Jaribio la kugomea Sensa: Mwitikio wa Serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jaribio la kugomea Sensa: Mwitikio wa Serikali

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by BAK, Aug 18, 2012.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Aug 18, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,681
  Likes Received: 82,533
  Trophy Points: 280
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #FFFFFF"]
  [TABLE]
  [TR]
  [TD]Serikali yawaangukia Waislamu
  • Walimu 108 waenguliwa kwenye semina ya Sensa Dar

  na Waandishi wetu
  Tanzania Daima

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  [TABLE]
  [TR]
  [TD]WAKATI shinikizo la baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu kutaka kususia sensa likishika kasi, serikali imewaomba radhi Waislamu kutokana na matangazo yaliyorushwa na Kituo cha Televisheni ya Taifa (TBC), yaliyoonesha kwamba idadi ya Wakristo nchini ni kubwa kuliko Waislamu.

  TBC ilirusha matangazo hayo siku ya Sikukuu ya Muungano (Aprili 26) mwaka huu na kuonesha idadi ya Wakristo ni asilimia 52, Waislamu asilimia 32 na madhehebu mengine asilimia 14.

  Akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa TBC, Clement Mshana alisema kuwa matangazo hayo yalitolewa kwenye mtandao wa Wikipedia na kurushwa hewani kimakosa.

  Alisema baada ya kurushwa kwa matangazo hayo kimakosa, TBC walipokea barua nyingi kutoka Chama cha Wanataaluma wa Kiislamu Tanzania (Tanzania Muslim Professional Association) zikieleza kukerwa na taarifa hiyo.

  Mshana Alisema katika barua hiyo, chama hicho kilitaka ufafanuzi jinsi takwimu hizo zilivyopatikana na TBC iwaombe radhi Watanzania.
  Alisema Mei 15, TBC ilimwandikia barua Katibu Mkuu wa chama hicho cha Waislamu, Pazi Mwinyimvua na kuomba radhi kwa kasoro iliyotokea na kueleza kwamba shirika lake limemwonya mfanyakazi aliyerusha hewani takwimu hizo kimakosa.

  "Nichukue fursa hii tena kuwaomba radhi ndugu zetu wa dini ya Kiislamu kutokana na maumivu waliyopata kutokana na takwimu hizo. Na kwa kuwa huu ni mwezi mtukufu wa Ramadhani na moja ya mahitaji wakati wa mfungo ni kusameheana, naomba waumini wote wa dini ya Kiislamu wapokee kwa moyo wa upendo ombi hili la kuwataka radhi," alisema Mshana.

  Aliongeza kwamba kwa kuwa suala hili limehusishwa na sensa ya watu na makazi, anawaomba waumini wa dini ya Kiislamu kusamehe kilichotokea na washiriki katika sensa ya watu na makazi itakayofanyika Agosti 26, mwaka huu.

  Wakati serikali ikiendelea kuhimiza wananchi kushiriki sensa, kuna kundi la Waislamu limejitokeza kupinga tukio hilo.
  Kundi hilo limekuwa likipita sehemu mbalimbali nchini kueneza sumu ya kuwataka Waislamu wasishiriki sensa kwa madai kuwa serikali imelenga kuwabagua kwa kutangaza takwimu zinazoonesha Wakristo ni wengi zaidi ya Waislamu.

  Mmoja wa viongozi wa kundi hilo, Issa Sadick, hivi karibuni alizitaja baadhi ya sababu za kukataa kuhesabiwa kuwa ni serikali kuendelea kuwabagua Waislamu katika miradi mbalimbali ya maendeleo.

  Hata hivyo Sheikh Mkuu Mufti Shabaan bin Simba hivi karibuni aliwataka Waislamu kushiriki sensa na walipuuze kundi la masheikh linalozunguka nchini kutaka wasusie.

  Wakati huo huo, walimu 108 walioteuliwa kuhudhuria semina ya makarani wa sensa, wameenguliwa na nafasi zao kuzibwa na watu wengine.

  Utafiti wa gazeti hili umebaini kuwa, walioenguliwa ni walimu wa Kituo cha Mafunzo cha Sekondari Tambaza jijini Dar es Salaam.

  Kwa mujibu wa habari hizo, walimu hao wameenguliwa kutokana na kushindwa kufanya vizuri kwenye mtihani wa majaribio.
  Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili, baadhi ya walimu hao walisema wanapinga kuondolewa kwao kwani walikwishakubaliana katika mkataba wa malipo, na tayari walishaanza mafunzo kwa ajili ya kazi ya ukarani wa sensa.

  Walisema kuwa wahusika wamekuwa wakiwaleta ndugu zao na kuwapunguza walimu ambao tayari walishaanza mafunzo kwa siku nne sasa.
  Walimu hao walisema wanaitaka serikali iwalipe fedha zao za siku nne ambazo tangu waanze mafunzo hayo hawajalipwa.

  Taarifa hii imeandaliwa na Zawadi Chogogwe, Agness Newa na Stella Mushi.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Aug 18, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,681
  Likes Received: 82,533
  Trophy Points: 280
  Kweli nchi imeoza maana kama takwimu zilikosewa takwimu ambazo ziko accurate ni zipi kama zipo? Kama hakuna je Serikali ina mpango gani katika kuhakikisha inapata takwimu ambazo ziko accurate?
   
 3. MWILI NYUMBA

  MWILI NYUMBA JF-Expert Member

  #3
  Aug 18, 2012
  Joined: Jun 18, 2012
  Messages: 819
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35

  Shangaa na wewe mkuu,wengine tukihoji tunaitwa wadini.
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Aug 18, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,681
  Likes Received: 82,533
  Trophy Points: 280
  Hapa kwa maoni yangu si swala la udini hata kidogo. Kama hao TBC wamefanya makosa na kukubali makosa yao basi Serikali ina wajibu wa kuhakikisha inakuwa na takwimu ambazo ziko up to date na ambazo ziko accurate. Sioni kwanini hii sensa itakayofanyika August 26 isitumike katika kupata takwimu ambazo zitakuwa hazina utata hasa ukitilia maanani kwamba sensa hufanyika kila baada ya miaka 10 na wakati mwingine Serikali ilipokuwa na ukata ilifanyika tena baada ya zaidi ya miaka 10.

   
 5. M

  Mzi2 Mpole Member

  #5
  Aug 18, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Fanyani yanayowahusu.
   
 6. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #6
  Aug 18, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Imeoza haswaaa sio kidogo..........inasikitisha mno!
   
 7. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #7
  Aug 18, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Kwanini na wakristo wasiombwe radhi pia,kwani takwimu zilikosewa kwa wote!
   
 8. MWILI NYUMBA

  MWILI NYUMBA JF-Expert Member

  #8
  Aug 18, 2012
  Joined: Jun 18, 2012
  Messages: 819
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35


  Mkuu tulishawahi changia hivi hivi kama unavyosema wewe tukaitwa UAMSHO.Jamani hivi kujua idadi ya wananchi na dini zao ni dhambi?Kwanini kwenye vyombo baadhi vya serikali vinaweka kama bodi ya utalii wanaweka takwimu hizi hawakemewi lakini wakisema wengine wanaambulia kejeli na matusi? LIWALO NA LIWE hiyo sensa nyie hesabiweni tu mimi nitakuwa busy na shughuli zangu.
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Aug 18, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,681
  Likes Received: 82,533
  Trophy Points: 280
  Waliostahili kuombwa radhi kwa maoni yangu ni Watanzania wote bila kujali wanatoka katika dini ipi. TBC walikurupuka.

   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Aug 18, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,681
  Likes Received: 82,533
  Trophy Points: 280
  Wee acha tu sweetlady...Hii Serikali jamani!!! dah! madudu kila mahali hakuna hata moja la kusema hili lina ahueni....halafu wanajipiga kifua na kujiita eti Serikali sikivu!!!! mxchyuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #11
  Aug 18, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Unahangaika na mambo madogo ambayo hayakusaidii kuleta mkate mezani kwako,ukiugua wewe na familia yako huwezi tibiwa kwasababu ya kutetea dini yako,elimu yako na wanao inategemea wewe kuchapa kazi siyo dini yako!! Hivi kwa akili yako ni nini majukumu ya serikali?
   
 12. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #12
  Aug 18, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Hapo red fanya times 100 lol........yaani ni kichefuchefu kitupu...........yaani ningekuwa na uwezo mie ningejilipua na nanihiii
   
 13. MWILI NYUMBA

  MWILI NYUMBA JF-Expert Member

  #13
  Aug 18, 2012
  Joined: Jun 18, 2012
  Messages: 819
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35

  Hapo kwenye bold!Kuliko kushinda nyumbani kusubiri kuhesabiwa nitakuwa nachapa kazi kupata mkate wa siku mkuu.Nadhani labda haujaielewa vizuri sentensi yangu ya mwisho hapo ulipo ni-quote.
   
 14. t

  tusichoke JF-Expert Member

  #14
  Aug 18, 2012
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 1,286
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Yeye mshana alikuwa wapi kutamka hayo mapema anangoja mambo yanaharibika ndio anaibuka,na watu wa sensa ole wao waweke vipengere vinavyofanana na dini km vile kabila watatuambia kina faida gani ,maana wamesema dini kuwepo haina faida,kazi ipo
   
 15. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #15
  Aug 18, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Wakutoka vyama vya upinzani mnatakiwa mgomee sensa kwani ,wahuni wanataka kupata idadi ya kuwaua utapowadia uchaguzi mkuu ,Zanzibar wamesema watagomea sensa kwani polisi wa utawala wa ccm huwa wanawapunguza kwa kuwapiga risasi na mambomu ya machozi hata watoto wachanga ,hivyo senza haina faida ikiwa polisi wanafuta hesabu.
   
 16. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #16
  Aug 18, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,808
  Likes Received: 2,583
  Trophy Points: 280
  Nchi hii hatari! MWALIMU anafeli majaribio ya SIMPLE DATA ENTRY dodosa la sensa. CCM wametufikisha pabaya jamani, we have hit rock bottom it cant get any worse.
   
 17. hovyohovyo

  hovyohovyo JF-Expert Member

  #17
  Aug 18, 2012
  Joined: Jul 8, 2012
  Messages: 540
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Hizi takwimu wajameni, zinakuwa manipulated na watu wengi hata hao wanaokataa kuhesabiwa leo. Nimewasikia hata hao wanaoitwa wanazuoni ktk mihadhara wakidai sensa ya mwisho iliyokuwa na kipengele cha dini ilionesha waislamu ni asilimia 62. Nani ataamini ujinga na upotoshaji huu?? Wadanganyane wao ktk miamsho yao!!
   
 18. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #18
  Aug 18, 2012
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,169
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Hapo kwenye red::: 52%+32%+14%=?

  Nadhani jibu ni 98%..........Hii haikutakiwa kuwa 100% kweli?
   
 19. m

  mkigoma JF-Expert Member

  #19
  Aug 18, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 1,182
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  waislam wameshituka, walitaka kutengeneza propaganda ya kuwa wakristo ni wengi izoeleke hivyo ili wapate kuendelea kuwafanyia dhulma, big up waislam kazeni hivyo hivyo, ahesabiwi mtu labda paka.
   
 20. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #20
  Aug 18, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Sensa ni haki kwa kila Mtanzania.
  Haitapendeza ikidoda.
   
Loading...