Jaribio la kugomea Sensa: Mwitikio wa Serikali

Wa kulaumiwa ni hii Serikali ambayo imeshindwa kusimamia hii sensa ili iwe na mafanikio kwa kuleta chuki, dhidi ya Walimu ambao walikuwa wameshahudhuria mafunzo ya sensa, ili kuwakomoa na hivyo kuwatumia watu ambao hawakupata mafunzo halafu kujikanyagakanyaga kuhusu kuongezwa kwa kipengele cha dini za wahesabiwa au la.

Sensa ni haki kwa kila Mtanzania.
Haitapendeza ikidoda.
 
Sioni mantiki ya kuzuai kipengele cha dini ndani ya Sensa. Ukiangalia takwimu nyingi online zinaonyesha asilimia za dini. Dini haina madhala yeyote na wala haitapunguza au kuvunja kipengele chechoye cha katiba. Ni muhimu sana hasa kwa watalii wanapokuja nchini kuelewa sehemu na uwiano wa dini, hivyo waheshimu law of land. Mfano watalii toka meddle east wakienda sehemu kama Mbeya, watafahamu from online majority ni wakristo, kwa hiyo ni rahisi kujihadhari na Kiti moto. Sama wazungu wakitembelea Mafya.
Kipengele cha dini ni muhimu sana hasa ktk fani ya utalii .
 
Kwanini na wakristo wasiombwe radhi pia,kwani takwimu zilikosewa kwa wote!

hujui kwamba unapoambiwa ukoo fulani ni mkubwa ni neema?ama unaposikia kabila fulani wapo wengi tanzania ni sifa?ama watu fulani ni wengi ktk idara fulani kwamba ni prestage?kwanini hawakusema kua waislamu ni asilimi 52 na wakristo 34 ingelikua takwimu zimewapendelea waislamu hata wasingali kuja juu na wakristo sidhani kama wangalinyamaza
 
hivi utakapokuwa na mipango miji utatengaje maeneo ya makaburi bila kujua dini za wahusika nauliza tu?
 
JK alipokuwa anaambiwa nchi haitatawalika alidhani ni kuzuia misafara yake ,na watu kuandamana..sasa haya ndo dalili za wazi kuwa nchi haitawaliki..
 
hujui kwamba unapoambiwa ukoo fulani ni mkubwa ni neema?ama unaposikia kabila fulani wapo wengi tanzania ni sifa?ama watu fulani ni wengi ktk idara fulani kwamba ni prestage?kwanini hawakusema kua waislamu ni asilimi 52 na wakristo 34 ingelikua takwimu zimewapendelea waislamu hata wasingali kuja juu na wakristo sidhani kama wangalinyamaza

wakristo hawana hizo akili
 
Tanzania sasa inakaribia kuwa nchi ya kusadikika. Kupinga hadi sensa ambayo inafanyika kwa manufaa ya wananchi na mustakabali wa maendeleo ya watanzania. Ni ajabu kubwa kusikia watu wanapinga sensa ya watu na makazi. Inasikitisha sana. Watanzania sasa wanakuwa maarufu wa kupinga kila na kushinikiza serikali kufanya mambo ambayo katika hali ya kawaida hata haikustahili kuyapa nafasi ya kuyajadili. Tunaelewa wale Bush men wakiomba nyama ya nyani ili wahesabiwe kwa kuwa wanaishi porini na hata shule hawajui. Lakini sisi ambao tunajiita civilized, kupinga sensa ya nchi ni uhaini.
 
Nisaidieni mlioelewa please, TBC walirusha takwimu za uongo au walirusha takwimu kwa makosa? Kama Wikipedia imedanganya, walijuaje? Takwimu zimekuwa za uongo/makosa kwa sababu wahisilamu wamekasirika au?
 
Unahangaika na mambo madogo ambayo hayakusaidii kuleta mkate mezani kwako,ukiugua wewe na familia yako huwezi tibiwa kwasababu ya kutetea dini yako,elimu yako na wanao inategemea wewe kuchapa kazi siyo dini yako!! Hivi kwa akili yako ni nini majukumu ya serikali?

timbilimu, KWA SEREKALI KUJUA IDADI YA WATU WAKE, KWA TOFAUTI ZAO, SIO JAMBO DOGO. HILO NALO NIJUKUMU LA SEREKALI KUJUA, NCHINI MWAKE KUNA MAKABILA MANGAPI, IDADI YA WATU WAKULINGANA NA "RACE" ZAO, DINI ZAO NA TAMADUNI ZAO ILI KUEPUSHA MIGONGANO KATI YA JAMII HIZO. VINGINEVYO SEREKALI HIYO ITASHINDWA KUWAUNGANISHA WATU HAO KAMA TAIFA MOJA.

TAKWIMU SAHIHI NI MUHIMU KWA MAENDELEO YA TAIFA MAKINI.
 
Hizi takwimu wajameni, zinakuwa manipulated na watu wengi hata hao wanaokataa kuhesabiwa leo. Nimewasikia hata hao wanaoitwa wanazuoni ktk mihadhara wakidai sensa ya mwisho iliyokuwa na kipengele cha dini ilionesha waislamu ni asilimia 62. Nani ataamini ujinga na upotoshaji huu?? Wadanganyane wao ktk miamsho yao!!

Kwani hujawahi kusikia kuwa idadi ya waislam Zanzibar ni 99%? Na dini zingine ni 1% lini hiyo sensa imewahi kufanyika? Hilo la % hata Pinda amewahi kulisema Bungeni akimjibu Mch. Msigwa maswali ya papo kwa papo kuhusu mwezi wa SMZ kufunga hoteli na kukataza mtu yeyote kuonekana akila hadharani na kuhusu mavazi ya kujifunika mwili mzima. Mbona hatukusikia kwamba kuna dini yoyote iliyokanusha hilo la asilimia wakati haijafanyika sensa yoyote? Kwa kweli hii serikali ni dhaifu na ni legevu kabisa. Kama ndivyo basi ingefuta sensa yote isiwepo maana inaonekana kuwa mradi wa watu, wakati hizo takwimu hata zikipatikana kwenye maisha ya kawaida hakuna kinachobadilika. Cha msingi ni uongozi wa juu kuacha ufisadi na kujenga matabaka ya wenye nacho na wasionacho ili kipaumbele iwe kwenye mambo ya kuwasaidia wananchi kama afya, elimu, kilimo. Kwa serikali dhaifu hii sidhani kama tutafika mbali maana inawaweka huru matajiri na wenye pesa huku inawabana kwa njia zote walalahoi. Eee Mungu tusaidie.
 
Unahangaika na mambo madogo ambayo hayakusaidii kuleta mkate mezani kwako,ukiugua wewe na familia yako huwezi tibiwa kwasababu ya kutetea dini yako,elimu yako na wanao inategemea wewe kuchapa kazi siyo dini yako!! Hivi kwa akili yako ni nini majukumu ya serikali?
Unachanganya mada
 
hujui kwamba unapoambiwa ukoo fulani ni mkubwa ni neema?ama unaposikia kabila fulani wapo wengi tanzania ni sifa?ama watu fulani ni wengi ktk idara fulani kwamba ni prestage?kwanini hawakusema kua waislamu ni asilimi 52 na wakristo 34 ingelikua takwimu zimewapendelea waislamu hata wasingali kuja juu na wakristo sidhani kama wangalinyamaza

Kwani Zanzibar wanavyodai kuwa kuna waislam 99% na dini zingine 1% nani amefanya hiyo sensa? Umewahi kusikia wakristo Zanzibar wanalalamika? Kwanini dini zingine hawalalamiki huko zanzibar? Haya mambo yanawezekana endapo serikali ikiwa imara. Kujua idadi ya waislam na wakristo wala sio dhambi, pia sio kosa. Haiiongezei gharama zozote serikali ila ni kiburi na kutaka kuonekana kama inajua sana. Ingeongeza kipengele cha dini kwenye dodoso wala isingekuwa na shida yoyote.
 
Nisaidieni mlioelewa please, TBC walirusha takwimu za uongo au walirusha takwimu kwa makosa? Kama Wikipedia imedanganya, walijuaje? Takwimu zimekuwa za uongo/makosa kwa sababu wahisilamu wamekasirika au?

Kwa mujibu wa sheria ya takwimu nchini, taasisi pekee inayoruhusiwa kutoa takwimu za watu na dini zao ni National Bureau of Statistics. TBC wamechukua takwimu kwenye mtandao kama huu ambao kila mtu anaweza kupost, kuhariri na mengineyo. Hakuna kuuma maneno, takwimu hizo siyo sahihi.

Tupate somo wanahabari, kufanyia kazi mambo tunayoyaandika ili kuepusha madhara kwa jamii. Jamii ikichafuka ni hasara kwa wote.
 
Wanahabari fanyeni kazi kwa mujibu wa taratibu za kazi na sivinginevo,mtasababisha chuki miongoni mwa wanajamii ambazo azina msingi wowote
 
Back
Top Bottom