Huyo 1954 anajitia hofu bure tu... hakuna sheria yoyote unayovunja kv kila jina utakalotaja litakuwa kwenye kumbukumbu ya mahakama! Tatizo linaweza kuwa pale ambapo mathalani, mtuhumiwa X hakukutwa na hatia lakini wewe ukasema ambao walihusika ni pamoja na X! Lakini ikiwa X alikutwa na hatia na utokaji wake kifungoni ama ulikuwa ni kwa Msamaha wa Rais au kumaliza kifungo; basi sidhani kama kutaja ushiriki wa mtu kama huyo kunakiuka kifungu chochote cha sheria unless kama kifungu hicho kinakusudia kuzima sehemu ya historia ya Tanzania!!Mkuu 1954 sheria ya mtandao nimeikiuka kifungu gani? Niambie niandae utetezi.
Kulikuwa na Mr.Y. Huyu ndiye aliyewachinjilia baharini watuhumiwa. Alikuwa na kumbukumbu kuanzia mtaa, eneo siku, saa na eneo.Mawakili Waliotia Fora ni Hussein Muccadam(RIP) Murtaza Larkha, Jadeja Wote walikuwa wa Asia Tarimo, Mwanyika naLamwai Kitabu Cha Kesi Ya Uhaini Kilitoka Mwaka 1985 Kilichokuwa kimeandikwa na Marehemu Mnenge S. Suluja Mhusika Mkuu wa Washtakiwa alikuwa Thomas Lugangira au ‘Uncle Tom’
Wenzake walikuwa ni Hatibu Gandi au ‘Hatty Mac Ghee’, Kapteni Mohammed Tamim, Kapteni Mbogoro, Kapteni Christopher Kadege, Luteni Badru Rwechungura Kajaja na Kapteni Mapunda.
Wengine walikuwa ni Banyikwa na mkewe, Christopher Ngaiza, Zacharia Hans Pope , Kapteni Rodrick Rosham Robert , na Eugene Maganga Wengi nadhani ni Marehemu kwa sasa Lakini Pia Waliowahi kuiitwa Kwa Kuhusika Japo Hawakupatwa na Hatia ni Pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro wakati huo Marehemu John Mhavile(Baba wa Joyce Mhavile wa I TV /Radio One Kingine Kilichokuwa very interested kwenye kesi ni Baadhi wana Usalama kutumia Alphabet kuji indetify Badala ya Majina Yao yani walikuwa Mr. X Kama Mabere marando Dr. Hassy Kitine nadhani pamoja na Mizengo Pinda nk.Washtakiwa 9 Kati ya 16 Walihukumiwa kifungo cha maisha. Na Jaji Nassoro Mzava. Mwaka 1993 Walitoka kwa Sababu ya Tanzania kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi hivyo wafugwa wa kisiasa walipaswa kutoka Lakini Hatty MCghee alitoka akiwa mahtuti na akafariki Hospital MCghee aliwahi kutoroka pamoja na Uncle Tom lakini akadakiwa Horohoro Tanga.
Mwaka 1994 Nikiwa Idara ya uhamiaji makao makuu Nilikutana na zacharia Hans Pope akitafuta passport aende kutibiwa Figo South Africa lakini kaimu Mkurugenzi wa uhamiaji wakati huo Marehemu Peter Hassan Akampa makavu live kuwa huwezi kupewa passports sababu alikuwa chini ya uangalizi agizo kutoka Ikulu Hans Pope alinipa lift siku hiyo mpaka mikocheni pale talk of the town alikuwa na Mgari mbovu zile Land cruser Pick up sura mbaya yeye alikuwa akiishi Mwezi beach njia ya kuelekea Mediterranio hotel
Nyerere na Kawawa walifichwa na mlinzi wa baba wa Taifa ndugu Mbwambwo. Na kiongozi pekee aliyefika Kigamboni kuwaona ni Bhoke Munanka.Companero,
Si kweli kwamba Oscar ndiye aliyemwokoa na kumficha Mwalimu katika mapinduzi ya 1964. Huyu mtafiti amekosea. Nadhani Kawawa alikuwa na jukumu kubwa zaidi kumshawishi Mwalimu kujificha kuliko Kambona. Kambona hakujua alipofichwa Mwalimu.
Mkuu, Mwalimu alipoambiwa habari za kutaka kupindua serikali yake alipuuzia. Akaondoka kwenda Butiama na kusema hakuna anayeweza kufanya hivyo. Huku watu wakajipanga kweli kweli. Kama ulivyosema TIS ya wakati huo ilikuwa inafanyakazi kizalendo. Watoa habari nao walikuwa wakifanya kazi kizalendo sana. Baada ya kuwa jamaa wamejiandaa sasa kuanza kupanga watu wao kila eneo waliloliona mhimu, mwalimu alipopewa taarifa akiwa huko Butiama kuhusu hali halisi, ilibidi achukue ndege fasta kuja Dar. Ila jaribio hilo lilizimwa kishujaa na kwa weledi mkubwa mno.Duh, wewe ni kiboko, umeeleza vema, isipokuwa sina uhakika na hilo jina la LAMWAI. Ila ile incidence naikumbuka sana. Yule TAMIM alikuwa noma sana, kwa mapambano, alikuwa ni komandoo haswa. Sina hakika sana yule jamaa, nadhani alikuwa wa Tanga kama sijakosea, but I am not so sure...ila lile kundi (wahaini) lilikuwa infiltrated sana, wao wenyewe walikuwa hawajui, basi tu hatuwezi kusema mengi humu JF. Ila TISS ya wakati ule ilikuwa kiboko, walikuwa wanachapa kazi kweli kweli, wazalendo, committed to their profession. Walikuwa wanakuwa vetted kweli kweli, lakini siku hizi, aaah, sijui bwana....
Uzi upo lkn haukuelezea kwa kina kama huu. Huu uko deep zaidiNadhani kuna uzi humu ulishawahi kuletwa kuhusiana na suala hili la uhaini. Tuutafute